Nimemkuta yu mjamzito!

Hili swali inabidi nalo LIPATIWE MAJIBU PIA!

Kwenye haya mambo hakuna majibu ya jumla. Kama kuna mwanamke ambaye mumewe amechiti na kuzaa nje na baada ya kugundua anaamua kuachana na huyo mumewe wala sitamlaumu. Ana haki zote za kufanya hivyo. Ila kama akigundua na kuamua kumsamehe huyo mumewe basi na yenyewe poa tu maana huo ni uamuzi wake.

Wewe huoni wadada wenzio wanavyoshadadia eti jamaa amsamehe…..na ukisoma ndani, nje, pamoja na katikati ya mstari utagundua kwamba hiyo kauli yangu ni kejeli (sarcasm).

Hivi na nyie mngekuwa mnaota liupele moja saizi ya pea kila mnavyotoka nje ya ndoa (mkiwa safarini) nyuso si zingekuwa zinatumika kusugua miguu?

Ndio msamahe, tatizo ni mimba au? Kama ni udanganyifu hata wewe utakuwa umeufanya. Kwa hiyo samehe 2 jifanye mlipeana mimba via bluetooth......

hahaha! Mimba via bluetooth?! Lol.

Jamani tuwe wakweli sawa alishindwa kuvumilia miaka 2 lakini mimba hapana haikubaliki,mi mjomba wangu ilimtokea hii baada ya kurudi maskini aliugua hajachukua hata mwezi akafariki yaani inauma saaana.

halaf na wewe urudi huku la sivyo utanikuta na kitambi.

Kuna moja nilisimuliwa: Jamaa mmoja aligundua kuwa mkewe alikuwa na mahusiano nje ya ndoa na akaamua amrudishe kwao kwa muda, baada ya baba yake na huyo jamaa kusikia hiyo habari ilibidi amuite mwanae kwake na akamuuliza vipi mbona umemrudisha mkeo kwao, jamaa akaja juu baba yule mwanamke siwezi kuishi naye amenisaliti, mzee akamwambia ok nisubiri then akaingia chumbani akatoka na picha ya watoto wake wote pamoja na huyo jamaa wakati akiwa mtoto, mzee akamwambia angalia picha hii kwa makini kisha niambie nyie wote hapo mnafanana, jamaa akaiangalia na kuona wengine wanafanana na wanafanana na baba yao lakini yeye tu ndo hafanani nao kabisa, mzee akamwambia nilipokuwa masomoni wewe ndo ulizaliwa kwa kifupi mimi ni baba yako mlezi lakini mama yako bado naishi naye.

Kama alivyosema George Herbet (mshairi Muingereza:1593-1633):
"Usaliti unakubalika kwani nafsi inahitaji kitu kimoja tu wakati mwili unahitaji vitu vingi".

Mara nyengine wanaume tuko watu wa ajabu. Mfano, mwanamume unaweza kumwachisha mke au mchumba wa mtu, pengine akiwa mja mzito au na watoto, na ukakubali kubeba mizigo hii, na pengine ukajiona mshindi, dume kama wewe hakuna. Lakini ukashindwa kusamehe iwapo mke au mchumba wako atatoka nje, tena sikwambii aje na mimba ya mwengine. Ni yale yale ya mtenda akitendewa.

Back to topic! Kama ikiwa na mimi ni kiwembe, ninaweza kumsamehe kwa usaliti, lakini nitashindwa kumsamehe kwa mimba, kwa sababu moja tu, "hana akili kiasi cha kubaki na mimba mpaka nirejee". Angelipaswa kuwa na tahadhari, na akili.

Kwa hivyo ikitegemea na mazingira, nitamshauri achague: Ama aende kwa baba wa mtoto wake, au akibaki nami mtoto ampeleke kwa baba yake. Na yeye, ikitegemea ni kwa kiwango gani ananipenda naanajuta, ataamua la pili. Lakini kama ataamua la kwanza, atakuwa amefanya vyema kwa yeye na kwa mimi.

yani masuke umenikumbusha jambo:
ni story ya kweli ilitokea kijijini kwetu moshi, kulikuwa na babu mmoja ambaye alikuwa na mtoto wake wa kiume. huyo mtoto alioa mke wake sasa siku moja akamshika mkwewe live na mtu mwingine wakivunja amri ya sita , kijana akaja juu na kwenda kwa wazazi kutaarifu kuwa anaandaa na kutoa talaka hamtaki tena tena huyo mke,
Baba wa kijana akamwambia sawa ila naomba hayo yafanyike hapa nyumbani siku ja jumapili.....kama ilivyo ada ikawadia na kijana akenda na mkwewe akatoe hiyo talaka.
babu akawa ameandaa madumu ya pombe na amechinja mbuzi akawaita na wazee wengine akasema kijana anataka kutoa talaka akaeleza sababu
akaingia ndani akatoa kibuyu cha pombe, kamba, akatandika na ngozii ya mbuzi AKASEMA NYOTE KWA YEYOTE YULE AMBAYE HAJAWAHI KUZINI NJE YA NDOA YAKE AJE ARUKE HAPA NASEMA AJE !
hakuna mtu aliyeruka vile vitu pale baada babu akavitoa akasema kijana hata wewe hujaruka HATA MAMA YAKO MZAZI HAJARUKA kwanin unatoa talaka???
kesi ikaisha kama hivyo kijana akmshika mkono mkewe na kuendelea na maisha ,
hivyo basi nataka kusema ktka mahusiano bwana mtu anajiona safi kwa sababu hajakamtwa ila kama ukimfumania mkeo/mumeo fanya maamuzi yenye busara sana ......wosia kwako nyani

mpaka saivi ratio inasema wanawake 3 kwa mwanume 1,,,,,mbona wengi hawajaolewa ???

