Nimemfumania mume wangu live

Nimemfumania mume wangu live

Jamani nimemfumania mumewangu live tena na rafiki yangu amekua akimtongoza huu mwaka wa pili tukaamua kuweka mchongo leo tukamkamata yani asivyo na haya anajitetea huyu rafik yangu ndie kamtongoza huyu mwanaume najiuliza nifanye nini hata msamaha hawezi kuomba
Fumanizi unatakiwa uwe na kifua dada sasa umekuja huku kutafuta ushauri wakati umeyataka mwenyewe
 
Umemtumia rafiki yako kumfumaniaje tena wakati ulipanga na rafiki yako!?

Unashangaza kama mwanamke, sasa huyo rafiki yako ukikuta kesho amempa penzi analolitaka miaka yote utafanyaje?

Wewe kama mke ulishindwaje kuyamaliza na mume bila kumtumia rafiki yako.

Unajua wqnaume wanajua kujibu kwa visasi, unamlazimisha akubali nini tena wqkati umemfumania kama unavyodai? Umejichemshia maji ya moto.

Natabiri kumeo kufanya ambayo hata hukutegemea, kwanza umemshushia hadhi kwa kumuabisha live, na walivyo na vinyongo eeeeeh

Umeokoa kwa rafiki, subiri kupata wenzakonhata kumi na watoto wake huko nje.


Haya mambo yanataka utumie akili, kwangu mimi umechemka vibaya mno. Ungetumia njia zingine kuyazima hayo anayofanya. Unalo kama unamjua vizuri basi jaribu kujenga na sio kwenda unapiga tarumbeta kila mahala kumsema.

Usisahau kumchunga huyo rafiki yako aliyekubali kutenda mliyotenda, hakutakii mema. Angekuwa anakutakia mema angetumia njia ingine kumuonyesha kuwa amekuambia na hujui leo kaambiwaje kwa hizo dakika chache na labda kapenda ha ha haaaaa

Kila la kheri.
Ujumbe mubashara kabisa ila tatizo wewe ni rafiki yake Bashite!!
 
Mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake mwenyewe unaamin marafiki pole sn
 
Hakuna mwanaume asiyecheat hata km wapo ni 0.11%, bt mwanaume anayejitambua hata km anacheat hawezi kukuoneshea dharau hata mara moja, so achana kufatilia mumeo hata ukiachana nae huko unakoenda ubaweza ukakuta unaletewa hadi kitandani kwako.
 
Ninakumbuka majeraha mama aliyopitia kwa uchungu wa mume
Unamaanisha baba yako?
Basi nimeshakuelewa mama.
Maombi ni muhimu, wewe hutapitia hio njia.maombi yatavunja vunja hayo mabaya yote .
 
Mwache mwanaume uone kazi ya kumpata mwanaume ilivyo ngumu!.......Kuna rafiki yangu wa kike alipendwa na mwanaume fulani yule mwanaume akapeleka hadi mahari kwao cha kushangaza huyo rafiki yangu akamkataa na kumfukuza kisa eti ananipenda mimi,mimi nimemwambia kuwa ataisoma namba na nimemuhakikishia kuwa hatapata tena mwanaume mwingine wa kumuoa!!
kumbe we ni jike.?
 
Hahahaha msamehe tuu maana wewe uliweka mtego wakati hujajua utatoa adhabu gani ukimkamata....................
 
kumbe we ni jike.?
Mkuu hujaelewa, soma vizuri au umeamka na hangover ya safari za jana??🙂🙂........Kwenye hiyo comment yangu kuna sehemu nimesema kuwa: alimkataa jamaa na kumfukuza kisa ananipenda mimi!!(hii ndo sentensi katika comment yangu inayodhihirisha kuwa mimi ni me).........Sasa mimi ningekuwa ni jike mwenzake angenipendaje??
 
kihere here chako...mwanaume hachunguzwi
 
Mkuu hujaelewa, soma vizuri au umeamka na hangover ya safari za jana??........Kwenye hiyo comment yangu kuna sehemu nimesema kuwa: alimkataa jamaa na kumfukuza kisa ananipenda mimi!!(hii ndo sentensi katika comment yangu inayodhihirisha kuwa mimi ni me).........Sasa mimi ningekuwa jike mwenzake angenipendaje??
khee sikuona hapo hatari sana kwa hiyo umeoa?.
 
khee sikuona hapo hatari sana kwa hiyo umeoa?.
Sijaoa wala sina mchumba ila yeye ni rafiki yangu tu wa kawaida na siyo mpenzi na ninampenda tu kama rafiki yangu wa kawaida na ninaamini kuwa tukiwa marafiki wa kawaida kutakuwa na utamu zaidi katika maisha yetu kuliko tukiwa wapenzi
 
By the way, mume wa huyo shosti wako mtamfumanishi lini? Au shosti yeye ameolewa na Malaika?
 
Sijaoa wala sina mchumba ila yeye ni rafiki yangu tu wa kawaida na siyo mpenzi/rafiki wa mapenzi na ninampenda tu kama rafiki yangu wa kawaida na ninaamini kuwa tukiwa marafiki wa kawaida kutakuwa na utamu zaidi kuliko tukiwa wapenzi
umemruhusu awe na mpenzi mwingine?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom