Nimejeruhi Vibaya Mhudumu wa Bar

Nimejeruhi Vibaya Mhudumu wa Bar

RaiaMbishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Posts
252
Reaction score
134
Ndugu zanguni,
nimekumbwa na kituko kibaya mjini arusha. Nilienda na ndugu yangu Bar jana, tukaagiza chakula. Tulikuwa tumeshakunywa konyagi kidogo. mhudumu kuleta chakula, akatuacha kwa kama dakika tano bila kutuletea maji ya kunawa. Nikaumuita na mazungumzo yakawa kama ifuatavyo:

Mimi: Oyaa mhudumu, mbona haujaleta maji, vipi?

Mhudumu: Oh, sikuleta kwa sababu nilidhani nyote wawili mnatumia NYUMA.

Mimi: Eti nini (huku nikiamka, na nikampiga kichwa kibaya sana, mhudumu chini, damu toka puani eneo lote lile). Baadae nikaeleweshwa kwamba alikuwa ana maana forks ambayo wingi wake ni Nyuma, ikiwa moja, ni umma.

Ndugu zanguni, hapa tatizo ni konyagi? au kutoelewana lugha?
 
Kutojua Kiswahili kama ilivyo kwa kutojua sheria si utetezi. Wewe Kisongo inakuhusu!
 
The home of great thinkers. Teh teh teh.
 
tabia zako kama jina lako
kumpiga mtu mzima wamfunza nn?
unasubiriwa na mfawidhi wa arusha hakimu magessa ukalale kisongo ndio ujue ubaya wa kupiga watoto wa wenzio
 
kenge akiwa na njaa anaweza akameza hata mkia wake.
 
nahisi unahasira za karibu sana ila si utetezi think twice
 
Kama angesema:
"Nilidhani nyote wawili mnatumia MBELE ungemfanya nini?
JF is never bored [Source: The Boss]
 
Kama angesema:
"Nilidhani nyote wawili mnatumia MBELE ungemfanya nini?
JF is never bored [Source: The Boss]

Hiyo ni tofauti, hapa naongelea chakula kimeletwa, lakini maji hayaletwi, huku ukweli ukiwa wazi kwamba alileta umma na kisu kwa sote. Sisi hatukujua kama wingi wa umma wa kulia chakula ni nyuma.
 
matatizo ni mbele, mkia na kichwa.
Ungekuwa huna kichwa una shingo tu usingeweza kumrukia kizinadini zidani.
 
una hakika hujawahi kuvuta bange maishani mwako? Kumbuka vizuri..
 
Baa gani Mkuu?
Ndugu zanguni,
nimekumbwa na kituko kibaya mjini arusha. Nilienda na ndugu yangu Bar jana, tukaagiza chakula. Tulikuwa tumeshakunywa konyagi kidogo. mhudumu kuleta chakula, akatuacha kwa kama dakika tano bila kutuletea maji ya kunawa. Nikaumuita na mazungumzo yakawa kama ifuatavyo:

Mimi: Oyaa mhudumu, mbona haujaleta maji, vipi?

Mhudumu: Oh, sikuleta kwa sababu nilidhani nyote wawili mnatumia NYUMA.

Mimi: Eti nini (huku nikiamka, na nikampiga kichwa kibaya sana, mhudumu chini, damu toka puani eneo lote lile). Baadae nikaeleweshwa kwamba alikuwa ana maana forks ambayo wingi wake ni Nyuma, ikiwa moja, ni umma.

Ndugu zanguni, hapa tatizo ni konyagi? au kutoelewana lugha?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom