Nimekataliwa kisa........!

Nimekataliwa kisa........!


yani huyo hakupendi hata chembe
akupendae haangalii pesa kama kigezo!!
huko ni kupenda usipopendwa!!utaumia bureee!!

Sioni ubaya wa Bi-dada yeye ana-standard zake.Mimi nnaponunua gari kama ni la kutumia mimi mwenyewe siagizi lisilo na Four wheel drive (4x4) siyo gari ni gari tu kwani mi najijua nipo rafu na foleni za Dar mi hufanya gari path finder (kupita kandoni mwa brbra ili niwahi kufika.hivyo naye dada pamoja na kupenda kuna -added factors (pochi) siyo ilimradi awe tu mwanaume!Ndo maana mimi niingiapo baa najijua mimi ni wa serengeti siwezi kuagiza zile za kupigia picha znaitwa..nini tena zile...Heineken na jamii yake.Ivyo Blaza-kaka naye akubali tu kwamba wa moja abaki na moja asitake kuwa wa mbili.Sasa Pasheni Ledi si umpende basi uyu jamaa kama una uzalendo wa kweli?

I wish ningekuwa demu..ubaya nimeumbwa nina huruma na haya sijui ingekuwaje kwani singependa kuNkatalia Ntu kitu Nnacho.
 
Kijana usilalame ,,,, fanya kazi tafuta pesa ukipata kamtongeze ufaidi mahabati.

Ha ha ha,zikiisha? Tatizo jamaa hapo anataka aoe,madem kama hao ni kuchapa unalala mbele. Kuna demu wa kuoa na wa wahuduma.Mia
 
Tatizo wewe unatongoza mademu wanao jua unafanya nini, tafuta asiye jua mishe zako, siku hiz mademu hawaambiwagwi ukweli. halafu ukimpata mtumie fasta akishajua mishe zako unamtema fasta... vinginevyooo mmmh.
 
Mapenzi kweli kizungumkuti,yanayonikuta yanautesa sana moyo wangu.
KUna msichana ambaye ninampenda sana toka siku nyingi na yeye aanalijua hilo,ila kila nikimueleza juu ya hisia zangu uu yake yeye huishia kusema NAKUPENDA ILA HATUWEZI KUWA PAMOJA KWAKUWA HAUNA KAZI,HUNA PESA.

Hiki kitu kinaniumiza sana kwani kukosa kwangu kazi na kukosa pesa kunanifanya nimkose mtu ninayempenda kwa dhati,pia najiuliza hivi siku hizi ndio mapenzi hayawezakani tena mtu aspokuwa na pesa/kazi?ndugu mwana-jamvi,fikiria kama wewe ndio ungekuwa umepata na situation kama hii inayonikumba mimi ungefanyaje?(kumbuka hii ni very true story)

Hivi mwanamme haswa anakosa kazi ya kufanya? Unanshangaza!

Hebu panga hata ndizi nje ya unapoishi utaona kama si kazi yenye kukuingizia pesa.

Inasikitisha sana kwa mwanamme kutangaza kuwa huna kazi. Huyo dada aliekupiga chini, kishaona hufai, nampa heko sana.

Mwanamme labda useme hujafanikiwa kupata kazi uitakayo na unajishughulisha kwa kazi nyingine yoyote na huku unaendelea kuitafuta uipendayo. Lakini hilo la mwanamme kutokuwa na kazi ya kufanya linasikitisha sana.

Janadume linalojisifia eti halina kazi, lina faida gani hilo?
 
ndo pakutafuta kazi upate hela ili umnase umtakaye.

kimsingi mwanaume asokuwa na kazi kuwa nae kwenye mahusiano ni mzigo wa gunia la misumari. utamtesa sana huyo dada kwasababu utamnyima raha kila muda utanung'unika tuuuuuuuu kisa yy anafanya kazi ww ni kama kochi tu humo ndani

aisee sijui kwanini wanawake mnawazaga tu kupewa, kutafutiwa, kulishwa, kunyweshwa, kulazwa na kupakatwa!

hivi kwanini na nyie msipate wanaume wasio na kazi ilhali nyie mkiwa na kazi ili msaidiane pole pole?

mnasubiri tu waume wafe mdai mali!!

ile nyie wanawake nyie!
 
Nina stori inayoendana na yako. Na wakati namtokea huyo binti nilifanya makusudi nione kuwa je, upendo wake unategemea nilicho nacho mfukoni ama!

Sikuamini macho na masikio, nilipomwambia ukweli kuwa mimi sina kazi, bado natafuta, sina kipato cha uhakika, bado nategemea ndugu kwa kiasi fulani.... wala yule binti hakusita! Alinionyesha upendo, alinipa nguvu pale nilipoonyesha kukata tamaa mpaka hali ikawa nzuri!

Huyo binti hataki shida, anataka mwanaume aliyenacho, hataki kusaidia ili mtafute pamoja. Kama unatumia akili, basi tafuta mwanamke atakayekupenda wewe na si ulichonacho... hamna binadamu aliyeandikiwa kuwa nacho siku zote!
 
Hivi mwanamme haswa anakosa kazi ya kufanya? Unanshangaza!

Hebu panga hata ndizi nje ya unapoishi utaona kama si kazi yenye kukuingizia pesa.

Inasikitisha sana kwa mwanamme kutangaza kuwa huna kazi. Huyo dada aliekupiga chini, kishaona hufai, nampa heko sana.

Mwanamme labda useme hujafanikiwa kupata kazi uitakayo na unajishughulisha kwa kazi nyingine yoyote na huku unaendelea kuitafuta uipendayo. Lakini hilo la mwanamme kutokuwa na kazi ya kufanya linasikitisha sana.

Janadume linalojisifia eti halina kazi, lina faida gani hilo?

Mpaka FAIZAFox kasema kweli vijana tubadilike!!
 
Ningezitafuta hela usiku na mchana bila kupumzika ila huyo bidada hakufai jamaa jipange.
 
huyo hakupendi wewe... yeye anapenda utakachokua nacho!
cha muhimu muweke pending halafu tafuta kazi ukishapata tu ndo mfuate tena ila sio kwa kukaa bali kupita tu.
ili roho yako iridhike.
mwanaume majukumu babu!
 
Naona hapa ni mwendo hapendwi mtu inapendwa pochi
 
inamaana usipompata huyo maisha yako hayataenda tena zaidi ya hapo?
 
Pole sana hata chakusema sina! money! money!!!
 

Attachments

  • Money is paper!.jpg
    Money is paper!.jpg
    8.6 KB · Views: 58
kwa maana hiyo wanaume wote wasiokua na pesa wala kazi hawana wanawake?

sio kwelii! hajampata wife material wake kakutana na wadada wa mujini macalculation kwanza hana hela for now ok fine hata future pia haioni loolz! huyo hamtaki amemtafutia sababu. kaka kajipange upya kwingine lakin utasoota kwa sasa uku mjini hali ndio io inapendwa pesa kwanza.
 
ni adhabu kupenda usipopendwa. Hivi kwanin umng'ang'anie? Mwanamke ni yeye peke yake? Wako wanaokesha kuomba kupata wakumpenda. Usismame kwenye mlango mmoja uliofungwa, ilihali ipo mingne 100 wazi.

Mara nyingi ndivyo inavyokuwa,unapenda sana pale usipopendwa,lakini itabidi niichukulie kama changamoto ya mii kutafuta zaidinili nikipata aje aone mafanikio yangu na jaue no situation is permenent
 
inamaana usipompata huyo maisha yako hayataenda tena zaidi ya hapo?

yataenda ila kwa shida sana kwasbabu ni msichana mzuri sana na anaukosha sana moyo,kumkosa itakuwa pigo sana kwangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom