Nimekataliwa kisa........!

Nimekataliwa kisa........!

Pole kijana sasa hivi hamna mapenzi kuna biashara na ndio maana mtu anaefika bei ndio anapata bidhaa.Wala usilalame maana kuna mwenzio nilikutana nae yeye amemsomesha chuo binti halafu binti kamuona kenge baada ya kumaliza .Ni jambo jema la kumshukuru mungu maana hujui kama huko mbeleni ingekuaje halafu ni wakati wa ww kutafuta pesa ukachukua bidhaa nzuri sokoni.

nimeiona hiyo avatar yako mkuu,imenitia hamu sana ya kuzisaka labda amani ya nafsi itapatikana,lakini hofu yangu itakuwa ni kwamba nanunua upendo
 
Akunyimae kunde anakupunguzia mashuzi. Achana nae utapata wako atakaekukubali. Maisha ni kupanda na kushuka, ndoa inataka kuvumiliana in the sense ya kuaccomodate each other. Tafuta hela umdolishie na sio kumnasa
una ushauri nzuri sana ubarikiwe
 
wanawake wa 21 century walishatangaza mapemaaaaa bila fedha no love
 
Maisha magumu haya ujue bora kakwambia ukweli kuliko angekukubalia af awe na wengne wa nje wenye pesa zao..
Ndo utafute kazi sasa nawe,ila kiukweli huyo hajakupenda wala nini ambae angekupenda asingekupa hayo makavu live namna hyo,angevumilia tu af bidae angekwambia in a polite wa.y
..
 
huyo hakupendi wewe... yeye anapenda utakachokua nacho!
cha muhimu muweke pending halafu tafuta kazi ukishapata tu ndo mfuate tena ila sio kwa kukaa bali kupita tu.
ili roho yako iridhike.
mapenzi yamepata transformation kubwa sana,hajaliwi mtu,inajaliwa pesa(material things)
 
nimeiona hiyo avatar yako mkuu,imenitia hamu sana ya kuzisaka labda amani ya nafsi itapatikana,lakini hofu yangu itakuwa ni kwamba nanunua upendo
Kwa huyo si utakua unanunua upendo bali utakua unanunua mchezo,maana she is not a wife material...mtoe kabsa katka mawazo yako
 
Umenena vyema sister,mgekuwa kama kumi tu humu JF basi hata zile thread za sijui wote wanauza zisingekuwepo!Mahusiano mazuri na matamu ni yale ya kila mmoja kujitahidi kumfanyia mazuri mwenzie sio kutaka kufanyiwa mazuri na mwenzio!Kila mmoja atake na ajitahidi kila mara kumfurahisha mwenzie sio kutafuta furaha yake binafsi!.Big up sister,nitafute nikupe zawadi!
Kuishi na mwanaume asie na kazi shida sana,kwanza huwa hawajiamini,akiomba pesa huna unamnyanyasa,ukimpa unahongwa!
Kwa sababu yuko nyumbani tu kama kitasa mlangoni basi anaji keep busy kwa kuku track,kutwa uko wapi,mbona leo umechelewa,mbona siku hizi vikao vingi na manung'uniko yasokwisha!
Tafuta kazi bwana Mr Yes uwe busy hata kama kipato kitakuwa kidogo
 
Last edited by a moderator:
Mapenzi kweli kizungumkuti,yanayonikuta yanautesa sana moyo wangu.
KUna msichana ambaye ninampenda sana toka siku nyingi na yeye aanalijua hilo,ila kila nikimueleza juu ya hisia zangu uu yake yeye huishia kusema NAKUPENDA ILA HATUWEZI KUWA PAMOJA KWAKUWA HAUNA KAZI,HUNA PESA.

Hiki kitu kinaniumiza sana kwani kukosa kwangu kazi na kukosa pesa kunanifanya nimkose mtu ninayempenda kwa dhati,pia najiuliza hivi siku hizi ndio mapenzi hayawezakani tena mtu aspokuwa na pesa/kazi?ndugu mwana-jamvi,fikiria kama wewe ndio ungekuwa umepata na situation kama hii inayonikumba mimi ungefanyaje?(kumbuka hii ni very true story)
wallet_empty_SS.jpg
dont wory,,,1 day yes.............
 
Nenda kasome ule uzi wa wanawake ni wauzaji. Huyo anataka amuuzie k jamaa mwenye wallet nene.
 
Kuishi na mwanaume asie na kazi shida sana,kwanza huwa hawajiamini,akiomba pesa huna unamnyanyasa,ukimpa unahongwa!
Kwa sababu yuko nyumbani tu kama kitasa mlangoni basi anaji keep busy kwa kuku track,kutwa uko wapi,mbona leo umechelewa,mbona siku hizi vikao vingi na manung'uniko yasokwisha!
Tafuta kazi bwana Mr Yes uwe busy hata kama kipato kitakuwa kidogo

Kazi na hela ni vitu vya kupita,unaweza kuwa na kazi na hela tena mamilion leo lakini kesho ukawa hauna kazi na hata sh mia hauna,pia unaweza ukawa huna kazi na hela leo lakn kesho ukapata kazi na mamilion ya hela,ni masuala ya muda tu!Cha msingi ni kuvumiliana,leo hana kazi lakini kesho anaweza kupata,au wewe leo una kazi lakini kesho unaweza kupoteza hiyo kazi!
 
Last edited by a moderator:
Kwa huyo si utakua unanunua upendo bali utakua unanunua mchezo,maana she is not a wife material...mtoe kabsa katka mawazo yako
muda mwingine yahitaji kujitoa muhanga tu,upendo ukizidi kwa mtu mayokeo yake ndio haya
 
Kuishi na mwanaume asie na kazi shida sana,kwanza huwa hawajiamini,akiomba pesa huna unamnyanyasa,ukimpa unahongwa!
Kwa sababu yuko nyumbani tu kama kitasa mlangoni basi anaji keep busy kwa kuku track,kutwa uko wapi,mbona leo umechelewa,mbona siku hizi vikao vingi na manung'uniko yasokwisha!
Tafuta kazi bwana Mr Yes uwe busy hata kama kipato kitakuwa kidogo

nashukuru,na nimedhamiria kweli kuzisaka,na ninaamini nitazipata tu
 
Hakufai huyo tafuta anayeendana na wewe
Kusoma hujui hata kuangalia picha nako !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom