Nimekosea Wapi?

Nimekosea Wapi?

Mkuu kila familia na maadili yake ila mimi nnachokiofia ni baadae watoto wangu na wake kuja kuoana manake itakua mparaganyo, yani mama ndugu baba ndugu sipendi hiyo itoke sijui kama kuna mtu ananielewa kwenye hili,mimi mwenyewe nimekataa kuolewa na mtoto wa mjomba na mjomba alininunia 3-4 good yrs na hata sasa ana cheka tuu ila anasema hakufurahi mimi kuolewa na mtu wa nje...
kumbe shida sio kuolewa na shemeji, shida ni watoto wenu wanaweza aona kwa kwa kuwa nyie huwa mnaona mjomba kwa shangazi.

hilo haliwezi tokea tena maana hao watoto watakao zaliwa hawatakuwa ukoo wenu (wenye kuoana watoto wa ma shangazi kwa mjomba) watakuwa ukoo wa wanaume na wao hawana utaratibu huo (maana wewe ulimkataa mtoto wa mjomba hivyo uko ukoo mwingine)

kifupi mwache aolewe maana watoto sio wa ukoo wenu wa kuoana watu wa karibu na hata ingekuwa hivyo tangu utotoni mngeweza weka misingi ya wao kuonana ni ndugu kabisa na kusiwepo mambo ya kuoana
 
Mkuu mume wangu Kwao wanatabia kama za kwtu ila sio kivile ila wanapenda sana kuowana familia,hilo mimi silikubali hata iweje najaribu sana kulipinga,mkuu laitani ungekua unaona family wanapokua wanagombana kisa kila mtu anamtetea mwanawe unakua ugomvi sio wa mke na mume nawa ndugu,sipendi kuona hivyo,na pili unakuta huyu ana pumu mara yule ana sijui nini hua sipendi,wanasema najitia mzungu ila ni sawa waseme tuu wanapokwenda hospital dr akisema wanaanza kutukana mpaka ma dr sasa ntajitahidi kwa huyu na inshallah ntaweza..
 
Baba Ni Mu Oman tabia zake niza Kiarabu kupitiliza,mkuu hakuna kitu hawa watu utawaeleza wakuelewe zaidi yakutumia force,kitu najivunia au kinachonisaidia jina langu nimepewa jina na Bibi mzaa baba na Dad humwambiii kitu kwa mamake
sasa mimi nikisema kitu hua ananisikiliza sana na najua ananipenda,na anajua kua nikiongea kitu hua mara nyingi sana nampa sababu,na kama kwenye hili yeye pia amesema sawa wewe ndio unamlea na ndio unajua nini kizuri kwake, kuna siku tuliwapeleka watoto hospital wa bro wana pumu balaa hakuna mwenye afadhali dr akasema sio vizuri kuoana familia moja,duu dr alichambwaaa mpaka nikaona aibu..

Arabs,na kweli hizo ni tamaduni za Kiarabu.Naniwabishi kweli hao watu.
Basi wewe tumia ushawishi wako kwa mdogo wako mkataze asiolewe na Huyo bwana.

Swali kidogo,Ni kwanini Arabs mnapenda kuona within family kuna ukweli kwamba mnakuwa na lengo LA kutaka kuzuia utajiri na Mali visiende nnje ya familia au kuna Lingine ? Alafu ni vigumu sana mwanamke wa kiarabu kuolewa na Muafrika mwenye ngozi Nyeusi naskia labda akiwa na pesa sana anaweza kufikiriwa...

Hilo kwa upande wako unalionaje..?
 
Wallah sio madogo,kuna watakao niona sina maana,na wengine wameshaanza kujiweka karibu na yeye kwakuharibu
ila Inshallah kheir..
...ila kiukweli kabisa,hili jambo ni dogo wewe tu ndo unalikuza!labda uwe na ya rohoni kwa shemeji yako,ila si kwa sababu hizi!
....mumeo na mdogo wake hawajawaoa ndugu zao,hii inaleta picha angalau kwao wao wawili huo sio 'utamaduni' wao;kwanini wewe uwe na hofu ya watoto kuoana?
..hiyo sababu ya kutotaka kuolewa kwenye familia moja ndo kabisaaaaa si ya kujadili!
.haya sasa mama,
....tuambie ya rohoni!
 
duh !yaan huon kuna shida hapo ! hv unajua kuna possiilities za kuzaa watoto wenye magonjwa ya kurithi na utaahira juu !aisee! kweli kua uyaone
 
  • Thanks
Reactions: BAK
hayo mambo ya kuoana ndugu nasikiaga kwa wahindi kumbe mpaka bongo yapo, sasa mwachie mdogo wako aolewe maana hamna tatizo hapo labda wewe tu una jingine
 
duh !yaan huon kuna shida hapo ! hv unajua kuna possiilities za kuzaa watoto wenye magonjwa ya kurithi na utaahira juu !aisee! kweli kua uyaone

Unajua kwenye hizi familia za kiarabu kunakuwaga na wototo wengi wenye natatizo ya akili ,wanaitwa mandondocha na watu wengi wanaishia kufikiri kwamba wamewatumia kishirikina ili kupata mali,Hakuna lolote shida yao kubwa inaanziaga hapo. Kuona ndugu kwa ndugu.!
 
duh !yaan huon kuna shida hapo ! hv unajua kuna possiilities za kuzaa watoto wenye magonjwa ya kurithi na utaahira juu !aisee! kweli kua uyaone
...hahahaha
..acha maskhara,
.zimekaaje hizo possibilities?(natumai waelewa unachokizungumzia)
 
