Nimejiridhisha: Wana-Kagera ni 'nshomile' kweli. Waliyoyaamua dhidi ya Dkt. Magufuli mioyoni mwao ni mazito!

Niko ndani ya mkoa wa Kagera kwa siku tatu sasa. Nimekuwa katika tafiti 'fit' za kikampeni. Nimefuatilia pia mikutano yote ya kampeni ya mgombea wetu wa Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli Nimeingia na 'site' mbalimbali hapa Kagera. Wana-Kagera nimewakubali. Wamenidhihirishia kuwa wao wamesoma kwelikweli, yaani, 'ishomile'. Mioyoni mwao wamepanga hili, hadharani wanaonesha lile.

Wamechukua tahadhari baada ya mikwara ya kutopata maendeleo endapo hawatawachagua wagombea wa CCM uchaguzini. wameamua kuwa 'wasanii' kwa muda ili wamuoneshe Dkt. Magufuli kuwa wako naye; wanampenda; wanamuunga mkono na wanamwamini. Ndani ya mioyo yao, mambo ni tofauti. Na watu hutema nyongo zao sirini. Katika harakati zetu za kiintelijensia ya kisiasa, tumeongea na wananchi wengi.

Wana-Kagera bado wana maumivu juu ya kilichotokea wakati wa tetemeko la ardhi na madhila waliyoyapata. Kubwa zaidi, ni namna suala hilo lilivyoshughulikiwa. Rambirambi zikayeyuka; makazi wakaachiwa wenyewe wayatengeneze; majeruhi wakajitibu kwa tabu wenyewe na kadhalika. Bado, maneno makali ya Dkt. Magufuli kwa wahanga wa tetemeko yanaendelea kuchoma na kufukuta ndani ya mioyo yao. Wamepanga kuonesha tarehe 28 Oktoba kwenye sanduku la kura.

Uwepo wangu hapa Kagera umenionesha mengi yaliyofichwa na Wana-Kagera tayari kutolewa kupitia sanduku la kura Oktoba 28. 'Ishomile' hawa wa Kagera wametudokeza kwa kutuuliza: inakuwaje Mpambanaji wa rushwa kama Dkt. Magufuli 'akatae kustaafu' kwa Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa kwenye kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya Escrow? wana-Kagera wamejilinda kwa kutoonesha hasira zao kwa mgombea wetu. Lakini, watautuma ujumbe siku ya kura.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)
Ila mzee kwa umri wako tunaomba utushauri
Hivi 2025 ni nani ataweza kurithi viatu vya Dr?
Watanzania wengi wana hofu ya kuja kuletewa wapiga dili tena.
Waliohamia CCM watarudi tena kwenye chama cha Mbowe
 
Ukimsikiliza Tundu Lissu anaongea zaidi kwa huzuni kuliko hasira sio kama anavyofanya mpinzani wake meko.

Tundu Lissu anaendelea KUSEMA Watanzania wamepoteza maisha yao na kazi zao:kutokana na rais ambaye hasemeleki hataki kukosolewa, analaumu wengine, anakataa ushirikiano na mpenda chuki.
Sawa tatizo lipo kwenye michango ndugu.
 
Magufuli ajirekebishe kwa kweli mtaani watu hawamtaki kabisa hali imekuwa mbaya mbaya kupita Maelezo biashara hazitoki kabisa
 
Ccm hatuogopi The Hague, isitoshe hawawezi kutukamata kama hatutoki nje ya nchi yetu.

Mwaka huu fisiemu watakunywa damu za pipo lakini hakuna atakayewajibishwa.
Laurent Gbagbo hakutoka nje ya Ivory Coast..wajuba wakaenda kumtoa Ikulu kavaa pajama na mkewe..ogopa mabeberu wakiamua yao...
 
Hizi propaganda zenu zinawapa faraja ya muda tu.
October 28 sio mbali subirini muone kichapo ndani ya BOKSI
 
Magufuli hawezi kushinda urais hata kwa nyumba kumi tuu kwa wapiga kura wenye Afya njema ya Akili.
Ndio maana Kikwete alipo kuwa anaondoka alisema "Naondoka mie mtanikumbuka " Alijua mgombea wao ni Garasa tupu.
😆😆😆😆
 
Katibu mkuu wa CCM nilimuokota kemondo alikuwa anauza ndizi, process ana amestahafu Ila kwangu mimi ajihesabu hajastahafu serikalini Kuna nafasi nyingi sana siwezi kukubali profesa mzima Tena Dada yangu hastahafu, Masilingi aliyekuwa mbunge wenu kabla ya profesa nilimteua kuwa balozi Marekani.

