Nimemsikia Rais Magufuli akiwaambia walinzi wake "Msiwazuie watu wake, watu wake waacheni waje"

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,498
Wajuzi wa mambo naomba mnieleweshe hapa. Nimemsikia rais akiwaambia walinzi wake kuwa wasiwazuie watu wa rais wa Ethiopia kuingia ndani. Wakati tu wameingia Ikulu ndogo ya Chato, zikawa zinatokea zile pilikapilika za kupiga picha, rais Magufuli akasikika akiwaamrisha walinzi wake wasiwazuie watu wa rais wa Ethiopia, na ghafla tbc wakakata sauti, nadhani walikata sauti baada ya kuona labda anachokiongea rais hakitakiwi kusikiwa na public.

Hiki kitendo kimenifikirisha sana. Ina maana walinzi wa rais wa Ethiopia hawana nguvu ya kumlinda rais wao mpaka rais wetu awaamrishe walinzi wake wawachie? Au ulinzi wa marais kutoka nje huwa unakuwa chini ya walinzi wa rais mwenyeji? Maana imeonekana waliwekwa pembeni walinzi wa rais wa Ethiopia na walinzi wa rais wetu.

Mnaojua protoko za haya mambo naomba mnijuze.
 
Ukitaka kuzuia Corona hapa nchi badilisha jina la huo ugonjwa badala ya Corona sema "Chadema" na ili watu wajikinge na walindwe mpaka nyumbani mwao sema Mbowe ya puani inauzwa wapi kila nyumba utakuta kuna polisi na mwanajeshi kuzuia Chadema isienee ambayo mda huu ndio korona na watu watavalishwa barakoa wakijua ni Mbowe huyo. Hapo walihisi walinzi wa raisi wa esiopia ni Red briged
 
Mambo mengine hayatuhusu , by the way pale ni ikulu ndogo nafasi nk, ushauri tu serikali ijenge ikulu ndogo yenye hadhi, jengo lile si mahususi na maalumu kwa ikulu ndogo.Kwa heshima ya mkuu wetu kuokoa garama za safari za nje.
 
Kiprotokali, mwenyeji ndio mwenye jukumu la kumlinda mgeni na walinzi wake huwa karibu tu kuangalia protocol na hupeana mkakati kwa pamoja. Akiwa ndani ya hotel au makazi waliofikia nje ya hotel mwenyeji huhusika ndani ya hotel ni jukumu la mgeni.

Kuna exceptions kwa wale wanachama 5 wa permanent seat kwenye UNSC tu ambao ulinzi wa viongozi wao muda woteni wa kwao wenyewe
 
Kiprotokali, mwenyeji ndio mwenye jukumu la kumlinda mgeni na walinzi wake huwa karibu tu kuangalia protocol na hupeana mkakati kwa pamoja. Akiwa ndani ya hotel au makazi waliofikia nje ya hotel mwenyeji huhusika ndani ya hotel ni jukumu la mgeni.

Kuna exceptions kwa wale wanachama 5 wa permanent seat kwenye UNSC tu ambao ulinzi wa viongozi wao muda woteni wa kwao wenyewe
Shukrani mkuu kwa majibu yako.
 
Kuna Uzi mmoja hapa ukiusoma utafamu mengi sana. Kama wewe sio mgeni humu atleast 5yrs back utakuwa unaufahamu
 
Mambo mengine hayatuhusu , by the way pale ni ikulu ndogo nafasi nk, ushauri tu serikali ijenge ikulu ndogo jengo lile si mahususi na maalumu kwa ikulu ndogo.Kwa heshima ya mkuu wetu kuokoa garama za safari za nje pajengwe Chato ikulu ndogo maalumu yenye hadhi.
Mimi nashauri wajenge ikulu kubwa kabisa Chato. My lifetime president
 
Wajuzi wa mambo naomba mnieleweshe hapa. Nimemsikia rais akiwaambia walinzi wake kuwa wasiwazuie watu wa rais wa Ethiopia kuingia ndani. Wakati tu wameingia Ikulu ndogo ya Chato, zikawa zinatokea zile pilikapilika za kupiga picha, rais Magufuli akasikika akiwaamrisha walinzi wake wasiwazuie watu wa rais wa Ethiopia, na ghafla tbc wakakata sauti, nadhani walikata sauti baada ya kuona labda anachokiongea rais hakitakiwi kusikiwa na public....
Kaombe kazi ya ulinzi wa rais utapata jibu sahihi, ila kama kuna mstaafu wa ulinzi wa rais atakupa jibu ila mang'anya kaeni pembeni.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom