Dkt. Tulia aitetemesha Mbeya. Atua kijeshi na ndege ya Jeshi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,264
9,715
Ndugu zangu watanzania,

Haijapata kutokea ,haijapata kuonekana kwa mapokezi makubwa aliyoyapata mh Dkt Tulia Acksoni Mwansasu mbunge wa Mbeya mjini,speaker wa Bunge na Rais wa umoja wa mabunge Duniani ni mapokezi ya kishindo,ni mapokezi ya karne,ni mapokezi ya kihistoria ni mapokezi yaliyovunja rekodi,ni mapokezi yaliyoitetemesha na kulisimamisha Jiji la mbeya.watu wamehudhuria haijapata kutokea,mafuriko ya watu wamemiminika haijapata kuonekana.

Kwa hakika Dr Tulia ni mpango wa Mungu mwenyewe,anapendwa na kuheshimika na wanambeya ni haijapata kutokea ,anakubalika na kuungwa mkono ni haijapata kushuhudiwa ,itachukuwa miaka mingi sana kwa kiongozi yeyote yule kupata mapokezi aliyoyapata leo hii Dr Tulia.mtoto wa Mbeya kapokelewa kishujaa Mithili ya wanajeshi waliotoka vitani na kurejea na ushindi wa kukomboa ardhi ya nchi na Taifa lao iliyokuwa imeporwa.

Kapokelewa na watu wa rika zote na makundi yote kuanzia viongozi wa dini, serikali,mila,vijana,akina mama,wazee n.k.kishindo chake kimeteka jiji la Mbeya, kwa hakika ujio wake tokea angani aliko kuwa akiingia na ndege ya jeshi kumefanya jiji lote kulipuka kwa shangwe, nderemo na vifijo ambayo haijawahi kutokea.

Rai yangu kwa upinzani na mtu yeyote yule asithubutu kuchukua Fomu ya ubunge kugombea ubunge jimbo la Mbeya mjini maana kwa hali iliyopo kwa sasa na kwa namna Dkt. Tulia anavyopendwa na kukubalika kwa hakika itakuwa ni kupoteza muda na fedha kushindana na Rais wa IPU Dkt. Tulia Acksoni mwansasu katika sanduku la kura.

Dr Tulia siyo mtu wa kawaida ,ana nguvu fulani ndani yake isiyo ya kawaida na ya ajabu sana yenye kuonyesha uwepo wa Mungu ndani yake hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Dr Tulia ni mcha Mungu mkubwa na mwenye kumtegemea na kumtumainia Mungu kwa kila jambo.upepo wa Dr Tulia ni mkali na wenye mvumo wa kipekee sana,ni mtu mwenye ushawishi wa hali ya juu sana. Kwa hakika kaiteka mioyo ya wana Mbeya na kutembea mioyoni mwao.

Ni faraja kwa wana Mbeya ni fahari kwa wana nyanda za juu kusini na ni Nembo kwa wana mbeya. ameuheshimisha mkoa ,amelipa hadhi jiji,amewafanya wana Mbeya watembee kifua mbele na kwa kujiamini .na kila mtu anaona anastahili kuringa na kujivunia Dr Tulia kwa kuwa ni Mbeya ndio iliyompeleka Bungeni Dr Tulia na ni Mbeya ndio iliyotoa Rais wa umoja wa mabunge Duniani kati ya nchi zaidi ya 180 wanachama wa IPU Duniani kwote.

ndio maana wana Mbeya wamefanya mapokezi ya kishindo na ya heshima kubwa sana kumpatia mtoto wao na dada yao na mbunge wao Dkt Tulia Acksoni mwansasu kwa ushindi na heshima ya kipekee aliyolipatia jiji la Mbeya.kila mmoja anajiona kuwa kupitia kura yake ya ndio kwa Dkt Tulia Taifa limepata heshima ya kutoa Rais wa IPU na mwanamke wa kwanza kutoka Barani Afrika kushinda na kushika urais wa IPU.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Mbeya imepata mtumishi wa kweli wa watu! Mbeya imepata mleta maendeleo! Mbeya imepata mtetezi wa wote! Dr. Tulia ni kiongozi mwakilishi wa kweli wa wanambeya.

Tulia ni nyota inayoangaza kutoka anga za Mbeya. Nilikuwa naongea na wachungaji na machifu wa Mbeya wanamwombea Dr. Tulia afya njema na ulinzi dhidi ya watu wenye Nia mbaya na wanambeya.
 
Kama kawaida namba yako huwezi kuisahau kila unapopost. Ila mkeka mpya unakuja Mara hii lazima utakumbukwa tu
Mimi sitafuti kukumbukwa.kazi yangu ni kuwapeni ukweli na kuwahabarisheni tu juu ya mambo mbalimbali yanayojiri nchini mwetu.
 
Baada ya kupokelewa hivyo kuna shida zilizotatuliwa...??
Utatuzi wa Kero na changamoto jijini Mbeya umekuwa ni utaratibu wa kila siku tangia Dr Tulia alipochaguliwa kuwa mbunge wa Mbeya mjini.ndio Maana wana Mbeya wanaendelea kumuunga mkono mh Dkt Tulia kila siku na kumpa ushirikiano wa kutosha.
 
Mimi sitafuti kukumbukwa.kazi yangu ni kuwapeni ukweli na kuwahabarisheni tu juu ya mambo mbalimbali yanayojiri nchini mwetu.
Wana Mbeya sio waoumbavu labda huyo kijana msaka uteuzi akikuwepo peke yake......Tulia ni upouzi mtupu..
.analia lia jimbo.ligawanywe maana ni aubu saanaà
 
Bila kusomba wanafunzi wa shule mbali mbali mkutano usingekuwa na watu.

Mwambieni huyu dada Mbeya ni mji usiokuwa na miundombinu kabisa.

Hakuna mpango wa ujenzi wa mji.
Mitaa haipitiki.

Mji unategemea bara bara moja tangu uhuru.

Watakapoanza kuijenga kazi zitakuwa hazifanyiki.
 
Ya Mwabukusi hujasimulia mkuu huko Mbeya 😎
Habari za Mwabukusi hakuna mwana Mbeya mwenye habari nazo wala hata kumfuatilia .ndio maana hata alipoitisha maandamano na yule mhuni na mvuta bangi Mdude Nyagali hakuna aliyewaunga mkono na wao wenyewe walikimbia mbio ndefu kwenda kujificha vichakani huko.
 
Wana Mbeya sio waoumbavu labda huyo kijana msaka uteuzi akikuwepo peke yake......Tulia ni upouzi mtupu..
.analia lia jimbo.ligawanywe maana ni aubu saanaà
Dr Tulia ni moto wa kuotea mbali,.hakuna mwenye uwezo wala ubavu wa kuweza kupambana naye katika sanduku la kura.kwa sasa hata mkoa mzima wa Mbeya ukiwa ni jimbo moja la uchaguzi na Dr Tulia akigombea atapita na kushinda kwa kishindo kikubwa sana.
 
Habari za Mwabukusi hakuna mwana Mbeya mwenye habari nazo wala hata kumfuatilia .ndio maana hata alipoitisha maandamano na yule mhuni na mvuta bangi Mdude Nyagali hakuna aliyewaunga mkono na wao wenyewe walikimbia mbio ndefu kwenda kujificha vichakani huko.
🤣🤣🤣
Upumbavu ni jambo baya sana, unafikia kujitoa ufahamu kiasi hiki. Aibu sana...
 
Bila kusomba wanafunzi wa shule mbali mbali mkutano usingekuwa na watu.

Mwambieni huyu dada mbeya ni mji usiokuwa na miundombinu kabisa...
Naona unajitekenya na kujichekesha mwenyewe tu kama kichaa tu. Maana unaongea vitu vya uongo uongo tu .eti wanafunzi walisomewa.hivi upo sawa kweli kichwani mwako? Walisombwa kutoka shule ipi?
 
Back
Top Bottom