Nimejiridhisha: Wana-Kagera ni 'nshomile' kweli. Waliyoyaamua dhidi ya Dkt. Magufuli mioyoni mwao ni mazito!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Niko ndani ya mkoa wa Kagera kwa siku tatu sasa. Nimekuwa katika tafiti 'fit' za kikampeni. Nimefuatilia pia mikutano yote ya kampeni ya mgombea wetu wa Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli Nimeingia na 'site' mbalimbali hapa Kagera. Wana-Kagera nimewakubali. Wamenidhihirishia kuwa wao wamesoma kwelikweli, yaani, 'ishomile'. Mioyoni mwao wamepanga hili, hadharani wanaonesha lile.

Wamechukua tahadhari baada ya mikwara ya kutopata maendeleo endapo hawatawachagua wagombea wa CCM uchaguzini. wameamua kuwa 'wasanii' kwa muda ili wamuoneshe Dkt. Magufuli kuwa wako naye; wanampenda; wanamuunga mkono na wanamwamini. Ndani ya mioyo yao, mambo ni tofauti. Na watu hutema nyongo zao sirini. Katika harakati zetu za kiintelijensia ya kisiasa, tumeongea na wananchi wengi.

Wana-Kagera bado wana maumivu juu ya kilichotokea wakati wa tetemeko la ardhi na madhila waliyoyapata. Kubwa zaidi, ni namna suala hilo lilivyoshughulikiwa. Rambirambi zikayeyuka; makazi wakaachiwa wenyewe wayatengeneze; majeruhi wakajitibu kwa tabu wenyewe na kadhalika. Bado, maneno makali ya Dkt. Magufuli kwa wahanga wa tetemeko yanaendelea kuchoma na kufukuta ndani ya mioyo yao. Wamepanga kuonesha tarehe 28 Oktoba kwenye sanduku la kura.

Uwepo wangu hapa Kagera umenionesha mengi yaliyofichwa na Wana-Kagera tayari kutolewa kupitia sanduku la kura Oktoba 28. 'Ishomile' hawa wa Kagera wametudokeza kwa kutuuliza: inakuwaje Mpambanaji wa rushwa kama Dkt. Magufuli 'akatae kustaafu' kwa Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa kwenye kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya Escrow? wana-Kagera wamejilinda kwa kutoonesha hasira zao kwa mgombea wetu. Lakini, watautuma ujumbe siku ya kura.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)

 
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
Acha uongo ,ww mzee.Tupe statistics umeongea na watu wangapi?Ili taarifa zako ziwe significant. Au JF ni kijiwe cha uongo tu.
 
Magufuli anaponzwa na uwezo wake mdogo wa kuelewa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hivyo kumfanya adeal na petty issues ndo maana akadhani kumuahidi cheo Prof Tiba ndo yaweza kuwa njia ya kupata kura kagera. Lakini pia uwezo wake mdogo ndo unamfanya aamini kuwa maendeleo yanapelekwa sehemu na rais na CCM yake. Shame on him.
 
Katibu mkuu wa CCM nilimuokota kemondo alikuwa anauza ndizi, process ana amestahafu Ila kwangu mimi ajihesabu hajastahafu serikalini Kuna nafasi nyingi sana siwezi kukubali profesa mzima Tena Dada yangu hastahafu, Masilingi aliyekuwa mbunge wenu kabla ya profesa nilimteua kuwa balozi Marekani.

Kuna huyu alikuwa diwani wenu muleba anaitwa milanga alikuwa upinzani akaamia CCM Sasa hivi nimemteuwa kuwa katibu wa CCM uko kigoma. Alafu kuna graduate na akili zake timamu anasema Magufuli mitano Tena. Yani Kuna watu sijui ubongo wao una virus basi tu.
 
Nami nimefuatilia nimegundua kuwa kuna nyumbu bado wana changishwa fedha hali ya kuwa wenyewe hata mlo mmoja ni wa kubabaisha na bado wana matumaini yakuchukua nchi kwa kupitia michango yao.
 
Porojo tu hizo, zimeandikwa tangu mfumo wa vyama vingi kuingia.Mwaka 1995 Benjamini Mkapa alikataliwa na wananchi wakati akinadiwa na Hayati baba wa Taifa Mwl. Nyerere pale Morogoro wananchi walimkataa hadharani, lakini mwisho wa matokea Mkapa aliibuka mshindi. Unayoyasema hayatamfanya JPM ashindwe kurudi ikulu, ushindi wake ni 85-95% huo ndiyo ukweli mchungu kwa upinzani
 
Maccm wenye akili na wanaojipenda hawawezi kufanya ujinga huu eti magufuli awe rais? wamejifunza kwamba huyu si mtu na si mwenzao ndo maana anawakubali wapinzani zaidi ya wanaccm wenyewe,vyeo vyote kagawa kwa kina mollel,Tumbiri etc
Hata kwenye mabango ya huyu mzee , jina lake limepewa sehemu kubwa kuliko hata jina la chama

Unakuta Maandishi makuuuuuubwa

CHAGUA MEKOOOO

Halafu tuandishi tudogoooo

chagua ccm

Ni kama vile yeye ni mkubwa kuliko Chama
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom