Nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam

Nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam

Waungwana nisaidieni, nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam, wakwe wanasema sifa zooote ninazo ila dini yangu eti sisi wengi wetu ni magaidi, bibie yeye yuko radhi tufunge ndoa bila ridhaa ya wazazi ila mimi naona haiwezekani hususan kwa tuhuma hii ya kidini, sasa wanajamii mnanishauri nini na upande wa dini je inaswihi ndoa ya ilofungwa bila ridhaa ya wazazi,, habari hii si ya kubuni hivyo naomba muelewe hivyo

If you can't beat them, join 'em
 
wewe pia dini yako hauijui vizuri, hebu tafuta muda usome kurani...muislam aoe muislam...
 
"
Safi sana, ahhh lakini inategemea una kashfu dini gani, mana ukikashfu wanao abudu sanam, sidhani kama utapata kipigo-mana sanam halisikii wala kuona.

kama unaweza muelimisha , muelimishe, ukiona hataki nyamaza, maana ukikashifu zio vizuri, maana hapa duniani tunaishi kwa kutegemeana , sidhani wewe Fazaa hapo unapochumia ugali wako wa kila siku mko waislam watupu/wakristo watupu haiwezekani ni lazima mchanganyike. So mm naona kama unaweza muelimisha mtu bila kumkashifu hiyo ni nzuri zaidi.

Ukikaa kimya utaonekana unahekima, muungwana, na mwenye busara kuliko kuongea sana watu watakudharau. "MUUNGWANA NI VITENDO SI KUONGEA"
 
Hapana hata Mwenyezi Mungu anasema hapendi wajinga, huwezi kukaa kimya ukiona kuna wajinga, lazima uwape elimu ili wajue kama wanakosea :biggrin1:
 
Kama vp umezimia mzigo take risk, sometime wazazi nao mikwara sana, mwambie binti akawatishe kuwa bila wewe yeye anajiua utafungishwa ndoa chapchap. Kama wakiwa manunda potezea oa muislamu mbona wako kibao tu tena wengine mchanganyiko wa kishombe flani acha mchezo, utafikiri simba serengeti anatafuna swala mtoto.
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokufika

Sio wewe peke ni wengi yamewakuta haya na bado yataendelea kuwakuta wengine pia kwa sababu Mapenzi huwa hayachagui, si dini, rangi wala kabila ukipenda umependa!

Mi binafsi huwa binafsi siamini katika ndoa ya dini tofauti kwa sababu ya madhara yake ya baadae, mfano mnaoana ili mjenge familia imara na yenye upendo na watoto wenu muwafunze tabia njema na kuwaonyesha upendo mkiwa pamoja(otherwise mngeendelea kuishi tu hivohivo). Sasa unapoa mtu wa dini tofauti hayo mambo yanapatikana kwa tabu ingawa yanawezekena! na pili kuwa na fikra ya pamoja katika familia yenu kutaongeza upendo na itakuwa sababu ya kurudisha upendo iwapo mtakosana (as both of u will have the same reference point (biblia/msahafu), wazazi na hata marafiki)!

Kwa hiyo cha muhimu ni kwanza pumzikeni kuwagasi wenyewe ongeeni mustakabali wenu nyie wenyewe (kama mmoja atabadilisha dini au la, iwapo hamtabidilsha je ni maadili gani ya kufuatwa na nyie au watoto wenu) then mkiungana mtakuwa na nguvu ya kuwashawishi wazazi kwa pamoja!

Ikishindikana mjue mbele ni giza bora muachane kwa amani(sorry for saying that)

Wishing you the best
 
Na kila mtu asikilize haja ya MOYO wake... mkuu kama unahisi huyo mwanamke ni mpenzi wako wa maisha, (love of your life),.. take risk then badili dini bila ivyo amini nakuambia laana ya wazazi ni kubwa hamuwezi kui-handle, pili mtashindwa kujenga familia imara kila mtu akiwa ameshika lake katika familia ila tu kumbuka usilazimishe mambo, ikishindikana yeye kubadilisha dini, au ww kubadilisha dini, call off the relationship and move on , though it pains lakini with time utakuwa powa. This time usifanye makosa tafuta ustaadhat usijichanganye.
BTW jamani acheni kukashifiana dini haina tija...
 
kwa mujibu wa misingi ya kiislam inaswihi ikiwa wazazi hawana sababu za msingi.ila kijamii ni hatari.mtapigwa na dhoruba ambayo hamtaiweza.chakufanya tumieni uwezo wenu wa kidiplomasia kuwashawishi wazazi.kuhusu waislam kuhusishwa na fujo;tuwalaumu watu jamii ya kina ponda ndo waaotufikisha hapa.
naomba ufafanuzi hapa, hata binti wa kiislam akitaka kuolewa lkn wazazi wakiwa hawako radhi inaswihi?
 
naomba ufafanuzi hapa, hata binti wa kiislam akitaka kuolewa lkn wazazi wakiwa hawako radhi inaswihi?

inategemea kama wazazi hawana sababu za mcingi zilizokatazwa na dini inaswihi kuolewa bila ridhaa yao bt viceversa z tru
 
Na mimi hamjui mnavyo nikera kumfananisha Mungu na binadamu, afu mmepigilia na misumari msalabani.