Familia za asili ya kiarabu jambo hilo ni la kawaida sana yaani huwa hawapendi kabisa ndugu aolewe nje ya ukoo wao

binafsi yameshanikuta hayo na nasikitika sana kwa hilo jambo kwani ilifikia kipindi binti alikunywa sumu ila aliwahishwa hospitali akapona na mpaka leo hawataki tuoane kwa kutegemea kuwa binti atabadili msimamo na leo hii tena wamemueleza ajiandae aende omani kukaa miaka4 ila najua yote ni kuweka mazingira magumu kwa yule binti ni kisa kirefu hapa nimeweka kwa kifupi na pia sio mahala pake
 
Hiyo tabia ya kabira gani kuoana ndugu?kwa sisi Wakristo hiyo ni laana na sio sawa hata kidogo maana magojwa ya asili yataendelea kuzunguka kwenye familia hiyo
 
Mnaoana "mtoto wa baba mkubwa na baba mdogo?" Hizi ni tamaduni za nchi gani? NIMPENDENANI inakuwaje mnaruhusu familia kuwa na mwingiliano wa karibu kiasi hicho?

Kuhusu mdogo wako kuolewa na shemeji yako, kiuhalisia its not a big deal kwa sababu hapo hakuna muingiliano wa damu hata kidogo, labda woga wako kwa vizazi vyenu vinavyokuja.

I'd advise you to let her decide, baki kuwa mshauri wake na mwambie positive na negative zote in case akiamua kuolewa na shemeji yako.
 
waliheshimu sababu niliwambia reason na baada ya muda wameiona,mkuu sitokubali makosa walofanya wale na huyu ayafanye mimi ni mlezi wake na sio adui yake siwezi kumtia kwenye matatizo mdogo wangu ila nataka aone kwanini nimechukua maamuzi haya..

Makosa yapi unazungumzia? shemeji na mdogo wako hawana undugu wa damu, right?

Na kwa mujibu wa mada yako, reason pekee uliyotoa ni hofu ya uwezekano wa watoto wenu (ambao bado hata hawajazaliwa) kuja kuoana badae, kufuata family tradition ambayo tayari ulishaivunja. Najaribu kukuelewa bila mafanikio.
 
Mkuu Ahsante sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa zaidi ya sanaaaaaaaaaaa,kwakusimama na mimi japo hunijua ila mwenyezi mungu ndio atakae kulipa kwani sio rahisi mtu kunielewa nna maana gani,na ndio mana kuna time hua nalia sababu angekuwepo mama afadhali angenisaidia, naandika huku machozi yananitoka nahisi napiga peke yangu na hakuna wakunielewa japo kwa mawazo, najiuliza kwanini hawanielewi? mabo mengi yapo wazi family wanagombana kisa watoto wao,why wanataka kumuweka huyu mdogo wetu kwenye matatizo?
Bro wangu anasema unavyotaka wewe ndio hivyo hivyo ila hasimami na kuongea yuko busy na life yake anasema hao watu ni visiki hakuna haja ya kuwaelimisha hawaelewi,anyway ahasante sana mwenyezi mungu akupe busara hiyo hiyo na hekma..

Mtu hawezi kukuelewa hadi avae viatu vyako, awe amekumbana na changamoto kama yako, binafsi kuna changamoto ya kifamilia nilikutana nayo inafanana na hii kwa kiasi fulani.

Mimi na ndugu zangu tulimpoteza mzazi wetu miaka kadhaa iliyopita. Kabla ya kufariki mzazi wetu aliugua kwa kipindi kirefu na ilibidi tujipange na kuweka utaratibu wa kumpatia matibabu. Katika kipindi hicho cha kuugua, pamoja na huzuni ya mzazi kuugua, faraja tuliyokuwa tukiipata ni ukaribu tuliokuwa tukiiujenga miongoni mwetu sisi kama ndugu, na ukaribu tuliokuwa tukiupata kutoka kwa mgonjwa, ambapo kabla ya hapo, ilikuwa vigumu kuupata ukaribu huo kwa kuwa tulikuwa mbali mbali kutokana na majukumu ya kazi. Ilikuwa fursa nzuri sana kwa mgonjwa kutuambia mengi yaliyokuwemo moyoni na akilini mwake kabal ahajafariki.

Hatimaye mzazi wetu akatangulia mbele ya haki, na sisi kama watoto wake tukapanga na kuamua taratibu za mazishi kutokana na tulivyoona sisi inafaa. Cha ajabu wakajitokeza ndugu wengine wa mbali, na baadhi ya wazee wakataka utaratibu wa mazishi ubadlike kwa matakwa yao wao, na walikuja kwa hoja kwamba marehemu anawahusu. Tuliwagomea, lakini polepole baadhi ya ndugu zangu walijawa na hofu kutokana na shinikizo kutoka kwa hawa 'ndugu zetu wengine wa mbali', nilibaki peke yangu kutetea uamuzi ule. Hawakunielewa mwanzoni, lakini nilisimama kidete hatimaye walifuata tulichopanga ingawa kwa shingo upande. Miaka kadhaa imepita maisha yanaendelea, ndugu zangu wananishukuru kwa kuwasemea na hata baadhi ya wale ndugu sasa wananielewa kwa msimamo ule.

Ikuwa changamoto iliyoleta majaribu na kutaka kusambaratisha familia, lakini nilisimamia nilichoamini, nilipingwa sana lakini nami nikasema sitetereki, mwishowe walikuja kunielewa. Nafsi ingenitesa sana maishani mwangu laiti nisingetetea ninachokiamini.

Nilichojifunza ni kwamba kama unaamini kilichomo moyoni mwako, kitetee kwa nguvu zako zote hata wasipoelewa ni suala la muda tu, watakuja kuelewa.
 
Nimekuelewa Ahsante sana..
 
Back
Top Bottom