Nimekosea Wapi?

Nimekosea Wapi?

duh,,,, kuna familia ziko kama wanyamya.......wajua nguruwe kamwe hawezi mpanda dadake au hata mama..........hiki kizazi kigumu sana.....sijui heshima imehamia wapi.....anyway ndio utamaduni wenu...dumisha....
 
duh,,,, kuna familia ziko kama wanyamya.......wajua nguruwe kamwe hawezi mpanda dadake au hata mama..........hiki kizazi kigumu sana.....sijui heshima imehamia wapi.....anyway ndio utamaduni wenu...dumisha....
Kwa kabila na utamaduni wetu its okay wala sio tatizo..
 
Ahsante kwa ushauri mkuu,nimempa nafasi juu yakua amesema nnachoona mimi na ndugu wengine wakasema asiolewe aolewe na family yetu kwa wale wanaotaka maslahi yao,nimemwambia afikirie tena mda upo ila hakuna kitu sipendi kama vineno neno au kuekewa vikao..
Vineno neno ni sehem ya maisha, sasa kuliko aolewe na ndugu wa familia si bora shemeji? Mpe uhuru ajihukum mwenyewe
 
Pole kwa changamoto za maisha na hongera kwa kuonesha msimamo wao bila kuficha ...lakini hiyo ndio namna ya kukua.
Katika maisha yetu ya kila siku, huwa tunakabiliwa na changamoto, tunazikabili, tunazitatua, tunakuwa wazoefu wa maisha na hatimaye tunajenga uwezo zaidi wa kupambana na changamoto zingine kwa siku zijazo.

Ningekuwa kwenye nafasi yako, ningefanya kama wewe, tena ningefanya zaidi.... ningelaani na kukemea kwa nguvu zangu zote. Nisingekubaliana kabisa na wazo hilo la shemeji na mdogo wangu kufunga ndoa. Simamia kile unachokiamini na kipiganie kwa nguvu zako mpaka mwisho, kuna siku watakuelewa hasa mdogo wako. Anaweza asikuelewe leo lakini kuna siku moja atakuja kukushukuru kwa msimamo wako huo. Usifanye mambo au usiache mambo yaharibike kwa sababu unataka kuwafurahisha wengine.. waache wakasirike kuna siku watakuelewa. Kumbuka wewe umepewa dhamana ya kuwa 'Mlezi Mama', yaani wewe ni zaidi ya dada, hivyo una jukumu la kupambana na kulinda maadili na maslahi ya mdogo wako.

Unakumbuka tulipokuwa wadogo kuna mambo mengi tulitamani kuyafanya tukiamini yangetupa furaha sana lakini wazazi wetu walituzuia na tulikasirika sana, na hata wakati mwingine tuliwachukia, lakini baadaye tulikuja kuwaelewa na kuwashukuru kwa maamuzi yao ambayo kwa wakati huo tuliyaona mabaya. Kwasababu wao walisimamia kwenye ukweli. Wewe umesimama kwenye ukweli, endelea kusimama hapohapo hata kama unapingwa na kuchukiwa na watu wako wa karibu. Inapofika mahali unatetea 'damu' yako, usimumunye maneno hatakama 'hubby' wako na shemeji hawaoneshi furaha, achana nao wataizoea hali lakini wewe endelea kusimamia kile unachoamini.

Hii ni hoja nzito na tete, inahitaji mjadala wa hoja na sio kutishana wala kununiana miongoni mwa wanafamilia, kama kweli wana nia ya dhati kwa hicho wanachotaka kufanya waambie waelete hoja yao mezani, muijadili kwa hoja. Sio kwa kutishana kwamba eti, 'unamuharibia mdogo wako', hiyo sio hoja, hata mtu anapoamua 'kutoonesha furaha yake kwako' ni aina ya udhaifu, kwani kama ana hoja ya kweli anapaswa aiweke mezani. Waneleta na kufanya yote hayo ili wewe ushindwe hoja yako, ili wao waendelee.

Hata kama huko mbeleni watafanya ujanjaujanja na labda wakafanikiwa nia yao ovu, ni muhimu sana wewe uoneshe msimamo wako sasa kwamba hukubaliani na hilo, ili hata yakitokea ya kutokea huko mbeleni utabaki na heshima kwamba msimamo wako haukutetereka.
 
Inawezekana halioni sababu ni normal thing kwenye familia ila mara nyingi sana hua namuelimisha pindi wanapo gombana
hua namwambia unaona ingekua mtu wa nje unajua una solve vipi,mfano mtoto wa Baba mkubwa anampeleka mtoto wa baba mdogo mahakamani kisa anataka amkomoe amkodishie nyumba alipe school fees ya watoto,kwangu naona sio sawa na hao wazee kila mmoja ana vutia kwa mwanawe,mimi nikiwa na issue na mume wangu wanakuja kama nyuki wote wanakua pamoja mpaka sipeleki tena kesi yangu kwao wanamsema mumewangu mpaka namuonea huruma..
sasa staki na yeye awe na akili kama yao na yeye ndio namtegemea sana kwenye malezi ya watoto wangu ndio mana najaribu kumtayarisha Inshallah anielewe..
Ni jambo zuri unalofanya kumuonya mdogo wako!
Kiuhalisia sio jambo nzuri wote muolewe sehemu moja!

Ila wasi wasi unajua mpaka inafika kupropose ishu ya kuoana kunakuwa Kuna mengi sana ambayo yanakuwa yakiendelea behind the scene baina ya hao wawili!!
Sasa sijui kama walishafika mbali kwenye mahusiano yao unaweza kuwazuia!

anyway Mungu akusaidie ufanikiwe kumshawishi huyo mdogo wako
 
Ushampa ushauri unamuacha aamue mwenyewe sasa. Ni rahisi zaidi kumzuia mtu kwamba usito.mbwe/ Kuto.mba fulani kwasababu hii ama ile- lakini ni vigumu zaidi kumzuia mtu asiolewe / kuoa mtu fulani( kumbuka huenda hayo umeyafahamu baada ya wao wahusika kuwa ktk mahusiano kitambo tu pasi na ww kujua)
 
Kwanza nikupe pole kwa Unayopitia.
Ivi ni kitu gani kilisababisha mkaamua kuoana ndugu kwa ndugu.? Huo ni mfumo mbaya sana ktk Maisha ya binadamu. Tatizo kubwa mtakalokutana nalo ni uwepo wa Magonjwa Mengi ya kurithi ktk familia zenu. Mtatengeneza familia za Wagonjwa,Dunia ya sasa imebadilika sana na naamini wapo wasomi ktk familia sijui kwanini waruhusu vitu vya namna hii.

Unajua zamani baadhi ya tamaduni walifanya hivi kutokana na uhaba wa watu. Sasa Leo Tz pekee inawatu Million 50 kweli ukose mmoja wa kuoana nae.

Maadam umeamua kulikataa hilo nakushauri ushikilie msimamo wako ili kunusuru familia zenu.

Tafuta reference kutoka kwa madaktari juu ya magonjwa ya kurithi na mengine ambayo tayari yapo kwenye Familia yenu then nenda na nakala uwape kila mmoja ktk kikao cha Familia. Jaribu kuwaelewesha.
Usitumie Nguvu,Tumia nguvu ya Hoja. Hoja tayari unayo.

Lakini naomba kuuliza kidogo nyie ni kabila gani au wahindi....?
Baba Ni Mu Oman tabia zake niza Kiarabu kupitiliza,mkuu hakuna kitu hawa watu utawaeleza wakuelewe zaidi yakutumia force,kitu najivunia au kinachonisaidia jina langu nimepewa jina na Bibi mzaa baba na Dad humwambiii kitu kwa mamake
sasa mimi nikisema kitu hua ananisikiliza sana na najua ananipenda,na anajua kua nikiongea kitu hua mara nyingi sana nampa sababu,na kama kwenye hili yeye pia amesema sawa wewe ndio unamlea na ndio unajua nini kizuri kwake, kuna siku tuliwapeleka watoto hospital wa bro wana pumu balaa hakuna mwenye afadhali dr akasema sio vizuri kuoana familia moja,duu dr alichambwaaa mpaka nikaona aibu..
 
Ushampa ushauri unamuacha aamue mwenyewe sasa. Ni rahisi zaidi kumzuia mtu kwamba usito.mbwe/ Kuto.mba fulani kwasababu hii ama ile- lakini ni vigumu zaidi kumzuia mtu asiolewe / kuoa mtu fulani( kumbuka huenda hayo umeyafahamu baada ya wao wahusika kuwa ktk mahusiano kitambo tu pasi na ww kujua)
Naheshimu maamuzi yake ila ntajitahidi nimshawishi manake sio sawa...
 
Kuna kitu nadhani hakipo sawa! Hii tabia wanayo sana watu wa kanda ya ziwa.........
Kwa maisha ya sasa mpaka Sasa hawajagegedana kweli hao?

Halafu ulivyoandika inaonekana mdogo wako anakataa tu kuolewa na huyo Shemeji yako kwasababu tu Wewe umesema ila yeye haoni vibaya kuolewa na huyo Shemeji yako!
Nilitegemea yeye awe wa kwanza kukataa ila inaonekana Wewe Ndio unamshawish akatae........kwanini yeye haoni hilo?
Toa uongo wako hapa kanda ya ziwa kabila gani wanaoana kama wanyama kindugu ndugu hivyo usituaingizie mkuu.
 
Mmmh kwa mwanamke atakuwa ameenda sana umri aisee!
au kawaida kwa jamii yenu?
Kuolewa hakuna haraka mda ukifika ataolewa tuu inshallah muhimu asome ajue future yake anaipangaje kujisaidia ki maisha,wanaume wapo na wanawake wapo asome kwanza..
 
Toa uongo wako hapa kanda ya ziwa kabila gani wanaoana kama wanyama kindugu ndugu hivyo usituaingizie mkuu.
Sijasema uongo na siwezi kuwasingizia!
Nimeishi na wakurya mda mrefu na Shemeji zangu kabisa!!
najua nini nasema na nina uhakika
 
Back
Top Bottom