Nimekata tamaa. Sina kazi na sina rafiki

Kijana Jr

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
838
Umri wangu miaka 23, Elimu yangu Form IV na Elimu ya Ufundi wa Umeme Level Two. Changamoto yangu mimi ni deaf (Kiziwi) ila nina uwezo wa kuongea na kumfundisha mtu akaelewa vizuri. Nilishawai kufundisha katika Chuo kimoja cha Ufundi somo la Theory Level One, niliacha kutokana na chuo hicho kufungiwa na VETA kwa kutosajiliwa.

Nimepitia machungu mengi sana, nakumbuka nilishawahi kukataliwa shule kwa sababu nitawapa tabu walimu katika ufundishaji sababu I am deaf pia walimu hawafahamu sign language. Pia na mimi sifahamu haya matatizo yalinikuta kipindi na miaka 17.

Wakuu na wanajukwaa wote, nimekaa nyumbani nikiwa nimekosa raha kabisaa. Nimeumia na kuumia sana, sina furaha tena katika maisha yangu ndoto zangu zakuja kuwapigania watu wenye matatizo ya ulemavu zimezima kabisa na Serikali hii ya Mama Ndalichako tena natamani kuchana hata Cheti changu chenye sahihi yakE.

Sina rafiki, sina mpenzi, sina kazi wakuu. Nipo siliasi. nipo njiani kunywa sumu wadau hapa nimejitaidi sana kuandika but ukweli bora kifo kuliko mateso
 
Tuliza akili Mkuu, kuna mamilioni ya watu wanatamani kuwa kama wewe.

Kuna watu wamelazwa wodini kwa zaidi ya miaka mitatu, lakini hawajawahi kufikiria kujiua,

Achana na mazoea ya kufikiri juu ya kujiua,

Jichunguze kwa makini utagundua kuna mengi unayoweza kuyafanya yatakayo kufurahisha.

Maisha ni kama siku, yana saa za mwanga na za giza pia.

Kuwa mvumilivu unapokabiliana na kila hali.

Miaka 23? you are too strong to die.
 
Pole sana ila mbona miaka 23 bado yanki dogo una give up mapema sana kufanikiwa siyo lazima uwe na marafiki au mpenzi wakati mwingine hata wewe mwenyewe unaweza kutoka

Nikiwa na miaka 3 nilikimbiwa na mama
Nikiwa na miaka 8 nikafiwa na mzazi
Miaka 9 nikazamia dasilamu nikahaswa hata kujuta kuzaliwa
Nilianza la kwanza miaka 12 nikiwa dar nilikuwa na moyo wa kupenda shule

Form two nikasimamisha masomo nikiwa na miaka 21 nikakimbiwa na mpenzi kisa sikuwa na hela

Nikifanya biznec badae nikarudi shule form four nikapata div two ya 20
Nikaenda advance level HGE nikapata two Nikaenda chuo kwa mazobe mazobe nikahitimu

Nikakosa kazi nikafikilia umri unakwenda nikarudi kijijini nikafuga ng'ombe na mbuzi wakawa wengi nikauza jumla mil 16
Nikaja dar nikaanza biashara ya usafirishaji hayo tu

Don't give up if ur a man ukiziwi siyo sababu ya kukata tamaa
 
Bado una umri mdogo sana achana na mawazo ya kishetani mdogoangu! furahia maisha na mshkuru mungu kwa kukupa viungo vyako vyote hilo tatizo lako ni la wastani sana kulinganisha na matatzo ya wengine! jichanganye na watu utumie taaluma yako achana na habari zs kutaka ajira na kama unataka kuendelea na masomo shule za wenye tatizo kama lako zipo ila vuta subira hali itulie kwanza, huu ni upepo tu unapita hali itajakua shwari usjali.
 
kwa umri wako bado kuna mambo mazuri sana mbele yako hujajua tu, trust me my friend. naomba uje pm tungee vizur. hayo ni mambo ya kawaida,kila binadam unayemwona anapitia changamoto zake ambazo zinamuumiza kichwa , unaweza mwona mtu anafedha nyingi na anapata kila anachoitaji ila anashindwa kufaidi hizo fedha kutokana na afya yake kuwa dhaif kila baada ya wiki miaka nenda rudi. kwa kifupi kila mtu ana msalaba ila ufumbuzi sio kujiua balu nj kuangalia plan B. usilazimishe kile ulichosomea kikutoe kimaisha.
 
Oy man ebu acha utani. Unatak kujiua kweli ? Ungekuw kama mimi sjui km ungekuwepo mpk Leo. Myb ungeshaga jiua siku nyingi. Mfikirie mtu ambaye ni mlemavu wa miguu hawez kupig ata hatua moja. Ao marafik na mpenz nawasikia tu kweny redio. Life langu lote ni ndani tu rafik yangu ni baba, mama na mitandao ya kijamii. Somtymz inapt ata wiki walokuwa marafik enz izo kbl sjaumwa hawafik kbs kuniona wala kunikumbuk kwa simu. Alaf Niko na umri km wew lkn sjawah ona sababu ya kujiua bdo. Ingaw kesho yang siijui
 
Oy man ebu acha utani. Unatak kujiua kweli ? Ungekuw kama mimi sjui km ungekuwepo mpk Leo. Myb ungeshaga jiua siku nyingi. Mfikirie mtu ambaye ni mlemavu wa miguu hawez kupig ata hatua moja. Ao marafik na mpenz nawasikia tu kweny redio. Life langu lote ni ndani tu rafik yangu ni baba, mama na mitandao ya kijamii. Somtymz inapt ata wiki walokuwa marafik enz izo kbl sjaumwa hawafik kbs kuniona wala kunikumbuk kwa simu. Alaf Niko na umri km wew lkn sjawah ona sababu ya kujiua bdo. Ingaw kesho yang siijui
dah very sad.pole sana mkuu.ugua pole.ulipata ajali ama
 
Back
Top Bottom