hapana.......kama ningekuwa mwanaume......basi ningekuwa na uanaume wa uongo kwa hili......haifai

je akichakachuliwa kwa soksi asipate mimba atafaa kuvumiliwa.........................................sioni tofauti....msamehe mjipange upya kwa sababu kitanda hakizai haramu..................na hata huyu mumewe utakuta anayo mengi yanayohitaji mkewe amsamehe................hivyo wasamehane na wajipange upya.................

Ningemwambia aende kwa aliyempa mimba wakalee mimba mpaka atakapo mwachisha mtoto
ndio nimfate my honey wangu
jamani tuwape uhuru wanawake

Hivi kweli nyie wote mnaosema amsamehe ingekuwa nyinyi ndiyo mmetendwa mngesamehe au ni rahisi tu kwenu kusema wengine wasamehe lakini yakiwatokea nyie itawawia vigumu?

Manake sielewi kabisa...mtu akuchiti hadi apachikwe mimba halafu eti umsamehe....hivi baada ya kumsamehe mtaishi maisha ya kama yalivyokuwa kabla ya hiyo mimba?

I'm not getting this samehe samehe bullshit.

NN hata huyo mleta mada kama ni kweli basi kaanzia movie katika kati kati. Inawwezekana aliata tottaly mwasialano akaacha mke jina. Sasa na wanawake walivyo weak bana wakiwa kwenye stress za imahusiano akapata msanii wa kutumia hiyo loophole.

Anaweza kumsamehe kwa kujua ukweli role aliyoplay mpaka huyo anayemuta mkewe akapata mimba nje ya ndoa. KAma akiona usaliti wa mkewe hausiki nayo hata kidogo basi aanze mbele.

Mimi nahisi jamaa alikata mawasiliano kabisa la sivyo huyo mke si angetoa hiyo mimba. Akimuuliza kwa nini hakuitaa anasemaje?

Inaonekana jamaa hana mtoto na huyo "mke" Na je kwenye ndoa yao walikuwa wana mpango wa nyota ya kijani? Je ni mke wa ndoa ya dini. mila au ni zile ndoa zetu sugu za kimjini mjini ambazo wanafmilia na wazazi hawajazibariki. I mean jamaa kaleta habari za upande mmoja

Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla . But sidhani hata huyo "mke" anategemea msamaha. Simaanishi msamaha sio option lakini itakuwa ni suprise kwa wote na mwanzo mpya. Msamaha still bado ni option

Hivi kweli nyie wote mnaosema amsamehe ingekuwa nyinyi ndiyo mmetendwa mngesamehe au ni rahisi tu kwenu kusema wengine wasamehe lakini yakiwatokea nyie itawawia vigumu?

Manake sielewi kabisa...mtu akuchiti hadi apachikwe mimba halafu eti umsamehe....hivi baada ya kumsamehe mtaishi maisha ya kama yalivyokuwa kabla ya hiyo mimba?

I'm not getting this samehe samehe bullshit.

inawezekana siku hyo hyo aliyokucheat ndio katundikwa. Ukisema mtu anakucheat hadi anapata mimba ni kama vile inachukua muda mrefu mimba kutungwa.

inawezekana siku hyo hyo aliyokucheat ndio katundikwa. Ukisema mtu anakucheat hadi anapata mimba ni kama vile inachukua muda mrefu mimba kutungwa.

Haijalishi...kuchiti mara moja au mara nyingi bado ni kuchiti tu. Kibaya zaidi ni mtu anachiti bila kutumia kinga. Hapo anajihatarishia maisha yake mwenyewe na pia ya huyo anayemchiti.

Hebu fikiri mumeo anakuletea likaswende au li chlamydia. Wewe mtoto wa watu hujui hili wala lile siku unaenda kuoga unaona usaa unatoka kwenye kitumbua chako....lol....hivi utajisikiaje?

Hamna cha kusamehe hapo.ni kumfungashia virago asepe zake,no way out.

Haijalishi...kuchiti mara moja au mara nyingi bado ni kuchiti tu. Kibaya zaidi ni mtu anachiti bila kutumia kinga. Hapo anajihatarishia maisha yake mwenyewe na pia ya huyo anayemchiti.

Hebu fikiri mumeo anakuletea likaswende au li chlamydia. Wewe mtoto wa watu hujui hili wala lile siku unaenda kuoga unaona usaa unatoka kwenye kitumbua chako....lol....hivi utajisikiaje?

Unamyonga.

Kwa miaka miwili kweli ni balaaa, hata mie nsingeweza vumilia, sema kakosea kubeba mimba tuu, japo sisi wanaume hata mwezi 1 tu mtu amcheat mkewe Laivu..

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom