VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Niko ndani ya mkoa wa Kagera kwa siku tatu sasa. Nimekuwa katika tafiti 'fit' za kikampeni. Nimefuatilia pia mikutano yote ya kampeni ya mgombea wetu wa Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli Nimeingia na 'site' mbalimbali hapa Kagera. Wana-Kagera nimewakubali. Wamenidhihirishia kuwa wao wamesoma kwelikweli, yaani, 'ishomile'. Mioyoni mwao wamepanga hili, hadharani wanaonesha lile.
Wamechukua tahadhari baada ya mikwara ya kutopata maendeleo endapo hawatawachagua wagombea wa CCM uchaguzini. wameamua kuwa 'wasanii' kwa muda ili wamuoneshe Dkt. Magufuli kuwa wako naye; wanampenda; wanamuunga mkono na wanamwamini. Ndani ya mioyo yao, mambo ni tofauti. Na watu hutema nyongo zao sirini. Katika harakati zetu za kiintelijensia ya kisiasa, tumeongea na wananchi wengi.
Wana-Kagera bado wana maumivu juu ya kilichotokea wakati wa tetemeko la ardhi na madhila waliyoyapata. Kubwa zaidi, ni namna suala hilo lilivyoshughulikiwa. Rambirambi zikayeyuka; makazi wakaachiwa wenyewe wayatengeneze; majeruhi wakajitibu kwa tabu wenyewe na kadhalika. Bado, maneno makali ya Dkt. Magufuli kwa wahanga wa tetemeko yanaendelea kuchoma na kufukuta ndani ya mioyo yao. Wamepanga kuonesha tarehe 28 Oktoba kwenye sanduku la kura.
Uwepo wangu hapa Kagera umenionesha mengi yaliyofichwa na Wana-Kagera tayari kutolewa kupitia sanduku la kura Oktoba 28. 'Ishomile' hawa wa Kagera wametudokeza kwa kutuuliza: inakuwaje Mpambanaji wa rushwa kama Dkt. Magufuli 'akatae kustaafu' kwa Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa kwenye kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya Escrow? wana-Kagera wamejilinda kwa kutoonesha hasira zao kwa mgombea wetu. Lakini, watautuma ujumbe siku ya kura.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)