Kuna huyu alikuwa diwani wenu muleba anaitwa milanga alikuwa upinzani akaamia CCM Sasa hivi nimemteuwa kuwa katibu wa CCM uko kigoma. Alafu kuna graduate na akili zake timamu anasema Magufuli mitano Tena. Yani Kuna watu sijui ubongo wao una virus basi tu.
Kubali kutokubaliana mkuu, usilazimishe kile unachoona kinafaa kwako kiwe sawa kwa mwingine. JPM mitano tena, "naweza kuwa graduate au zaidi"!
 
Magufuli hawezi kushinda urais hata kwa nyumba kumi tuu kwa wapiga kura wenye Afya njema ya Akili.
Ndio maana Kikwete alipo kuwa anaondoka alisema "Naondoka mie mtanikumbuka " Alijua mgombea wao ni Garasa tupu.
Ukimsikiliza Tundu Lissu anaongea zaidi kwa huzuni kuliko hasira sio kama anavyofanya mpinzani wake meko.

Tundu Lissu anaendelea KUSEMA Watanzania wamepoteza maisha yao na kazi zao:kutokana na rais ambaye hasemeleki hataki kukosolewa, analaumu wengine, anakataa ushirikiano na mpenda chuki.
 
Niko ndani ya mkoa wa Kagera kwa siku tatu sasa. Nimekuwa katika tafiti 'fit' za kikampeni. Nimefuatilia pia mikutano yote ya kampeni ya mgombea wetu wa Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli Nimeingia na 'site' mbalimbali hapa Kagera. Wana-Kagera nimewakubali. Wamenidhihirishia kuwa wao wamesoma kwelikweli, yaani, 'ishomile'. Mioyoni mwao wamepanga hili, hadharani wanaonesha lile.

Wamechukua tahadhari baada ya mikwara ya kutopata maendeleo endapo hawatawachagua wagombea wa CCM uchaguzini. wameamua kuwa 'wasanii' kwa muda ili wamuoneshe Dkt. Magufuli kuwa wako naye; wanampenda; wanamuunga mkono na wanamwamini. Ndani ya mioyo yao, mambo ni tofauti. Na watu hutema nyongo zao sirini. Katika harakati zetu za kiintelijensia ya kisiasa, tumeongea na wananchi wengi.

Wana-Kagera bado wana maumivu juu ya kilichotokea wakati wa tetemeko la ardhi na madhila waliyoyapata. Kubwa zaidi, ni namna suala hilo lilivyoshughulikiwa. Rambirambi zikayeyuka; makazi wakaachiwa wenyewe wayatengeneze; majeruhi wakajitibu kwa tabu wenyewe na kadhalika. Bado, maneno makali ya Dkt. Magufuli kwa wahanga wa tetemeko yanaendelea kuchoma na kufukuta ndani ya mioyo yao. Wamepanga kuonesha tarehe 28 Oktoba kwenye sanduku la kura.

Uwepo wangu hapa Kagera umenionesha mengi yaliyofichwa na Wana-Kagera tayari kutolewa kupitia sanduku la kura Oktoba 28. 'Ishomile' hawa wa Kagera wametudokeza kwa kutuuliza: inakuwaje Mpambanaji wa rushwa kama Dkt. Magufuli 'akatae kustaafu' kwa Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa kwenye kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya Escrow? wana-Kagera wamejilinda kwa kutoonesha hasira zao kwa mgombea wetu. Lakini, watautuma ujumbe siku ya kura.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)
Tunashukuru , Hadithi njoo, uongo ukole
 
Hata kwenye mabango ya huyu mzee , jina lake limepewa sehemu kubwa kuliko hata jina la chama

Unakuta Maandishi makuuuuuubwa

CHAGUA MEKOOOO

Halafu tuandishi tudogoooo

chagua ccm

Ni kama vile yeye ni mkubwa kuliko Chama
Afadhali kama wameanza hata kuweka tumaandishi tudogo 2015 ilikuwa Chagua MEKOO full stop.
Utendaji wa Meko umeifufua saaana CCM, kiasi leo hata wanaovaa nguo za CCM wanaheshimika mitaani tofauti na enzi zileeee.
 
