Nimemuacha ila kama najutia

Nimemuacha ila kama najutia

Mimi na yeye tumekubaliana tuishi pamoja mana pia tumezaa mtoto ,na amenihaidi atabadilika ila wazazi watia ngumu.
Hawawezi kukubali kirahisi tu,ungekuwa na binti ungewaelewa,kwani wao hawampendi binti yao?

La msingi mchukue mshenga mwende kuweka mambo sawa,mkubaliane namna ya kumaliza hiyo changamoto ya yeye kuacha mawasiliano na wapenzi wake wa zamani.
Na kama hujalipa mahari wende nayo kidogo uwapoze.huenda mahari hujatoa hata mia..
 
Habari za siku wapendwa.
Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwao wananitambua na michakato ya kutoa mahali nilishaianza kwa maana ya kishika uchumba ,kiasi kwamba wazazi wake walinikabidhi kuishi nae.

Nimekaa nae kwa muda wa miezi 3,katika kipindi hcho tumeishi kwenye ugomvi mwingi wa mambo mengi, ila kubwa kuhusu yeye kuwasiliana na x wake akidai mbona ww unawasiliana na wazazi wenzako kwa maana kabla ya kumuoa yy nilikuwa nimezaa na wanawake wawil kabla.

Nilimkata asiwasiliane,amfanye x wake ashindwe kumtafuta nilishindwa , usiku uo, aliniambia naweza mrudisha nyumbani nikamjibu sawa ,asubuh ilipofika nikamuona yuko bize anafanya usafi na kupika,nikamuuliza nikurudishe nyumban akajibu ndio,basi nikaitisha usafiri ili umbebe yy na vitu vyake.

Sasa iv ananiambia turudiane mana siku ile hakuwa na nia ya kurudi nyumban,nakuniambia ninakurupuka sana nilimjibu sikupenda kauli yake aliyokuwa akitoa mara kwa mara ya nirudishe nyumban.

Sasa nimeamua nimrudishe nyumbani mana nimegundua huwa anafanya ma x zake kama marafik zake nimemfuatilia ata sasa iv anawasiliana na ma x zake ,kipindi kile alikuwa 1 ila sasa kawarudisha wote,ingawa mawsiliano yao kwamba x wake wanamwitaji kimapenz ila yy kawafanya kama marafk.

Kumrudisha nyumbani wazazi wake hawataki ,na wazazi wake ndo wanaompa jeuri mana wanakiuwezo .Naomba ushauri wenu.
Ninyi ni wangoni ??
 
Mkuu hapo hujaoa bado unachezeshwa hiyo ngoma, vipi ukioa akijikuta ndio maza-hausi Kua mmeshakula viapo msiachane??

Siku zote mwanzo wa ngoma ni leelee, kama hiyo midundo michache imekushinda kimbia mapema utakuja kulia hapa jukwaani kila siku Kua unasaidiwa
 
Ngoma droo lakini?😅 Unawasiliana mzazi mwenza na yeye anawasiliana aliogusanisha nao vikojoleo ...

Lakini kwa ushauri tu hapo ngoma nzito hawezi kukujibu jeuri hivyo,maamuzi ni yako tafuta mwingine au kubali uishi naye Huku ukifahamu 80% wakupasha naye kiporo wapo.

Usisahau kutupa card tutajitahidi kufika kwenye harusi hata kupitia video call
 
Hawawezi kukubali kirahisi tu,ungekuwa na binti ungewaelewa,kwani wao hawampendi binti yao?

La msingi mchukue mshenga mwende kuweka mambo sawa,mkubaliane namna ya kumaliza hiyo changamoto ya yeye kuacha mawasiliano na wapenzi wake wa zamani.
Na kama hujalipa mahari wende nayo kidogo uwapoze.huenda mahari hujatoa hata mia..
Kwa majibu ya huyo mwanamke inaonesha hiyo changamoto haitoisha,atakubali tu mwanzo ili atimize lengo lake la kuolewa.
 
inasikitisha kuwa unashindwa kuamua Kama mwanaume.
Hatua ya Kwanza mtafutie laini mpya.mwambie sitaki uwe unawasiliana na watu nisiowataka.
 
Tulizana acha KUKURUPUKA. Anawasiliana na maex ili iweje?
Habari za siku wapendwa.
Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwao wananitambua na michakato ya kutoa mahali nilishaianza kwa maana ya kishika uchumba ,kiasi kwamba wazazi wake walinikabidhi kuishi nae.

