Nelson nely
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 4,251
- 2,870
Huyu mzee mara ya kwanza tulikutana hapa mtaani nikiwa bado mgeni na bahasha yangu ya khaki mkononi.Ilikuwa mahala fulani napata kahawa hapa tegeta.Akanichangamkia sana halafu akaninunulia kahawa ya kutosha then akaniita pembeni akaniambia kuwa yeye ni mganga na jini wake amemuotesha leo aje mahali pale(kwenye kahawa)na atakutana na mtu ameshika bahasha,ana matatizo hivyo amsaidie.Nilimuelewa nikamshukuru na kumuomba mawasiliano yake kwa ahadi ningemtafuta.Sikumtafuta.
Mara ya pili tulikutana dukani akanambia "kijana mbona ulipuuzia?"...nijamdanganya na kumuahidi tena kumtafuta.Sikumtafuta.Sasa leo asubuhi nikiwa nimewahi kuamka na frustrations zangu nikakutana nae dukani tena akaniambia "kijana unajua una matatizo makubwa sana halafu unaleta upumbavu?"!
Hiyo kauli yake kiukweli sikuipenda nikajikuta limenitoka tusi kubwa sana.Yule mzee akaniangalia kwa huzuni halafu akaondoka.
Mimi huwa siwaamini hawa watu hasa wanaojiita wana majini,sasa nataka nimfate kwake nikavunjevunje matunguli yake yote kama anayo.