Nimejivua Gamba Rasmi

Nimejivua Gamba Rasmi

Usingeichoma, ungewarudishia uchafu wao wahangaike wenyewe mahali pa kupeleka hilo kadi lao la kijani, hongera mkuu na karibu kwenye mapambano!!!!!!!!!

ahsante nshakaribia ndugu
 
Hongera sana kijana, wanaokuponda hawajui tabu wanazopata ndugu zetu huko vijijini. Mimi nimefanya sana kazi vijijini, nilichokiona ukilinganisha na hawa mafisadi wanavyotoa majibu rahisi kwa maswali magumu ya hatma ya Tanzania unaweza kulia. Mimi namkaribisha kila mtu mwenye nia ya kuikomboa nchi yangu, haijalishi ametoka wapi.
Kazi yetu sisi underground ni kuhamasisha elimu ya uraia ili 2015 ukombozi upatikane kwelikweli, tusisubili DR slaa kuitisha mkutano, mabadiliko yaanzie nyumbani kwetu, mimi nimefanikiwa kumbadilisha mama yangu na mke wangu, nina imani hata mtoto wangu atakuwa cdm siku akikua!!!! Mungu ibariki Tanzania.

pamoja sana mkuu
 
Asante kaka yangu mi nilichukua miaka mitatu iliyopita makao makuu kinondoni nitafute nikutumie vocha ya kukupongeza kwa uhamuzi wako makini
 
Naomba kuuliza...
Wewe origin yako ni Moshi or Arusha?

huyu nadhani ni wa mbozi...kwa mheshimiwa mbunge silinde!
kama nimekosea sana basi atakuwa wa mpanda kule kwa mheshimiwa arfi!
 
Karibu sana hujachelewa coz wakati wa mabadiliko ni sasa. Uamuzi mzuri na wengine humu magamba msifikirie mara mbili fanya uamuzi wako maopema!
 
nimetafakari sana juu ya hiki Chama nimeona mimi kama kijana ndio natakiwa niwe kiini cha mabadikiko katika nchi yangu. Nimeamua nijivue gamba rasmi. Na sasa naingia rasmi CDM.
Dunia yangu chaguo langu.


Mkuu, yaani miaka yote hiyo madudu yanaonekana dhahiri lkn we unakuja kuona leo?! una kichwa kigumu kiasi gani? mbona madudu ya magamba hayahitaji elimu ya kidato chochote kuyabaini? akili timamu tu inatosha, ila wewe hadi ulupofika chuo ndo unyaona, ni kituko. Ila nitakusamehe iwapo nitajuwa umri wako, ur age please.
 
Back
Top Bottom