Nimeingiziwa laki nane kimakosa nimeirudisha kwa mwenyewe

Kama sikosei waliwahi kutueleza kuwa ukitumiwa Fedha kimakosa...

Kausha mhusika anatakiwa kuripot kwenye mtandao husika.Baada ya hapo wao watawajibika kuurudisha ama kuusitisha.

Japo umefanya jambo lenye mashiko ila pindi shida ikijitokeza basi niliwahi kusikia kuwa Unaisaidia Polisi katika ushirikiana hasa katika mambo ya utakatishaji Mzigo...labda nilielewa vibaya.
 
Nilishwahi kufanya hivyo Japo kwangu iliingia laki 530,000

Baada ya kumrudishia yule mtu (alikua m'mama) alilia sana

kesho yake bila taarifa niliona nimewekewa 100,000 toka kwa namba ile ile

This time around nikasema huyu kazoea sasa,leo simrudishiii Nikanyamaza

Baadae nikapokea msg "Mwanangu chukua hiyo kama asante yangu kwako kwa wema wako"

Basi siku yangu ilikua bam bam sana kale kalaki nilinunulia kitu ambacho kila ataekiangalia pale kwangu

akikisifia nampa historia ya jinsi nilivyopata hela ya kununua kile kitu pale ukutani,anapata somo.
 
Katika huu mkanganyo wa NIDA kuna mtu kajichanganya kanitumia 805,000 jina lake ni Romano Mwakanosya nimekaa masaa matatu bila kutoa nikampigia nikamrudishia YOTE! Je wewe ungeweza?
Kisa kubwa sana umefanya.

Kuna siku yatakukuta ya kukukuta.

Mtu akikosea kukutumia hela yeye mwenyewe ndio inabidi apige simu kwa service provider ili irudishwe....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kabisa. 100%
Kama sikosei waliwahi kutueleza kuwa ukitumiwa Fedha kimakosa...

Kausha mhusika anatakiwa kuripot kwenye mtandao husika.Baada ya hapo wao watawajibika kuurudisha ama kuusitisha.

Japo umefanya jambo lenye mashiko ila pindi shida ikijitokeza basi niliwahi kusikia kuwa Unaisaidia Polisi katika ushirikiana hasa katika mambo ya utakatishaji Mzigo...labda nilielewa vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nyingine acha system yenyewe irudishe pesa, hii ya wewe kufanya transaction haijakaa vizuri, Unaweza kujikuta unapata kesi hapo

Ulichotakiwa kufanya ni kuhakikisha katika matumizi yako hugusi hiyo pesa, bw Romano kama alituma pesa kimakosa lazima angewasiliana na mtandao husika na wenye mtandao wangekuja Moja kwa moja kwa akaunti yako kuchukua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kabisa. 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
Yamewahi nikuta 1M ilikosewa kutoka kwa Mteja wa Vodacom..tena siku ya wajinga ile Tarehe 1 mwezi wa nne.Miaka Mitano iliyopita.

Niliitamani ile fedha ila niliiacha kama ilivyo....ilipofika saa tisa Mchana walianza Tigo kupiga simu then wakaja Vodacom.

Walinipa maelekezo mazuri sana juu ya ile fedha..na niliwajibu kuwa sihusiki naye mhusika aliyetuma pesa.Simtambui...japo nina wadeni wangu ila hakuwa sehemu ya yeye kunitumia kiasi hicho cha FEDHA.

Baaada ya maongezi ...ukaja ujumbe toka Tigo..then ulikuja mwingine toka Vodacom kama reference.Na jamaa baada ya kupata Fedha zake alinipigia kushukuru,alikuwa ni Mhindi.

Uzuri nili rekodi maelezo yote kama akiba mbeleni isije kuwa tatizo.

Ilikuwa strange sana maana awali kuna jembe lilinishauri twende kutoa ... :D :D :D
Sasa kufika kwa wakala nikampa simu mhusika aliyenishauri kuwa tutoe..
Akaonesha sms na jamaa kuwa hizi FEDHA zimezuiliwa..tena watu wa Heshima kabisa..

Ilibidi kuzuga kuwa kwanini jamaa ametufanyia hayo...:D:D:D:D kwanini azuie Fedha zetu tunazomdai...

Mana wakala alikomaa kuwa labda tuwapigie au tumpigie mdai wetu.

Hapo ndipo kujifunza kuwa ustaarabu na Hekima inahitajika.
 
Katika huu mkanganyo wa NIDA kuna mtu kajichanganya kanitumia 805,000 jina lake ni Romano Mwakanosya nimekaa masaa matatu bila kutoa nikampigia nikamrudishia YOTE! Je wewe ungeweza?
Huo ndiyo ustaarabu wetu ingawa kwa sasa wengi watakucheka na kukukejeli lakini ukweli unabaki pale pale.
 
Back
Top Bottom