Nimekata tamaa. Sina kazi na sina rafiki

hupaswi kukata tamaa kwani si peke yako mwenye matatizo, wengine humu ukiona michango yetu unaweza dhania tuko peponi kumbe la hasha tuna matatizo lukuki na mengine ni makubwa kuliko ulinayo cha msingi ni kuwa na subira na kutokukata tamaa katika kutafuta kwa hakika mwenyezi mungu anajua zaidi.
 
Eeeh Mungu nisemehe bure sijui ni nini kimenileta kwenye huu uzi watu wanapitia mengi kwenye haya maisha

Nisamehe bure kwa kukufuru ama kwa kujua au kutokujua

Baraka naona umesoma wanayopitia watu humu sasa jipime kama kweli unapaswa kutoa uhai wako kwa unayoyapitia
 
Unaujuzi wako. Usijiue.

Kujiuwa si mutatuzi wa matatizo. Kuna watu wana masikio yao kamili lakini wana taabu kweli kweli na mwishowe hushukuru Mungu na kuchukulia kuwa hiyo ni "part of life". Hakuna mwanzo usio na mwisho, hakuna dhiki isiyo na faraja.

Yote hayo ni katika maisha tu.

Unaweza kupata rafiki mwishowe ukajuta kwanini nimepata rafiki wa aina hii.

Kama ni Muislam, hakikisha unakuwa na udhu na una sali sala tano na unavuta uradi na kama si Muislam basi nnakushauri ingia katika Uislam na ujifunze Uislam hutakosa marafiki wema.
 
Pole sana ila mbona miaka 23 bado yanki dogo una give up mapema sana kufanikiwa siyo lazima uwe na marafiki au mpenzi wakati mwingine hata wewe mwenyewe unaweza kutoka

Nikiwa na miaka 3 nilikimbiwa na mama
Nikiwa na miaka 8 nikafiwa na mzazi
Miaka 9 nikazamia dasilamu nikahaswa hata kujuta kuzaliwa
Nilianza la kwanza miaka 12 nikiwa dar nilikuwa na moyo wa kupenda shule

Form two nikasimamisha masomo nikiwa na miaka 21 nikakimbiwa na mpenzi kisa sikuwa na hela

Nikifanya biznec badae nikarudi shule form four nikapata div two ya 20
Nikaenda advance level HGE nikapata two Nikaenda chuo kwa mazobe mazobe nikahitimu

Nikakosa kazi nikafikilia umri unakwenda nikarudi kijijini nikafuga ng'ombe na mbuzi wakawa wengi nikauza jumla mil 16
Nikaja dar nikaanza biashara ya usafirishaji hayo tu

Don't give up if ur a man ukiziwi siyo sababu ya kukata tamaa
fundisho kubwa sana hilo. Kama MTU hawezi kijifunza kwa MTU aliyepitia magumu kuliko yeye atakuwa ana yake. Keep it up
 
Mkuu si kipindi hichi cha viongozi wenye misimamo mikali ukandamizaji mkuu kwa kipindi kile unaweza hila si miaka hii ya sasa
Ukianza kuwaza mambo kwa kutanguliza vizuizi hutafanya lolote duniani hapa. Maisha ni kuruka vikwazo,ondoa mentality ya kuangalia mambo kwa kutanguliza negativities .

Wewe unasema hapa serikali ni kikwazo, lakini sehemu kubwa ya nchi kama Somalia hakuna serikali wala guarantee ya kitu chochote kuanzia maisha mpaka uhai wa biashara yoyote lakini watu wana Biashara zinazohitaji mitaji mikubwa kama Banks, hoteli Makampuni ya Bima na zingine nyingi tu wakati unaweza kupigwa risasi muda wote ukikutwa umekiuka vitu vidogo sana au hata kwa bahati mbaya bila kukusudiwa, jengo kulipuliwa, mfanyakazi kutekwa nyara n.k Labda hizo ni biashara kubwa, sasa umejiuliza wasafirishaji wanaopeleka mchele,ngano,sukari,viungo,vifaa vya ujenzi n.k walikuwa na sababu gani ya kufanya biashara katika mazingira kama hayo wakati wana kila sababu na visingizio vya kukaa chini na kuachana na uhangaikaji?

Ukitaka kutafuta vikwazo, kila mahali kuna vikwazo vya kila aina, hapa utasema serikali, Sahara ya magharibi watakwambia ukame na ukosefu wa mvua, Congo Drc watakwambia mvua zipo na mito inatiririsha maji ila mapigano yanawafanya wasilime, Somalia watakwambia Serikali, vita na ukame, Sudan ya Kusini watakwambia ukame,ardhi isiyo na rutuba na vikundi vya waasi. Kwa hiyo kama ukilenga katika vikwazo, utakuwa unaviona vingi tu lakini haina maana kuwa haviwezi kuvukwa au kukwepeka na ndio maana, hukohuko kuliko na mazingira mabovu, wapo mamilionea na watu wanaolalamikia hali pia huwa ni aina ileile, watafutaji wa vikwazo. Na kwa nchi unazoona kuwa zina kila fursa na mazingira mazuri, masikini pia wapo. Ingekuwa mafanikio yanapatikana bila bidii kubwa na kujitolea, kila mtu angekuwa Dangote. Lakini ukiangalia alikotoka Dangote, walikuwepo watu pia waliokuwa wakipuuza fursa ndogo alizoziona yeye Dangote wakisubiria fursa za maana na leo hii bado wanaendelea kulalama tu wakisubiri fursa.

Jifunze kujibadili na mazingira kwa kukomazwa na hali na kujiimprovise na mabadiliko. Haya nayokwambia hata kama hutayaelewa sasa, kuna siku utaelewa. Hakujawahi kutokea mazingira rafiki kwa kila mtu kufanikiwa, mitaa ingejaa benzi na anga lingefungwa na wingu la helikopta maana kila mmoja angekuwa tajiri mkubwa jambo ambalo ni ndoto.
 
Usijione kama uko peke yako Aisee usione watu wanacheka ukadhani mambo safi.... badili mtazamo wako usimuonee aibu mtu otherwise utashindwa kutimiza malengo yako kwa kuhofia wengine watakuonaje
 
Baraka the current Poleee kaka Na mshukuru Mungu kwa kila jambo Maana kesho yako ni yeye tu aijuaye Kaka nimeacha kusikia Vizuri tangu nikiwa darasa la pili Nimesoma kwa shida sana wakati mwingine unapata adhabu kisa tu hujasikia darasani nimefika mpaka advance tena nimesoma science CBG Kwa changamoto hizihizi ulizo nazo Wewe Mpk Chuo!! Ulishawahi kufika shule ya msingi UHURU pale kunawatoto hawaoni Afu ni viziwi na Bado wanatabasamu tu!!! Mungu anakusudio nawewe
Nitafute 0769199375/0672723147 tuzungumze ndugu yangu!!!
 
Back
Top Bottom