Nimemtafutia kazi bar mke wangu!

Nimemtafutia kazi bar mke wangu!

Maisha yakikaba hakuna kitu kinachoshindikana ilimradi pesa ipatikane,mwingine karuhusu mkewe afanye kazi baa na kamsisitiza mkewe aheshimu kazi wakati mwingine ameacha mke wake ameenda ulaya kwenda kusoma kwa muda wa miaka mitatu na hajui mke wake atazimuduje hisia zake,kwahiyo kila huyo anajua anavyokabiliana na maisha.
 
Mi naish na wazaz akin baba atak ata kuiskia iyo kazi kaniambia labda afe ndo niifanye ama vipi nitembeze vitumbua Sasa mi na vitumbua wap na wap jaman
 
Muombe mungu tuu akumbuke kutumia kondomu pindi uzalendo unapomshinda. Hata awe anakupenda kiasi gani sembuse kilichompeleka hapo ni shida ya pesa aaaa basi ataliwa tuu. Kikubwa strictly condom!
 
Mi naish na wazaz akin baba atak ata kuiskia iyo kazi kaniambia labda afe ndo niifanye ama vipi nitembeze vitumbua Sasa mi na vitumbua wap na wap jaman
Mtoto mzuri km wewe uuze vitumbua hapana aisee! Karibu pm tuulizane mawili matatu..
 
Na Wateja wa Bar za Sinza sio watu wa Utani .....
 
Wabongo kwa nini mnapenda kuchagua kazi, kwani hata akifanya kazi ikulu akiamua kuwa mama huruma kitu gani kitamzuia
 
Kazi ni kazi, cha ajabu nini mpaka uanzishe uzi?
 
Habarini,

Nimeoa na nina mtoto mmoja! Tunapendana sana na mke wangu! Nampenda nami naamini ananipenda.... Mimi nafanya kazi fulani hapa mjini inayo tuingizia kipato mm na mke wangu na kuweza kulea mtoto wetu! Kwa mapenzi nilio nayo kwa mke wangu nimeamua asikaee tuu nyumbani idol nimeamua nimtafitie kazi ya kufanya ambayo ni kupeleka vinywaji kwa wateja! Katiba BAR fulani maarufu hapa Dar ipo maeneo ya sinza!

mke wangu amekubari kwa mikono miwili na kwa moyo mweupe kufanya hiyo kazi! kila ikifika sa 12 jioni wakati mimi ninarudi toka kazini yeye ndio huwa anatoka kwenda kazini hadi sa 9 usiku muda mwingine sa 11 ndio hurudi nyumbani kutoka kazini! Maisha ya Magufuli yamekuwa magumu sanaa nashukuru Mungu anacho pata mke wangu si haba tukichanganya na changu basi machango mdogo wa mama Unaonekana na Maisha yanaenda! Mimi mara nyingi hutumia mda wangu kumsisitizia mke wangu na kumuelemisha umuhimu wa kazi na uzuri wa kufanya kazi kwa Juhudi na weledi! kubwa zaidi huwa namsisitizia mke wangu kuheshimu kazi yake! Aheshimu kazi kama anavyo niheshimu mimi

Nina imani Mungu atatusaidia katika maisha yetu nasi siku tutakuwa watu katika watu! Nawasihi wanaume wenzangu msichague kazi na wadada acheni kuchagua kazi! kikubwa ni kujitambua

Ngoja nimjulie hali mke wangu anaendeleaje na kazi nitarudi tena.......
Msisitize aifanye kazi yake kwa 'weledi mkubwa' ili ndoa iendelee kuwepo
 
Ushauri
Kama kweli unampenda mkeo na ndoa yako, basi mtafutie kazi nyungine au mpe mtaji afanye biashara
 
Jiandae kulea mtoto wa pili wa baba asiyejulikana
 
Mi naish na wazaz akin baba atak ata kuiskia iyo kazi kaniambia labda afe ndo niifanye ama vipi nitembeze vitumbua Sasa mi na vitumbua wap na wap jaman
Mrembo kama bakhresa anauza vitumbua,maandazi na chapati kwanini wewe uone soo badirika na chukua hatua uone fursa,
7581a60b4c3f0493ad56f4edbe4cd527.jpg
hapo naona ukuta haujasakafiwa ndio chumbani kwako?
e3b50ad24329b414f61ead836059211d.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom