Nimekoma kukagua simu ya mume wangu

Hilo sio suluhisho la tatizo hata kidogo. Hutoipata hiyo furaha zaidi ya maumivu zaidi. Mwenzako atafanya hayo anayoyafanya na mchepuko wake kwa ajili ya furaha, ila wewe unayelipiza kisasi hutofanya kwa furaha bali kisasi.

Ha ha ha haa
Wapi nimeandika ya kuwa ni kulipiza?
Kama mume anaenda kupata furaha ambayo anaona ni bora ampe mchepuko.. basi jua na mke anaenda kupata furaha kutendewa yale mume hampatii raha na furaha.. mkome wanaume.. ngoma draw wote ni furaha tu kupata huko nje.
 
Ha ha haaaaaa hapo mwanamke hajiumizi wala hajidhalilishi.. bali anatafuta furaha na rafiki wa kumpa raha na kumdhamini kama mwanamke akina Fadhili.. hujasoma story ya mama Davis

Huyu mwenzetu labda ndoa yake ilishakuwa bomu.. akawa anaona simu ndio ndoa huku labda furaha hawana kwa muda mrefu au makosa ya kila mmoja hawasemani wabadilike.

Labda hii itamsaidia atulie aone wapi nae anakosea ili awe bora kwa mchepuko wake.. eeeeeh akimbeba mazima sawa.. wanaume nyie ni hamjui mnaua wanawake mapema tu

Sho hiyo story ya mama Davis naisoma wap
 
Uislam raha sana, haujaacha kitu...

49_12.gif

12. Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu
 
Mimi Mawazo yangu ni kuwa
Humpi akatosheka ndio anakimbilia Nje kupewa kwa kunogewa Ama kakimbilia network za mtandao pendwa 0713....
Ni Hatari Kwa Afya yako
 
Mimi dume,nakwambia hivi,acha kihere here,wewe umeolewa,maana yake ndo unapendwa,mengine hayakuhusu
wanaume hatuchunguzwi,ili mradi unapata mahitaji mengine achana nayo mdogo wangu,ona sasa yaliyokukuta..
Na vipi kama mwanamke ndiye anahudumia familia mahitaji yote...in short ndiye mwenye kipato, still akae kimya?
Na je akikaa kimya awe tayari kuletewa magonjwa?
 
Dada nakushauri msome Iddi Makengo instagram utapata jibu la huyu mume wako
 
Habari za usiku huu waungwana..naamini wote mko salama.

Niwaambie yaliyonikuta sasa..week kama tatu zilizopita nilianza kuhisi mume wangu anakimada ila sikutaka kumuuliza wala sikutaka ajue kama nahisi anachepuka.

Mumewangu alikua na tabia ya kuwahi kurudi nyumbani au hata kama anajua anachelewa hua lazima apige simu kunitaarifu.

Mumewangu alikua amenipa Uhuru na simu yake hata kama anaoga alinipa ruhusa niipokee na niongee na mpigaji na sio tu mimi Uhuru huo aliwapa hata watoto wake.

Wiki tatu zilizopita nikaona mwenzangu ameanza kubadilika..hatuna ruhusa ya kushika simu..hata kama inaita atatoka bafuni na apovu lake ataichukua simu maongezi yatafanyika bafuni..ukali ukaanza kwangu na watoto hata kama haikua na haja ya kutukalipia.

Nikaanza kufuatilia mwenendo wake ndipo nilipogundua ana mwanamke..leo asubuhi nikasubiri ameenda kuoga nikachukua simu bahati nzuri nywila yake naifahamu nikapunguza sauti nikaanza kupekua kwenye whatsapp.

Nikakutana na picha za tupu za huyo mwanamke huku wakisifiana wanavyofurahishana kitandani..nilijikuta sina nguvu kwakweli..ghafla na yeye akatoka bafuni akavaa huyo akaondoka hata kifungua kinywa hakupata.

Muda wa kama nusu saa hivi nikamtumia meseji
Mimi: "ahsante nimeona na nimejua kila kitu"
Mumewangu: "umekipata ulichokua wakitafuta na ukome"
Mimi: "yani Mume wangu ndio wanijibu ivyo?"
Yeye: "tena umenikera na sirudi Leo "

Yani ninavyoandika hapa hadi sasa 11:36pm huyu mwanaume bado hajarudi na simu yake haipatikani.

Wanawake wenzangu naomba mnishauri nifanye nini?

Wanaume mnahisi alichokifanya mwanaume mwenzenu ni sahihi?

Hizi ni simulizi tu. Kama ni kweli weka picha hapa ya huyo mchepuko wake na sms chart kati yako na yeye
 
Ni sahihi ningekuwa mimi ningekaa wiki 2 ndiyo nirudi..
 
Usipate shida uko wapi dawa ya moto ni Moto namba hiyo 0784577642 na wewe ni binadamu na una hisia nitafute tumalize
 
Back
Top Bottom