konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,666
- 8,582
Wajuzi wa mambo naomba mnieleweshe hapa. Nimemsikia rais akiwaambia walinzi wake kuwa wasiwazuie watu wa rais wa Ethiopia kuingia ndani. Wakati tu wameingia Ikulu ndogo ya Chato, zikawa zinatokea zile pilikapilika za kupiga picha, rais Magufuli akasikika akiwaamrisha walinzi wake wasiwazuie watu wa rais wa Ethiopia, na ghafla tbc wakakata sauti, nadhani walikata sauti baada ya kuona labda anachokiongea rais hakitakiwi kusikiwa na public.
Hiki kitendo kimenifikirisha sana. Ina maana walinzi wa rais wa Ethiopia hawana nguvu ya kumlinda rais wao mpaka rais wetu awaamrishe walinzi wake wawachie? Au ulinzi wa marais kutoka nje huwa unakuwa chini ya walinzi wa rais mwenyeji? Maana imeonekana waliwekwa pembeni walinzi wa rais wa Ethiopia na walinzi wa rais wetu.
Mnaojua protoko za haya mambo naomba mnijuze.