K
Porojo tu hizo, zimeandikwa tangu mfumo wa vyama vingi kuingia.Mwaka 1995 Benjamini Mkapa alikataliwa na wananchi wakati akinadiwa na Hayati baba wa Taifa Mwl. Nyerere pale Morogoro wananchi walimkataa hadharani, lakini mwisho wa matokea Mkapa aliibuka mshindi. Unayoyasema hayatamfanya JPM ashindwe kurudi ikulu, ushindi wake ni 85-95% huo ndiyo ukweli mchungu kwa upinzani
KAMA ZA WIZI SAWA
 
Hivi Tupatupa ni mzee au ni kijana?

Huko kwenye chama una cheo gani?

Halafu mbona unatoa Siri za chama kwamba mnafanya inteligensia ya siasa?
 
Unahadaa watu tuu! Uanajua tafiti wewe? Hapo sijaona vielelezo vyovyote vya kitafiti zaidi ya siasa kavu kavu tuu
 
Niko ndani ya mkoa wa Kagera kwa siku tatu sasa. Nimekuwa katika tafiti 'fit' za kikampeni. Nimefuatilia pia mikutano yote ya kampeni ya mgombea wetu wa Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli Nimeingia na 'site' mbalimbali hapa Kagera. Wana-Kagera nimewakubali. Wamenidhihirishia kuwa wao wamesoma kwelikweli, yaani, 'ishomile'. Mioyoni mwao wamepanga hili, hadharani wanaonesha lile.

Wamechukua tahadhari baada ya mikwara ya kutopata maendeleo endapo hawatawachagua wagombea wa CCM uchaguzini. wameamua kuwa 'wasanii' kwa muda ili wamuoneshe Dkt. Magufuli kuwa wako naye; wanampenda; wanamuunga mkono na wanamwamini. Ndani ya mioyo yao, mambo ni tofauti. Na watu hutema nyongo zao sirini. Katika harakati zetu za kiintelijensia ya kisiasa, tumeongea na wananchi wengi.

Wana-Kagera bado wana maumivu juu ya kilichotokea wakati wa tetemeko la ardhi na madhila waliyoyapata. Kubwa zaidi, ni namna suala hilo lilivyoshughulikiwa. Rambirambi zikayeyuka; makazi wakaachiwa wenyewe wayatengeneze; majeruhi wakajitibu kwa tabu wenyewe na kadhalika. Bado, maneno makali ya Dkt. Magufuli kwa wahanga wa tetemeko yanaendelea kuchoma na kufukuta ndani ya mioyo yao. Wamepanga kuonesha tarehe 28 Oktoba kwenye sanduku la kura.

Uwepo wangu hapa Kagera umenionesha mengi yaliyofichwa na Wana-Kagera tayari kutolewa kupitia sanduku la kura Oktoba 28. 'Ishomile' hawa wa Kagera wametudokeza kwa kutuuliza: inakuwaje Mpambanaji wa rushwa kama Dkt. Magufuli 'akatae kustaafu' kwa Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa kwenye kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya Escrow? wana-Kagera wamejilinda kwa kutoonesha hasira zao kwa mgombea wetu. Lakini, watautuma ujumbe siku ya kura.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)

Usituletee porojo zako za kijinga - unaleta habari za kuchonga tu hapa - kitu cha kwanza wewe si mzaliwa wa Kagera hata Kihaya ukijui, eti "wana Kagera ni ishomile" - ishomile maanake nini, hakuna neno kama hilo kwenye lugha ya Kihaya.

Umeleta taarifa hizi za ki-Lucifer ukiwa na lengo la kutaka kichonganisha Wahaya na JPM - FYI Wahaya hawana tatizo na Dr.Magufuli uliona mwenyewe mapokezi aliyo pewa alipo wasali Mkoani Kagera - mwenye macho .... tazama, nani ambaye hajui hujuma zenu za chini chini za vyama vya upinzani, mnatoka zenu kasikasini kwenye ngome ya upizani mnafunga safari kufatilia fatalia mikutano ya Kampeini za JPM na kujaribu kuleta labsha zenu za kipumbavu na uchonganishi - wana Kagera wanajua michango ya tetemeko la aridhi zilitumika vipi katika kutuletea maendeleo ya kweli Mkoani na yanaonekana dhahili. Punguzeni ngojera zenu.
 
Back
Top Bottom