Nimekuja kumegewa siri hii baada ya miaka mingi!

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
3,977
Reaction score
5,352
Salaam, nimekuja kujua kitu kilichonitonesha kidonda changu, na kinaendelea kunitonesha. Ni kuwa nikiwa na miaka 7 au 8 hivi, mama yangu mzazi alitaka kuniua, kwa mujibu wa aliyenisimulia ni kuwa siku moja alinikaba mno shingoni ili aninyonge, baadaye roho ya huruma ikamuingia mara baada ya kuona naanza kutoa macho na kukosa nguvu, akaniacha. Anasema kuwa mama alishadhamiria kunimaliza, alishapanga.

Nakumbuka nilikuwa mtundu, ndiyo sababu kuu iliyopelekea kutaka kuuawa, haya nimeyajua nikiwa MTU mzima hivi hivi! Nimehuzunika sana!

Ila mama hajui kama nimeshajua, nafikiri alitaka iwe siri.!
 
Angetaka kukuua usingekuwepo hapa. Hata usiku angeweza kukunyonga.

Labda hasira zilipanda akafanya hivyo na baada ya kuona kweli umeanza kupoteza fahamu basi akakuwachia.

Au alikuwa na depression na akafanya kitu kwa hasira.

Ungemuuliza ili uweze kusafisha roho yako na akuombe msamaha. Lakini pia umsamehe usichukulie kisasi au kinyongo.
 
Salaam, nimekuja kujua kitu kilichonitonesha kidonda changu, na kinaendelea kunitonesha. Ni kuwa nikiwa na miaka 7 au 8 hivi, mama yangu mzazi alitaka kuniua, kwa mujibu wa aliyenisimulia ni kuwa siku moja alinikaba mno shingoni ili aninyonge, baadaye roho ya huruma ikamuingia mara baada ya kuona naanza kutoa macho na kukosa nguvu, akaniacha. Anasema kuwa mama alishadhamiria kunimaliza, alishapanga.

Nakumbuka nilikuwa mtundu, ndiyo sababu kuu iliyopelekea kutaka kuuawa, haya nimeyajua nikiwa MTU mzima hivi hivi! Nimehuzunika sana!

Ila mama hajui kama nimeshajua, nafikiri alitaka iwe siri.!
Usihuzunike bro mpende sana huyo mama maana ukiacha hiyo story amefanya mengi mpaka uko hapo na unasimuliwa hiyo story kumbuka juhudi zake kwako

Nilichomwa moto wakati niko mtoto mikononi nilifungwa kitambaa na nikamwagiwa mafuta ya taa na Baba yangu wa kambo mama alinificha ila uzuri ninakumbukumbu sana ila sikuwa na uhakika na kumbukumbu zangu kuna siku ilibidi nimkazie bi mkubwa akaniambia kila kitu kuwa mumewe ndio alinichoma moto nikiwa mdgo, nashukuru nilisamehe siku ileile maana bado wanaishi pamoja na nina 27yrs now
 
Watoto watundu , wanaokwenda kinyume na mafundisho ya wazazi wao wakiwa wadogo au katika hatua fulani za makuzi yao ndio huwa wakombozi wa familia na huwatunza wazee.

Mzazi binti yako akipata ujauzito akiwa anasoma usikubali umuue mjukuu wako kwa kutoa mimba itakugharimu milele roho yake, na binti uliyefikiri atarudi kwenye ubinti tena na kufanikiwa kimaisha haitakuwa hivyo. Huyo mjukuu ndio ilikuwa baraka kwako ni mtoto wa ujombani

Mzazi mwanao akibadili dini usitamke malaana ya ajabu kwa mwanao kisa eti wewe unajiita mkristo safi na kuona imani nyingine kama kituko, au wewe ni muislam safi na kiongozi wa dini unaona imani zingine makagiri kama mijusi, ndugu yangu ya Mungu mengi, Yeye angeamua tuwe na imani moja angetuumba kabila moja, lugha moja, rangi moja lakini utofauti wetu ndio ukuu wake

Mzazi, mtoto akizaliwa na kuwa mkorofi sana na hata kutumia vilevi , pambana mpaja mwisho huo ndio msalaba wako, kwenye maisha ni mzunguko wa huzuni na furaha, usimlaani kuna siku atabadilika hutoamini
 
Umeongea, wazazi walilazimisha sister atoe ujauzito ili aendelee na shule, leo yuko ndoani miaka inakatika na hakuna mtoto, so sad😢
 
Salaam, nimekuja kujua kitu kilichonitonesha kidonda changu, na kinaendelea kunitonesha. Ni kuwa nikiwa na miaka 7 au 8 hivi, mama yangu mzazi alitaka kuniua, kwa mujibu wa aliyenisimulia ni kuwa siku moja alinikaba mno shingoni ili aninyonge, baadaye roho ya huruma ikamuingia mara baada ya kuona naanza kutoa macho na kukosa nguvu, akaniacha. Anasema kuwa mama alishadhamiria kunimaliza, alishapanga.

Nakumbuka nilikuwa mtundu, ndiyo sababu kuu iliyopelekea kutaka kuuawa, haya nimeyajua nikiwa MTU mzima hivi hivi! Nimehuzunika sana!

Ila mama hajui kama nimeshajua, nafikiri alitaka iwe siri.!
Pole sana mkuu....pole sana sana sana!
 
Mchongo
 
Huyo alokwambia ni limbeya likubwa sana,mchonganishi na mgombanishi,mkuu piga chini uchawi wa wazi hivyo.
 
Kwel kabisa mkuu kama mama angetaka kumuua angemmaliza muda wowote tena bila ushaidi
 
Usihuzunike bro mpende sana huyo mama maana ukiacha hiyo story amefanya mengi mpaka uko hapo na unasimuliwa hiyo story kumbuka juhudi zake kwako

Nilichomwa moto wakati niko mtoto mikononi nilifungwa kitambaa na nikamwagiwa mafuta ya taa na Baba yangu wa kambo mama alinificha ila uzuri ninakumbukumbu sana ila sikuwa na uhakika na kumbukumbu zangu kuna siku ilibidi nimkazie bi mkubwa akaniambia kila kitu kuwa mumewe ndio alinichoma moto nikiwa mdgo, nashukuru nilisamehe siku ileile maana bado wanaishi pamoja na nina 27yrs now
Pole sana mkuu. Hayo mateso si mchezo.
Pia nakupongeza kwa kuumbwa kiajabu kabisa na hiyo roho ya kusamehe.
Hiko ni kipaji.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom