Nimekutana na malaika

Nimekutana na malaika

Status
Not open for further replies.
Dah umejitetea kweli.. okay tumewaelewa
Bado tupo wengi sanaaaa, kuomba pesa haimaanishi hatuwapendi jamani. Ni shida tu ndio hazina adabu, mtuvumilie tu na mzidi kutupatia pesa. Tunawapenda sana na mbarikiwe kila mtoapo. Amen.
 
Mwanaume kuelezea hisia zake kiasi hiki ni awe ameguswa haswa kwa ulivyojitanabaisha kua ni mgongaji msepaji. Natumaini haujakosea, na nakutakia kila la heri.

One more thing ulimpata mitaa gani na mimi nikashinde huko? Uanaume ni kusaidiana
 
Haha siwezi kumkaribisha labda aje na Id nyingine. Kama hana Id nyingine ya zamani basi hana bahati maana Id za kuanzia 2015 pm kwangu hazikaribishwi
Kwa ninavyomjua hearly kwa hii post mpe siku mbili akatafute ugomvi na shemeji kisha aanze kushinda pm kwako
 
"Hakuna Mungu"
"Nimekutana na Malaika"
Duniani kuna watu wa ajabu sana.
Anyway ongera Mkuu.
 
Huu uzi bila namba ya simu ya huyo binti ni batili. Mods sukuma ndani huyu mtu.
 
Salamu zifike kwenu " Waungwana


Wakati sehemu " kubwa ya Jamii yetu ikiendelea kuzua taharuki na lawama dhidi ya Mmong'onyoko wa kimaadili uliopo sasa na kuendelea kuvuma kwa kasi ya moto wa petrol " Moto ambao umepelekea kuyafanya mahusiaono yetu ya Mapenzi kufikwa na changamoto ya kutoweka kwa Utu.Upendo wa dhati " na upotevu wa soni (haya) Na kusababisha kila mtu awe analia kilio cha aina yake baada ya kutendwa na mpenzi wake/aliyekuwa mpenzi wake "

Huku ikibainika kwamba kichochezi kikubwa ni tamaa " ni wazi kwamba "sote humu tumekuwa washuhuda wa matukio mbali mbali " ambayo yametupatia experience za kutosha "iwe nikutoka kwa Watu wanao tuzunguka au sisi wenyewe na kutufanya tuingiwe na hofu ya kutowaamini wenza wetu tunapokuwa nao katika mahusiano "

a) wanaume tuna walaumu wanawake kuwa sio wa kweli " wana tamaa ya mali na niwapenda pesa walio kubuhu "wame poteza utu " na vimelea vyote vya upendo


(b) hali pia iko hivyo hivyo kwa wanawake pia " imani yao dhidi yetu wanaume imekufa " wanalalamika kwamba wanaume haturidhiki. Hatufadhiliki " tumekuwa ni watu tusiojali na tunao endekeza mno umalaya " kufanya usaliti imekuwa ni sehemu ya maisha yetu "

(c) naomba nitamke tu wazi kuwa na mimi (me) nilikuwa miongoni ya watu ambao wana imani finyu (haba) dhidi ya hawa wanawake wa sasa " tokana na wengi kuwa na mienendo ambayo haisadifu upendo " .wala utu ".

****** ******** ******* *******
Je nimekutana na malaika !!?


hili ndio swali ambalo limekuwa linaitafuna akili yangu na kunifanya nijiulize kila saa " na nisipate jibu "

(A) imepita miezi mi-tatu sasa " tangu nikutane 'na mwanamke ambaye ana Tabia za tofauti sana ambazo hazipaswi kuchanganywa pamoja na hawa wanawake wengi wa sasa " ... kwanza binti anajitosheleza " kielimu " kiuchumi " mpaka kihekima " tabia zake zimejaa kweli"toka rohoni " muda wote amekuwa anaonyesha kwamba ananijali sana mimi kuliko hata wallet yangu " hajawahi kuthubutu hata kuuruhusu ulimi wake unitamke neno " naomba hela " (nikasuke. Ninue voucher . Ninunue umeme gesi imeisha " nataka nikafanye shopping ya kitu fulani' nataka nijaze mafuta .nataka nilipe kodi) wanaume wenzangu nadhani wenyewe Tabia hizi mmeshakutana nazo " zile text za baby ni kwambie kitu kwa huyu binti hazipo kabisa " na kwakupitia yeye nimesha anza kuzisahau "

