Nimejivua Gamba Rasmi

Usingeichoma, ungewarudishia uchafu wao wahangaike wenyewe mahali pa kupeleka hilo kadi lao la kijani, hongera mkuu na karibu kwenye mapambano!!!!!!!!!
 
nimetafakari sana juu ya hiki Chama nimeona mimi kama kijana ndio natakiwa niwe kiini cha mabadikiko katika nchi yangu. Nimeamua nijivue gamba rasmi. Na sasa naingia rasmi CDM.
Dunia yangu chaguo langu.

Sijui kama unatania au uko serious.
Ila ninachojua ni kwamba hiyo picha inaonekana mitandaoni
kwa zaidi ya mwaka sasa.
 
.
Acha ujinga wewe! ... kwanza haiitwi speaker! ... hiyo inaitwa microphone au kwa kiswahili fasaha inaitwa mikrofoni.
Speaker ni hizi hapa
url


Mikrofoni ni hii hapa chini

url



Kusoma hujui ... hata picha huioni!
.


Halafu mwambie akulipe na ada kabisa mkuu kwa darasa ulilompa!
 
Mkuu kadi ya CDM utaichukulia wapi? Nasikia Ole Millya na Mawazo wanaandaliwa karamu kubwa na watakabidhiwa kadi kijijini kwao (Millya). Nawe wapi mkuu?

Mie ninazo kadi na kitabu cha kuorodhesha wanachama wapya. Anitafute tu nitamworodhesha. Mpenda mabadiliko hahitaji sherehe kukabidhiwa kadi.
 
Nampongeza huyo Kijana kwa uamuzi wake wa busara mimi nawashauri wote wenye nia ya mabadiliko ya haki hakuna pa kwenda pengine zaidi ya CDM wakati ni huu.


kipugala
 
nimetafakari sana juu ya hiki Chama nimeona mimi kama kijana ndio natakiwa niwe kiini cha mabadikiko katika nchi yangu. Nimeamua nijivue gamba rasmi. Na sasa naingia rasmi CDM.
Dunia yangu chaguo langu.

Pole sana kwa kuvumilia kukaa ndani ya CCM kwa muda wote huo.Hongera pia japo umetuchelewesha lkn karibu tupambane.Binafsi si mwanachama wa chama chochote lkn namshangaa sana kijana anayeshabikia CCM hadi muda huu na hasa kwa wale vijana waliobahatika kusoma au wanaoishi mijini kwani nao wanataarifa nyingi za nini kinaendelea nchi hii.
 
nimetafakari sana juu ya hiki Chama nimeona mimi kama kijana ndio natakiwa niwe kiini cha mabadikiko katika nchi yangu. Nimeamua nijivue gamba rasmi. Na sasa naingia rasmi CDM.
Dunia yangu chaguo langu.


Ahsante ingawa umechelewa kidogo, eneza ujumbe(butua uwakomboe wenzio waliobaki).
 
Naona hapo umechemka kidogoo. Wenzio hawachomi, wanakabidhi kwa chama unachoijiunga.
 
.

Acha ujinga wewe! ... kwanza haiitwi speaker! ... hiyo inaitwa microphone au kwa kiswahili fasaha inaitwa mikrofoni.




Speaker ni hizi hapa

url




Mikrofoni ni hii hapa chini

url



Kusoma hujui ... hata picha huioni!


.


Hapo lazima umdai tuition fee, hakuna elimu ya bure!!!!!!!
 
Ama kweli kuna watu wana akili za peke yao duniani,hata huko bungeni wabunge wa CCM wameanza kutokuwa na imani na serikali ya chama chao.Wanajenga hoja kali na nzito..humu Jamvini bado wapo wanaoisifia CCM na kuitetea,haya Rejao na wenzako endeleeni kuamsha maiti,huenda akaamka
 
Mkuu hongera umesahau ukaonyesha mikono tu lakini haidhuru yatosha kuonyesha kadi ikiungua VIVA!!!!
 
Wenye Jeneza naona ni CUF ila hata wao sasa hivi wako ICU na jeneza lao litakuwa kubwa kuliko walilobeba halafu litafunikwa na shuka iliyoandikwa Arabic
 
Hongera sana kijana, wanaokuponda hawajui tabu wanazopata ndugu zetu huko vijijini. Mimi nimefanya sana kazi vijijini, nilichokiona ukilinganisha na hawa mafisadi wanavyotoa majibu rahisi kwa maswali magumu ya hatma ya Tanzania unaweza kulia. Mimi namkaribisha kila mtu mwenye nia ya kuikomboa nchi yangu, haijalishi ametoka wapi.
Kazi yetu sisi underground ni kuhamasisha elimu ya uraia ili 2015 ukombozi upatikane kwelikweli, tusisubili DR slaa kuitisha mkutano, mabadiliko yaanzie nyumbani kwetu, mimi nimefanikiwa kumbadilisha mama yangu na mke wangu, nina imani hata mtoto wangu atakuwa cdm siku akikua!!!! Mungu ibariki Tanzania.
 
Hongera, lakini kuhama chama kimoja kwenda kingine haimaanishi kuwa mpigania haki. Kinachotakiwa ni utashi na nia ya kweli toka moyoni mwako.
 
Back
Top Bottom