Nimekaa nae kwa muda wa miezi 3,katika kipindi hcho tumeishi kwenye ugomvi mwingi wa mambo mengi, ila kubwa kuhusu yeye kuwasiliana na x wake akidai mbona ww unawasiliana na wazazi wenzako kwa maana kabla ya kumuoa yy nilikuwa nimezaa na wanawake wawil kabla.

Nilimkata asiwasiliane,amfanye x wake ashindwe kumtafuta nilishindwa , usiku uo, aliniambia naweza mrudisha nyumbani nikamjibu sawa ,asubuh ilipofika nikamuona yuko bize anafanya usafi na kupika,nikamuuliza nikurudishe nyumban akajibu ndio,basi nikaitisha usafiri ili umbebe yy na vitu vyake.

Sasa iv ananiambia turudiane mana siku ile hakuwa na nia ya kurudi nyumban,nakuniambia ninakurupuka sana nilimjibu sikupenda kauli yake aliyokuwa akitoa mara kwa mara ya nirudishe nyumban.

Sasa nimeamua nimrudishe nyumbani mana nimegundua huwa anafanya ma x zake kama marafik zake nimemfuatilia ata sasa iv anawasiliana na ma x zake ,kipindi kile alikuwa 1 ila sasa kawarudisha wote,ingawa mawsiliano yao kwamba x wake wanamwitaji kimapenz ila yy kawafanya kama marafk.

Kumrudisha nyumbani wazazi wake hawataki ,na wazazi wake ndo wanaompa jeuri mana wanakiuwezo .Naomba ushauri wenu.
 
Hao wazazi gani wanatoa mtoto kwa kishika UCHUMBA[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

MAZWAZWA
 
Aiseee... mwanamke amekosa busara..Ex unawasiliana nae Nini..Jamani
.Yaaani Mimi huwa nawashangaa eti tuliachana kwa AMANI..SAWA....sasa mnawasiliana Kitu GANI...?

Ptuuu.....SITAKI KABISA..
Huyu muache TU Kwanza UNASHINDANA VIPI NA Mwanaume...like how?
 
Jokajeusi Njoo huku Kuna mwana kazingua kila siku unasisitiza watu waoe bikra lakini yeye haelewi tayari Mungu kaishamuepushia huu ugonjwa wa kuoa wasio na bikra lakini yeye anataka kurudi
 
Una hakika hao watoto wote ni wa kwako?
Shida nimezaa nae huyu ni mtoto wangu wa 3,alinihaidi atabadilika,ananipenda hata biashara zake hutaka nizisimamie mimi ingawa tumeachana.
 
Hao wazazi gani wanatoa mtoto kwa kishika UCHUMBA[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

MAZWAZWA
Kishika uchumba milion 1,nimelipa bado tulisha zaa so waliona wanipe mahali watanibana kwenye ndoa.
 
ACHANA NAE.
AU KAMA VIPI MPE NAYE MIMBA USEPE ZAKO AWE WA TATU.
BAADAE KUSANYA WATOTO.....!

Ila nawe dada yako akifanyiwa hivyo au mwanao, USILAUMU.




Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
ACHANA NAE.
AU KAMA VIPI MPE NAYE MIMBA USEPE ZAKO AWE WA TATU.
BAADAE KUSANYA WATOTO.....!

Ila nawe dada yako akifanyiwa hivyo au mwanao, USILAUMU.




Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Na yeye pia nimemzalisha tiyar,ila nia yangu nikuishi nae mana ndio pekee nilimpenda,tofauti wa2 wa mwanzo .
 
Kama hawataki umrudishe achana nae.wazazi wameweka ngumu kwasababu hawakufurahishwa na maamuzi ya mwanzo kumrudisha mtoto wao kwao.
Wanaona unayumba katika kujisimamia kutatua changamoto ndogo ndogo za hapa na pale.
Ilikuwa vyema kama kuna jambo hamuelewani mngemuita mshenga aliyepeleka kishika uchumba awasuluhishe mkiwa kwenu bila wazazi wake kujua.
Kitendo cha kumrudisha kwao kilitakiwa kiwe cha mwisho,na kwakuwa umeshamrudisha kwao maana yake tayari mmefika mwisho.

Wazazi wake wapo sahihi, labda kama unataka arudi mchukue mshenga mwende mkaweke mambo sawa .wakikataa basi uchumba uvunjwe rasmi,kila mtu afanye yake.

We mwenyewe double fadher umezaa watoto wawili kwa wanawake wawili na hukuwaoa,au uliwaoa mkaachana, nawewe ipo shida mahali..
Yeye kuwasiliana na ma X unaita jambo dogo? Real?
 
Back
Top Bottom