(B) nilikuwa nimeshaamua kujiweka mbali kabisa na kujihusisha na haya mahusiano bandia yaliyopo mioyoni mwetu kwa sisi binaadamu wa wakati huu " ..nitamke tu wazi nilikuwa mzee wa hit and run " ... lakini tangu binti huyu aje katika maisha yangu na jihisi kuzaliwa upya .. binti amenifanya nijihisi kuitawala ardhi na mbingu ' kila kukicha ananifanya nifikirie zaidi kubaki na yeye " Anauwezo mkubwa sana wakufikiri " ana ushawishi wa kimaongezi " uliopambwa na mpangilio wa maneno mazuri " yenye mchanganyiko wa sauti yenye Utamu mithili ya ladha ya chocolate " .Zaidi ya yote huwa nafurahishwa na Jinsi ambavyo huwa ananieleza mikakati mbali mbali ya sisi kuweza kufanikisha malengo yetu (kiuchumi "kiafya" na kimapenzi ) Ambayo tumejiwekea " Hakika anani staajabisha '"

(C)nilishazoea kuombwa ombwa hela nilishazoea ( lakini kwa huyu binti story nitofauti kabisa nimpaka nijiongeze mwenyewe) " kutamkiwa maneno ya kukatisha tamaa " nilishazoea kutoungwa mkono katika mipango yangu niliyo kuwa naifanya " ... unaishi na mwanamke lakini the way anavyotaka kukuchokonoa utadhani ni mshirika mkuu mwenzio wa biashara/kampuni " hawana sweet tongue kabisa " anaweza kushinda kutwa nzima hata kuku tumia text ya kukujulia hali anashindwa" maneno ya pole "samahani .Asante kwake " ni Anasa kuyatamka " ...


Nimalizie tu kwa kutoa Rai kwa wanaume wenzangu " Jamani wanawake wastaarabu wapo " msikate Tamaa endeleeni kutafuta mtawapata " lakini katika kuwatafuta huko mnapaswa kuwa na subira " pia muwe mnaangalia na wanawake wakuongea nao " Maana hawa wanawake ambao ni wastaarabu wamebaki wachache mnoo tena katika hili nilikuwa naiomba serikali ya JMT iingilie kati na kujenga sera itakayo weza kuwalinda hawa viumbe wesiweze kutoweka kabisa " uwepo wao utakuwa ni chachu ya kimaadili kwa jamii husika na kuwafanya watu wengine waige ustaarabu wao " utakao pelekea kuitengeneza Tanzania mpya yenye watu waliostaarabika zaidi katika mahusiano "...

Though mpenzi huwa hatafutwi kama pesa bali huwa anajileta au analetwa na wakati stahiki/sahihi " huku kutafuta tafuta hovyo ndio sababu kubwa inayopelekea " tukutane na watu ambao hawafanani na taratibu zetu tunazo zipenda na kutuvutia "

nakupenda sana x " Malaika wangu Mungu akujaalie Baraka uzima na upendo kwa watu wote maradufu " ... wabarikiwe wazazi wako pia kwa kukulea vyema mpaka kufanikiwa kuku-shape" hatimae Leo umekuwa hivyo mwenye Tabia njema ambayo ni faida kwa watu wengine ...

Najua unaogopa Jongoo hahaa leo namleta Aisee ndani lazima pachimbike "(kidding)
@Mzigua90 pita hapa ujue wapi umefeli kuniweka kwenye angle yako...!
 
Umeona mwenzio amesema haombwi hela anajiongeza!? hapo ndipo ulipofeli boo. Anza kunipa uone kama nitaendelea kukuomba. Halafu si unaona huyo wifi kajitosheleza kiuchumi?? Mi bado hivyo vinginw unisaidie tu. Kodi najua huwezi kunilipia basi hata salon baba.
@Mzigua90 pita hapa ujue wapi umefeli kuniweka kwenye angle yako...!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom