Nimeibiwa simu yenye thamani ya Tshs laki 6

Pole sana
Hela ya kutrack ongezea laki 2 nunua simu yako ya laki 3 hadi 4 safi kabisa.
 
Wengi ya wanao kuambia achana nayo huenda ni wezi wenyewe wanaogopa utawakamata, Mimi mwaka Jana niliibiwa simu nikaenda kuriporti ,ikafanyiwa tracking,cha kushamgaza mwizi wangu alikuwa ni jirani yangu mwana mama,


Kama una IMEI ifuatilie utaipata.

Ushauri : jaribu kuwasiliana na polisi wa mbali na eneo ilipoibiwa simu ili kuepuka polisi kumkata mwizi wako na baadae wakamalizana kishua na wewe usipate simu yako,kama uko wilaya X wasiliana na polisi wa wilaya Y,utaipata simu bila shida,kikubwa hatua ya kwanza kariporti upate RB kwa kituo cha polisi karibu na wewe,usiwape details za simu
 
Nicheki nikuunganishe na jamaa yangu yeye ni pongo, atakutrakia kwa malipo kiduchu yamkini ukaipata..yuko smart sana kwenye hizo mambo
 
Pole sana. Mitaa ya wapi umeibiwa?
 
Pole sana mkuu, unaweza kuipata kama watakuzingatia hao police kinyume chake ni ngumu sana, ila jaribu kufuatilia na ukimjua ambae yupo kwenye kitengo hicho hapo ulipopeleka mashtaka yako nadhani ingekua vizuri zaidi.
 
Kuna Mganga kule Lushoto, Soni, mkoani Tanga, huyo mwizi atakutafuta ulipo mwenyewe. Gharama zake ni kuanzia f40 tu..Maadui wa Chadema watakusumbua tu, wakiipata watakuomba password kwa madai ya kutrack account yake online, inauzwa mapema sana. Labda kama una ndugu huko.
 
Pumbavu kabisa, nilichogundua kumbe hata polisi tunaowalaumu hawana vifaa vya kutrack, serikali haijawawezesha. Ni ujinga ujinga tu.
 
M
mkuu Ndengaso naomba code ya huyo mtaalam, Kuna mshenzi kanidhulumu pesa zangu hafu anatamba kbs!
 
niliwahi kushauri
kwa nini TCRA wasiwe wanazifungia simu zinazoibiwa
mmiliki awapatie imei namba na taarifa ya upotevu tokea polisi
Watajuaje ni kweli umeibiwa, maybe tuseme umegombana na mtu sasa kisa unajua imei za simu yake ukafanya kumkomoa kwa kushtaki kwa tcra kuwa simu yako imeibiwa?
Najua utaleta kisingizio cha line/namba ya simu ila hilo achana nalo, nipe sababu nyngn
 
Kuna jamaa yupo humu JF alileta story kuwa aliibiwa laptop maskani kwake Morogoro, akaelekezwa akavuka kwenda Kinole huko baada ya siku kadhaa jamaa aliyeiba alirejesha laptop yake vzr kbs na shughuli nzima ilimgharimu 40k+ nauli, yule mdau plz kama unaona huu uzi msaidie mwana plz!!
 
Are you sister as avatar look like
 
Kama ni iPhone unaipata. Kama ni Android hapo ni kazi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