Nimekuja kumegewa siri hii baada ya miaka mingi!

Nimekuja kumegewa siri hii baada ya miaka mingi!

Salaam, nimekuja kujua kitu kilichonitonesha kidonda changu, na kinaendelea kunitonesha. Ni kuwa nikiwa na miaka 7 au 8 hivi, mama yangu mzazi alitaka kuniua, kwa mujibu wa aliyenisimulia ni kuwa siku moja alinikaba mno shingoni ili aninyonge, baadaye roho ya huruma ikamuingia mara baada ya kuona naanza kutoa macho na kukosa nguvu, akaniacha. Anasema kuwa mama alishadhamiria kunimaliza, alishapanga.

Nakumbuka nilikuwa mtundu, ndiyo sababu kuu iliyopelekea kutaka kuuawa, haya nimeyajua nikiwa MTU mzima hivi hivi! Nimehuzunika sana!

Ila mama hajui kama nimeshajua, nafikiri alitaka iwe siri.!
Umeambiwa na nani?

Wife ?

Kazi ijayo jibaba.
Unajitoa ufahamu ukapotezw
 
Miaka 8 ni mkubwa ungekuwa unakumbuka hili tukio.

Miaka 8 uko darasa la 1 ana 2, kusahau matukio ya namna hii isingekuwa rahisi.
 
Huwa unawafikiliaga sana kabla ya kuandika jambo comment nyingi naona, na hongera sana, mimi nimejiuliza swali hilo hilo je ameambiwa ndiyo kastuka kuwa mama yake alitaka kumuua hiv katika hali ya utoto unashindwaje kukumbuka vitendo vya ukatili, mimi. Nimewaza pia aliemwambia anataka wakosena na mama yake
Unajua kuna vitu mtu anakuambia ili iweje ufanyejee na unavyotujua wabongo kwa maneno
 
Kuwa makini na huyo mtu aliyekusimulia, hao huwa ni wanafiki kwenye familia za watu. Jiulize anataka nini mpaka akusimulie habari hiyo sahivi wakati huu unaishi vizuri na mama yako.
Be careful
 
Mungu wa ajabu sana,unaweza kuja kuzaa mtoto mwenye tabia kama hizo,what goes around comes around,kwahiyo usimlaumu sana mama yako...
 
Mama ni Mama! Sahau kabisa,maana pamoja na hayo amekulea akakufikisha mpaka hapo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom