Nimekosea Wapi?

Nimekosea Wapi?

Sidhani kama ni sawa nna sababu nyingi sana za kukata,aolewe na mtu mwengine ila sio shemeji yangu hatuwezi kuolewa na familia moja..
Kama Issue ni wasiwasi wa watoto kuoana nafikiri hili linaongeleka, Ni suala la kukubaliana kwamba kama wataoana wahakikishe kuwa watoto wenu hawaowani.
Sidhani kama ni sawa kumfanyia mtu maamuzi ya yeye kuolewa au kutokuolewa na na nani, acha yeye mwenyewe aamue. Lakini kama una sababu nyingine zaidi ya ulizosema ok, ungea na mdogo wako azielewe na mwache yeye mwenyewe aamue, usimuamulie.
Tayari msimamo wako binafsi umewayumbisha wengi, Usiwe mbinafsi.
Ninaifahamu familia ya kaka 3 waliooa nyumba moja.Wanaelewana na kusaidiana vizuri.
 
Nadhani unakuwa mbinafsi zaidi kwa sababu unaliangalia hili kwa upande wako tu. Muache mdogo wako aamue maisha yake, kama wewe ulivyoamua ya kwako na familia ikaheshimu japo kwa shingo upande.
 
Pole kwa changamoto za maisha na hongera kwa kuonesha msimamo wao bila kuficha ...lakini hiyo ndio namna ya kukua.
Katika maisha yetu ya kila siku, huwa tunakabiliwa na changamoto, tunazikabili, tunazitatua, tunakuwa wazoefu wa maisha na hatimaye tunajenga uwezo zaidi wa kupambana na changamoto zingine kwa siku zijazo.

Ningekuwa kwenye nafasi yako, ningefanya kama wewe, tena ningefanya zaidi.... ningelaani na kukemea kwa nguvu zangu zote. Nisingekubaliana kabisa na wazo hilo la shemeji na mdogo wangu kufunga ndoa. Simamia kile unachokiamini na kipiganie kwa nguvu zako mpaka mwisho, kuna siku watakuelewa hasa mdogo wako. Anaweza asikuelewe leo lakini kuna siku moja atakuja kukushukuru kwa msimamo wako huo. Usifanye mambo au usiache mambo yaharibike kwa sababu unataka kuwafurahisha wengine.. waache wakasirike kuna siku watakuelewa. Kumbuka wewe umepewa dhamana ya kuwa 'Mlezi Mama', yaani wewe ni zaidi ya dada, hivyo una jukumu la kupambana na kulinda maadili na maslahi ya mdogo wako.

Unakumbuka tulipokuwa wadogo kuna mambo mengi tulitamani kuyafanya tukiamini yangetupa furaha sana lakini wazazi wetu walituzuia na tulikasirika sana, na hata wakati mwingine tuliwachukia, lakini baadaye tulikuja kuwaelewa na kuwashukuru kwa maamuzi yao ambayo kwa wakati huo tuliyaona mabaya. Kwasababu wao walisimamia kwenye ukweli. Wewe umesimama kwenye ukweli, endelea kusimama hapohapo hata kama unapingwa na kuchukiwa na watu wako wa karibu. Inapofika mahali unatetea 'damu' yako, usimumunye maneno hatakama 'hubby' wako na shemeji hawaoneshi furaha, achana nao wataizoea hali lakini wewe endelea kusimamia kile unachoamini.

Hii ni hoja nzito na tete, inahitaji mjadala wa hoja na sio kutishana wala kununiana miongoni mwa wanafamilia, kama kweli wana nia ya dhati kwa hicho wanachotaka kufanya waambie waelete hoja yao mezani, muijadili kwa hoja. Sio kwa kutishana kwamba eti, 'unamuharibia mdogo wako', hiyo sio hoja, hata mtu anapoamua 'kutoonesha furaha yake kwako' ni aina ya udhaifu, kwani kama ana hoja ya kweli anapaswa aiweke mezani. Waneleta na kufanya yote hayo ili wewe ushindwe hoja yako, ili wao waendelee.

Hata kama huko mbeleni watafanya ujanjaujanja na labda wakafanikiwa nia yao ovu, ni muhimu sana wewe uoneshe msimamo wako sasa kwamba hukubaliani na hilo, ili hata yakitokea ya kutokea huko mbeleni utabaki na heshima kwamba msimamo wako haukutetereka.
Mkuu Ahsante sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa zaidi ya sanaaaaaaaaaaa,kwakusimama na mimi japo hunijua ila mwenyezi mungu ndio atakae kulipa kwani sio rahisi mtu kunielewa nna maana gani,na ndio mana kuna time hua nalia sababu angekuwepo mama afadhali angenisaidia, naandika huku machozi yananitoka nahisi napiga peke yangu na hakuna wakunielewa japo kwa mawazo, najiuliza kwanini hawanielewi? mabo mengi yapo wazi family wanagombana kisa watoto wao,why wanataka kumuweka huyu mdogo wetu kwenye matatizo?
Bro wangu anasema unavyotaka wewe ndio hivyo hivyo ila hasimami na kuongea yuko busy na life yake anasema hao watu ni visiki hakuna haja ya kuwaelimisha hawaelewi,anyway ahasante sana mwenyezi mungu akupe busara hiyo hiyo na hekma..
 
Naheshimu maamuzi yake ila ntajitahidi nimshawishi manake sio sawa...
Ukute kwa upande wake yeye anaona sawa ndio shida itakapoanzia hapo.

Kwasababu wakati mwingine mtu hakubishii lakini moyoni mwake anapingana na wewe. Mshirikishe Mungu pia kwa maombi atakusaidia kulivuka hilo
 
Nadhani unakuwa mbinafsi zaidi kwa sababu unaliangalia hili kwa upande wako tu. Muache mdogo wako aamue maisha yake, kama wewe ulivyoamua ya kwako na familia ikaheshimu japo kwa shingo upande.
waliheshimu sababu niliwambia reason na baada ya muda wameiona,mkuu sitokubali makosa walofanya wale na huyu ayafanye mimi ni mlezi wake na sio adui yake siwezi kumtia kwenye matatizo mdogo wangu ila nataka aone kwanini nimechukua maamuzi haya..
 
Ukute kwa upande wake yeye anaona sawa ndio shida itakapoanzia hapo.

Kwasababu wakati mwingine mtu hakubishii lakini moyoni mwake anapingana na wewe. Mshirikishe Mungu pia kwa maombi atakusaidia kulivuka hilo
Inshallah,Ahsante sana kwa mawazo yako..
 
Back
Top Bottom