Nimekuwa mpweke sana, sina rafiki wa karibu. Je, kuna madhara kuishi hivi?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,703
36,150
Habari?

Mimi ni baba wa watoto 2 na mke mmoja.

Jumla home kwangu sasa tuko watu 7, wakubwa hasa ni Mimi na wife tu wengine ni watoto wadogo wa primary na kindergarten na wengine ni wadogo zaidi.

Ratiba yangu ni kazini- nyumbani, nyumbani- kazini. Ila muda mwingi niko nyumbani. Napiga stori na watu tukikutana kazini basi nikiondoka kazini mchezo umeisha.

Sina rafiki wa ku share naye mambo ya maisha au hata kufanya naye tour za hapa na pale.

Nilipokuwa na usafiri kidogo nilikuwa napata muda kuzunguka na watoto sehemu za karibu na nyumbani, nikiwanunulia chips na vikorokoro vingine tunarudi home. Sasa hivi sina usafiri. Mimi muda wote naishia ndani.
Siku nyingine naishia kutoka nje ya geti na kuchungulia nje mara Moja basi.

Au nitatoka kulishia kuku na kuangalia mayai bandani naingia ndani siku itapita.
Muda mwingine natoka nje na kuzunguka nyumba ili kuhakikisha usalama wa nyumba na familia, asije mtu akatupia maiti nyumbani kwangu kisha kunitia mtegoni.

According to my work kwa wiki kazini nakwenda mara 3 au 4 tu na nikienda naingia masaa 12. Hivyo muda mwingi niko nyumbani.

Sina rafiki kazini wala mtaani.

Ninapofanya kazi kwenda Kariakoo hata kwa mguu ukiamua unaweza kwenda lakini ni mwaka sasa sijakanyaga Kariakoo.

Wanangu na wanafamilia yangu ndo hugeuka kuwa marafiki zangu.

Naweza kuchangia hharusi ila siwezi kwenda ukumbini. Nilikwenda hharusi moja tu kwakuwa nilikuwa best man wa bwana hharusi.

Hata mke wangu tulifunga ndoa kwa DC Ilala mashahidi tuliwapata hukohuko.

Kwa ufupi Mimi sipendi sherehe, naona kama zinanitilia makelele tu.

Wengine wanataka kuwa karibu na Mimi lakini Mimi nakuwa mzito kuwa karibu nao.

Nawaza hapa sasa nina 36, hii hali ya kukaa nyumba haitaniathiri?

Maana napenda kulalia mgongo muda wote, hii tabia ya kupenda kulalia mgongo nimeianza nikiwa school miaka zaidi ya 10 imepita.

Hata kazini kiti lazima nikilalie ndo nasikia mdadi.

Au nikipata pesa tabadilika?

Maana kujifungia sometimes nahisi ni ukata labda.
 
Sina la kukushauri sana kivile maana

Umenizidi umri

Umenizidi familia

Umenizidi uzoefu wa maisha

Ila naona Inawezekana ukawa uko sahihi kiasi fulani unakwepa mengi huko njee tafuta labda activity nyingine mfano draft, mazoezi n.k ili uwe unatoka toka usikae sana ndani, ndani achia makochi na masufuria
 
Michezo yangu hii, sema sasa pale kazini kwetu mashangazi na wajomba na kina mama ndio wamejaa. Sasa nikishalalia kiti nakuta nishafinywa nikae vizuri naumiza mgongo.

Kulalia sana mgongo sijui, ila kukaa unproper kwa kiti kiukweli nasikia madhara yako.
Vya kulalia ni vingi, usilalie mgongo
 
Sina la kukushauri sana kivile maana
Umenizidi umri
Umenizidi familia
Umenizidi uzoefu wa maisha
Ila naona Inawezekana ukawa uko sahihi kiasi fulani unakwepa mengi huko njee tafuta labda activity nyingine mfano draft,mazoezi n.k ili uwe unatoka toka usikae sana ndani,ndani achia makochi na masufuria
Basi wewe ni mdogo sana.
Mimi 36 nimekupita age?
 
marafiki wengi huwa tunawapata tukiwa chini ya miaka 25 huku huwa tuna muda mwingi majukumu machache inakuwa rahisi kujuana na kuzoeana na hata tukikosana huwa ni rahisi kupatana.

Shukuru una mke na watoto hao ni zaidi ya marafiki ni familia,

Kwa miaka yako kutafuta marafiki ni changamoto, labda tafuta tu shughuli zingine kama kwenda kanisani / msikitini,

Ukubwani huwa kuna upweke wa hali ya juu sana kama huku chini ulishindwa kupata marafiki,

Kuhusu ndugu zako vipi ?
 
marafiki wengi huwa tunawapata tukiwa chini ya miaka 25 huku huwa tuna muda mwingi majukumu machache inakuwa rahisi haya kujuana mambo mengi ya kuendeleza urafiki wenu.

Kwa miaka yako tafuta tu shughuli zingine za kukukutanisha na watu kwa shughuli husika kama kwenda kanisani / msikitini,

Ukubwani huwa kuna upweke wa hali ya juu sana kama huku chini ulishindwa kupata marafiki,

Kuhusu ndugu zako vipi ?
Aiseee.
Inauma sana.
Kwa upweke huu sijui tatoboa miaka 70!!
 
Kama unaridhika na hiyo hali basi sawa.

Kama huridhiki nayo basi tafuta suluhisho.
Mf mimi siridhiki.

Aina ya washkaji wa job hawaendagi bar kabisa. So hao tu ni tuende AiM mall tukacheze game, ama tukale mahali.

Sasa siku nikimiss bar! Nateseka kutafuta anaza kampani 🤣
 
Back
Top Bottom