Nimekoma kukagua simu ya mume wangu

Nimekoma kukagua simu ya mume wangu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mwenza we kaa nae tu, ngoja kwanza nami nipumue kidogo. Kaa kaa nae hadi mwezi wa tisa.
Heee mwezi wa 9??? Hapana lazima akuje kukupa haki yako...loh😂😂
 
Habari za usiku huu waungwana..naamini wote mko salama.

Niwaambie yaliyonikuta sasa..week kama tatu zilizopita nilianza kuhisi mume wangu anakimada ila sikutaka kumuuliza wala sikutaka ajue kama nahisi anachepuka.

Mumewangu alikua na tabia ya kuwahi kurudi nyumbani au hata kama anajua anachelewa hua lazima apige simu kunitaarifu.

Mumewangu alikua amenipa Uhuru na simu yake hata kama anaoga alinipa ruhusa niipokee na niongee na mpigaji na sio tu mimi Uhuru huo aliwapa hata watoto wake.

Wiki tatu zilizopita nikaona mwenzangu ameanza kubadilika..hatuna ruhusa ya kushika simu..hata kama inaita atatoka bafuni na apovu lake ataichukua simu maongezi yatafanyika bafuni..ukali ukaanza kwangu na watoto hata kama haikua na haja ya kutukalipia.

Nikaanza kufuatilia mwenendo wake ndipo nilipogundua ana mwanamke..leo asubuhi nikasubiri ameenda kuoga nikachukua simu bahati nzuri nywila yake naifahamu nikapunguza sauti nikaanza kupekua kwenye whatsapp.

Nikakutana na picha za tupu za huyo mwanamke huku wakisifiana wanavyofurahishana kitandani..nilijikuta sina nguvu kwakweli..ghafla na yeye akatoka bafuni akavaa huyo akaondoka hata kifungua kinywa hakupata.


Muda wa kama nusu saa hivi nikamtumia meseji
Mimi: "ahsante nimeona na nimejua kila kitu"
Mumewangu: "umekipata ulichokua wakitafuta na ukome"
Mimi: "yani Mume wangu ndio wanijibu ivyo?"
Yeye: "tena umenikera na sirudi Leo "

Yani ninavyoandika hapa hadi sasa 11:36pm huyu mwanaume bado hajarudi na simu yake haipatikani.

Wanawake wenzangu naomba mnishauri nifanye nini?

Wanaume mnahisi alichokifanya mwanaume mwenzenu ni sahihi?
Ndio ni sahihi
 
Usijaribu tena hiyo itakupelekea uvunje ndoa yako Usipende kumshuku mume wako wewe ndio mwenye thamani ndio maana kakuweka ndani ya nyumba achana na hao wa nje itakupotezea muda Muheshimu,mpende na tekeleza wajibu wako kama mke ukifanya hivyo utaishi miaka mingi na ndoa itadumu.
 
Bora huyo wako, wangu nilimwambia umeyatafuta mwenyewe, malizana nayo mwenyewe, usinishirikishe [emoji23][emoji23] akaingia front, mchepuko ulikiona cha mtema kuni, nami nikasema mke ninaye
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom