Nimemuacha ila kama najutia

Nimemuacha ila kama najutia

Whk

Member
Joined
Oct 1, 2020
Posts
77
Reaction score
93
Habari za siku wapendwa.
Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwao wananitambua na michakato ya kutoa mahari nilishaianza kwa maana ya kishika uchumba, kiasi kwamba wazazi wake walinikabidhi kuishi nae.

Nimekaa nae kwa muda wa miezi 3, katika kipindi hcho tumeishi kwenye ugomvi mwingi wa mambo mengi, ila kubwa kuhusu yeye kuwasiliana na x wake akidai mbona wewe unawasiliana na wazazi wenzako kwa maana kabla ya kumuoa yeye nilikuwa nimezaa na wanawake wawili kabla.

Nilimkata asiwasiliane, amfanye x wake ashindwe kumtafuta nilishindwa, usiku huo, aliniambia naweza mrudisha nyumbani nikamjibu sawa, asubuhi ilipofika nikamuona yuko bize anafanya usafi na kupika, nikamuuliza nikurudishe nyumban akajibu ndio, basi nikaitisha usafiri ili umbebe yeye na vitu vyake.

Sasa hivi ananiambia turudiane maana siku ile hakuwa na nia ya kurudi nyumbani, na kuniambia ninakurupuka sana, nilimjibu sikupenda kauli yake aliyokuwa akitoa mara kwa mara ya nirudishe nyumbani.

Sasa nimeamua nimrudishe nyumbani maana nimegundua huwa anafanya ma x zake kama marafiki zake, nimemfuatilia hata sasa hivi anawasiliana na ma x zake, kipindi kile alikuwa 1 ila sasa kawarudisha wote, ingawa mawsiliano yao kwamba x wake wanamwitaji kimapenz ila yy kawafanya kama marafiki.

Kumrudisha nyumbani wazazi wake hawataki ,na wazazi wake ndo wanaompa jeuri mana wanakiuwezo .Naomba ushauri wenu.
 
Kama hawataki umrudishe achana nae, wazazi wameweka ngumu kwasababu hawakufurahishwa na maamuzi ya mwanzo kumrudisha mtoto wao kwao. Wanaona unayumba katika kujisimamia kutatua changamoto ndogo ndogo za hapa na pale.
Ilikuwa vyema kama kuna jambo hamuelewani mngemuita mshenga aliyepeleka kishika uchumba awasuluhishe mkiwa kwenu bila wazazi wake kujua.

Kitendo cha kumrudisha kwao kilitakiwa kiwe cha mwisho na kwakuwa umeshamrudisha kwao maana yake tayari mmefika mwisho.

Wazazi wake wapo sahihi, labda kama unataka arudi mchukue mshenga mwende mkaweke mambo sawa. Wakikataa basi uchumba uvunjwe rasmi, kila mtu afanye yake.

We mwenyewe double father umezaa watoto wawili kwa wanawake wawili na hukuwaoa, au uliwaoa mkaachana, na wewe ipo shida mahali..
 
Hmmmmm, nionavyo mimi hapo una changamoto, kumbuka hata kama ni ma x lazima kuna muda anawamiss tuu coz hakuna mtu ambaye huwa anatenda makosa muda wote hivyo lazima na yeye anawakumbuka kwa mazuri yao, and sometimes wakizoeana sana na wakakutana wanaweza wakarudia ile michezo @@, so chakufanya wewe ni kufanya lelote ili asiwe karibu na hao x zake,,

A good marriage ni huwa inaanza na 0:0
 
Hakuna urafiki wa mpenzi ulienae na x wake mzee analiwa/ataliwa sio mda
Kipato cha wazazi wake kinahusianaje na mahusiano yenu na ukimuacha icho kipato chao ndo kitakuathiri vipi mkuu em fafanua hapo
 
Daah! 0-0 maisha haya kuipata ngumu sana,
Haya mambo ndio joka jeusi anaongea kila siku.
Kikubwa uhai tu..
 
Mungu anakuepusha na mambo mabaya ya mbeleni wewe unajidai ndo una mapenzi saana..
kaa ukijua tabia mbaya zinazidi mtu akishakuwa ndani tayr, ilo ni trela tu subiri picha ukishamuoa

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna urafiki wa mpenzi ulienae na x wake mzee analiwa/ataliwa sio mda
Kipato cha wazazi wake kinahusianaje na mahusiano yenu na ukimuacha icho kipato chao ndo kitakuathiri vipi mkuu em fafanua hapo
Kuna ishu ya yy kwenda kushinda kwa wazazi wake ambayoa sikuipenda na wazazi wake niliwaambia siipendi hii tabia,ila chakushangaza siku asipoenda wanampigia simu aende akashinde kwao.
 
Jokajeusi, njooo huku mmoja tayari yamempata... huyu dada angekuwa bikra, I tin hilo la kuchat na ma-x wake lisingetokea.

Ila pole sana mkuu. Ushauri: Achana nae huyo dada kwako atakuwa amefwata vitu vizuri tu ila siyo upendo. Mwanamke anayekupenda hawezi kuwa anajibu hivo. Huyo si ridhiki.
poleeeeee
 
Mimi na yeye tumekubaliana tuishi pamoja mana pia tumezaa mtoto ,na amenihaidi atabadilika ila wazazi watia ngumu.
 
Kuna ishu ya yy kwenda kushinda kwa wazazi wake ambayoa sikuipenda na wazazi wake niliwaambia siipendi hii tabia,ila chakushangaza siku asipoenda wanampigia simu aende akashinde kwao.
Mkuu inaonekana uyo mwanamke anaujua udhaifu wako aisee mbona kama hauna sauti kwake ivi??
Yani kama mnalipiziana hivi jitahidi uwe jiwe yeye awe yai aisee bila ivo hata hao maex wake wataletwa ndani sasa
 
Jokajeusi, njooo huku mmoja tayari yamempata... huyu dada angekuwa bikra, I tin hilo la kuchat na ma-x wake lisingetokea.

Ila pole sana mkuu. Ushauri: Achana nae huyo dada kwako atakuwa amefwata vitu vizuri tu ila siyo upendo. Mwanamke anayekupenda hawezi kuwa anajibu hivo. Huyo si ridhiki.
poleeeeee
Shida nimezaa nae huyu ni mtoto wangu wa 3,alinihaidi atabadilika,ananipenda hata biashara zake hutaka nizisimamie mimi ingawa tumeachana.
 
Back
Top Bottom