Nimekosa Mkopo benki kisa nilichelewesha rejesho mwaka 2018 kwa siku 60

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,545
9,944
Wadau njooni hapa tufarijiane.

Huko serikali imeshaweka mazingira magumu Tena kwenye kukopa. Mimi 2018 nilichelewesha rejesho kwenye Moja wapo benki hapa nchini. Mambo ya yangu hayakwenda vizuri, nilicheleweshewa malipo sehemu, ila benki tulikuwa tunawasaliana vizuri tu.
Badae nikalipa na mda wote huo benki wamekuwa wakinipa Mkopo bila shida yoyote.

Saa wiki juzi nikaomba Mkopo, kuna watu wa Credit info wakaja na report eti Mimi sikopesheki kwa sababu nacherewesha malipo.

Serikali imetengenza hiki kitego ila hakina ufanisi kabisa.
Benki wanataka kunipa Mkopo ila Credit infor wameweka ngumu. Nami nimeagiza mzigo ukifika kabla sijapata hela basi nitakuwa na bonge la hasara.

cc. Mwigulu Nchemba.
 
Watz wengi kwa sasa wako huko maana mikopo mingi ya simu usipolipa wanakuweka huko
Naona mabenki pia yanahaha,maana wanatamani kuwakopesha watumishi lakini bahati mbaya mtumishi hakopesheki kwa sababu ya record mbaya ya kutolipa. Hata ukiwa unadaiwa elf tano,, record husika ipo.

Ninacho ona benki itapoteza wateja wengi mnoo,hasa watumishi. Ni wakati wa micro finance kupiga hela
 
Kama baada ya kuchelewesha kulipa 2018 lakini ulipoilipa uliendelea kukopeshwa na mara hii unawekewa ngumu siyo kwamba kuna watu wanataka wajue wanaishi vipi kwenye hii issue na wewe hutaki kufunguka?

Inaweza ikawa ni ishu ya kimaslahi jamaa wanakuona ukisogea huku wao hawaelewi,jaribu kukaa nao mezani waulize shida ni nini ili uone uelekeo wao.
 
Niko Makini sana, shida ni hao credit info. Ila benki hawana shida kabisa. Na humu nimeona wengi wanalalamikia jambo hili
 
Kama baada ya kuchelewesha kulipa 2018 lakini ulipoilipa uliendelea kukopeshwa na mara hii unawekewa ngumu siyo kwamba kuna watu wanataka wajue wanaishi vipi kwenye hii issue na wewe hutaki kufunguka?

Inaweza ikawa ni ishu ya kimaslahi jamaa wanakuona ukisogea huku wao hawaelewi,jaribu kukaa nao mezani waulize shida ni nini ili uone uelekeo wao.
Thread closed.
 
Huu uhuni utawanufaisha watu wasio hata na leseni ya biashara hii ya kukopesha.

Na common mwananchi atakutana na riba za ajabu.
 
Back
Top Bottom