Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,360
- 11,505
Inawezekana ningekuwa na chuki kiasi kikubwa sana kutokana na mambo mbalimbali ambayo aliyatenda au nena Mh. Rais alipokuwa Madarakani.
Kwa njia moja au nyingine yalitesa na kuumiza watu wangu wa karibu na mimi mwenyewe pia. Lakini inapofikia mtu akawa mgonjwa mahututi akiwa kitandani hana msaada mwingine wowote au anapofariki ukimtizama na kugundua kila kitu kilikuwa ubatili. Unaingiwa na moyo wa kibinadamu. Unamsamehe.
Unaweza kumbuka mtu alivyokukana wakati wa dhiki ukiwa unahitaji msaada wake. Au alipokukanyaga na akaendelea kusimama juu yako ukiwa umelala chini. Unayaacha hayo yapite.
Ntampongeza Mh. Magufuli kwa kuwa vile ambavyo alikuwa. Aliishi vile ambavyo alikuwa. Ingawa naamini katika Utawala wake ndipo ambapo tulishuhudia Viongozi wanafiki ambao hawajawahi kutokea. Ukimtoa yeye ambaye aliishi kama alivyokuwa. Alikuwa amezungukwa na viongozi wanafiki, wachumia tumbo, wasiokuwa na msimamo.
Ntaendelea kujifunza kuwa Duniani tunapita. Kila kitu kitabaki. Hatuhitajj majivuno. Itakayobaki ni Milima, Mawe halisi na viumbe visivyo hai.
Roho ya Marehemu IWEKWE INAPOSTAHILI. AMINA