Kawaida Mu islam kuoa Mu Islam sio kwenda kuoa kwa wanamshirikisha Mungu.

wewe hatuhubiri imani za dini hapa kama unaona wanakutia hasira wafate huko, jf haina itikadi pls
 
inategemea kama wazazi hawana sababu za mcingi zilizokatazwa na dini inaswihi kuolewa bila ridhaa yao bt viceversa z tru
sababu ya msingi ni moja tu. kwa kuwa si wa dini yao je hiyo si sababu ya msingi.
 
sababu ya msingi ni moja tu. kwa kuwa si wa dini yao je hiyo si sababu ya msingi.

hiyo ni ya mcingi kwa imani yao so hapo hakuna kuforce u have to respect wazazi coz wapo right unles huyo mtoto aamue kusema ye kaingia hiyo imani nyingine na inategemea huko anakokwenda micingi yake ipo vipi
 
kwa waislam najua haikubaliki wazazi kuridhia bint yao kuolewa na mkristo, bila kubadili dini kuwa muislam japo kuna andiko mwanamke hana dini.alikadharika mwanaume haruhusiwi na wazazi kumuoa mwanamke mkristo bila kubadili dini kuwa muislam. na hili liko pia kwa baadhi ya madhehebu ya kikristo lkn WAKATOLIKI wako tofauti si lazima muoaji/ muolewaji kudadili dini ila atapitia mafundisho ya dini, hatalazimishwa kubadili ila ndoa itafungwa kwa imani ya kikatoliki na kila mmoja atabaki na imani yake.
 
Kama mnapendana kiasi hicho kiasi cha wote kuwa tayari kufunga pingu za maisha na yeye yuko tayari kuwa nawe bila ridhaa ya wazazi wake basi endeleeni na maandalizi ya harusi yenu. Ila uwe tayari kumpenda kupita kiasi, kumjali kupita kiasi na kumheshimu kupita kiasi ili hata wazazi wake na nduguze wakiamua kumtenga kwa uamuzi wake wa kuolewa nawe isifikie wakati akajilaumu kwamba alifanya makosa makubwa sana ya kuamua kuolewa nawe bila ridhaa ya wakwe zako. Kila la heri Mkuu.

Waungwana nisaidieni, nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam, wakwe wanasema sifa zooote ninazo ila dini yangu eti sisi wengi wetu ni magaidi, bibie yeye yuko radhi tufunge ndoa bila ridhaa ya wazazi ila mimi naona haiwezekani hususan kwa tuhuma hii ya kidini, sasa wanajamii mnanishauri nini na upande wa dini je inaswihi ndoa ya ilofungwa bila ridhaa ya wazazi,, habari hii si ya kubuni hivyo naomba muelewe hivyo
 
Last edited by a moderator:
ninyi mnawaita wenzenu makafiri. why unataka kuoa kafiri?

mtazamo wangu:

kwa wazazi walio makini (wenye umakini wa kutosha na ukristo wao) kamwe hawawezi kuruhusu mtoto wao kuolewa na muislamu, kamwe. na kwa trend tunayoenda nayo hata ningekuwa mimi nisingekubali binti yangu kolewa na muislamu.

uwe mwangalifu kwa sababu ukiamua kuoa bila ridhaa ya wazazi wa binti unaweza kupata laana maisha yako yote badala ya baraka.

by the way "i am just trying to think loud"
 
Kila mtu awe anatoka na watu wa dini yake, la sivyo mnakuja kuumizana tu...
 
naomba ufafanuzi hapa, hata binti wa kiislam akitaka kuolewa lkn wazazi wakiwa hawako radhi inaswihi?
inategemea sababu ya wazazi kukataa.kama ni ya kimsingi na inayokubalika kidini,ndoa hiyo haitawezekana.lakini kama ni mbwembwe tu,inaweza kufungwa na kadhi na ikakubalika.hata hivyo sikushauri kufunga ndoa na mwanamke kabla wazazi wake hawajaridhia kwa sababu kwa kufanya hivyo utakumbana na majanga makuu.
 
wewe hatuhubiri imani za dini hapa kama unaona wanakutia hasira wafate huko, jf haina itikadi pls
Hahaha hakuna anaye hubiri hapa, jamaa kauliza swali na sisi tunamjibu swali.

We kama ndo wale kina mkwawa basi bora utulize ball, mana usiende kwenye dini mana bado sana kufika huko na ukienda huko utakwama tu, hutanishinda utabaki kama yule mkwaya akawa hajui anaongea nini.

Tazama thread inasema nini kwanza kabla ya kuanza poroja zako ambazo si za msingi.
 
Back
Top Bottom