Speaker
JF-Expert Member
- Aug 12, 2010
- 6,324
- 2,242
Waungwana nisaidieni, nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam, wakwe wanasema sifa zooote ninazo ila dini yangu eti sisi wengi wetu ni magaidi, bibie yeye yuko radhi tufunge ndoa bila ridhaa ya wazazi ila mimi naona haiwezekani hususan kwa tuhuma hii ya kidini, sasa wanajamii mnanishauri nini na upande wa dini je inaswihi ndoa ya ilofungwa bila ridhaa ya wazazi,, habari hii si ya kubuni hivyo naomba muelewe hivyo
Achana nae,
Tafuta mwenye imani kama yako,usije msumbua dada wa watu
au yeye kukusumbua hapo baadae.
Mnaunganisha spirits,kama hamfanani kiimani,hamfanani kabisa
kufunga ndoa. Wazazi wako sahihi