Nimehamia Njiro "Kwa Msolla"

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,893
31,101
Wakuu leo nimetimiza miezi miwili tangu nihamie Njiro kwa Msolla.Njiro ni sehemu ambayo imepangika (imepimwa)bila shaka hii ni sababu kubwa iliyonivutia kujenga hili kukwepa hadhaa ya msongamano kama maeneo ya Ungalimited,Kambi ya Fisi na Sombetini.

Leo pia nimetimiza miezi miwili kamili bila huduma ya maji AUWSA kila nikirejea nyumbani nalazimika kubeba maji ndani ya gari kwaajili ya matumizi ya nyumbani.Nimejaribu kuuliza majirani na marafiki kadhaa wote kilio ni maji Njiro ni sehemu nzuri sana lakini maji ni tatizo kubwa ambalo linahitaji jitihada madhubuti kukabilina nalo_Ongezeko la watu eneo la Njiro na Arusha kwaujumla haliendani kabisa na uwekezaji katika sekta ya maji.Mamlaka ya maji imekuwa imezidi kuwa hovyo tangu Mkurugenzi Mtendaji Eng Asili Munisi astaafu kazi kwa mujibu wa sheria.Chanzo kikuu cha maji mji wa Arusha ni mto Themi na mto Nduruma pamoja na visima virefu vichache sana bahati mbaya hakuna uwekezaji wa maana unaoendana na ongezeko la mahitaji.

AUWSSA Mamlaka ya maji jijini Arusha badala ya kuwekeza kwenye uchimbaji wa visima na mabwawa kwaajili ya kuhifadhi maji wakati wa mvua wameamua kujenga jengo refu kwaajili ya maofisi na kununua magari mapya [Mashangingi] kwaajili ya maofisa wake warasimu.

Naomba kuwasilisha.
 
Ngongo tatizo la maji kwa arusha halipo njiro peke yake, toka mwezi sept arusha kuna tatizo kubwa la maji. Mabomba yanatoa maji mara moja kwa mwezi au kwa miezi miwili.
 
Sweetlady,

Nimeishi Sanawari,Kaloleni sijawahi kukumbana na hali mbaya kiasi hiki.

Ngongo tatizo la maji kwa arusha halipo njiro peke yake, toka mwezi sept arusha kuna tatizo kubwa la maji. Mabomba yanatoa maji mara moja kwa mwezi au kwa miezi miwili.
 
Lowassa kachukua maji ngaramtoni kapeleka monduli watu wa ngaramtoni ndoo moja mia tano hawana maji
arusha huwa siwaelewi kabisa
 
Wakuu leo nimetimiza miezi miwili tangu nihamie Njiro kwa Msolla.Njiro ni sehemu ambayo imepangika (imepimwa)bila shaka hii ni sababu kubwa iliyonivutia kujenga hili kukwepa hadhaa ya msongamano kama maeneo ya Ungalimited,Kambi ya Fisi na Sombetini.

Leo pia nimetimiza miezi miwili kamili bila huduma ya maji AUWSA kila nikirejea nyumbani nalazimika kubeba maji ndani ya gari kwaajili ya matumizi ya nyumbani.Nimejaribu kuuliza majirani na marafiki kadhaa wote kilio ni maji Njiro ni sehemu nzuri sana lakini maji ni tatizo kubwa ambalo linahitaji jitihada madhubuti kukabilina nalo_Ongezeko la watu eneo la Njiro na Arusha kwaujumla haliendani kabisa na uwekezaji katika sekta ya maji.Mamlaka ya maji imekuwa imezidi kuwa hovyo tangu Mkurugenzi Mtendaji Eng Asili Munisi astaafu kazi kwa mujibu wa sheria.Chanzo kikuu cha maji mji wa Arusha ni mto Themi na mto Nduruma pamoja na visima virefu vichache sana bahati mbaya hakuna uwekezaji wa maana unaoendana na ongezeko la mahitaji.

AUWSSA Mamlaka ya maji jijini Arusha badala ya kuwekeza kwenye uchimbaji wa visima na mabwawa kwaajili ya kuhifadhi maji wakati wa mvua wameamua kujenga jengo refu kwaajili ya maofisi na kununua magari mapya [Mashangingi] kwaajili ya maofisa wake warasimu.

Naomba kuwasilisha.

Nikupongeze kwanza kwa kuwa na kwako tena Njiro bila shaka umetumia jasho halali kusimamisha mjengo.

Nikupe pole kwa kukosa huduma ya maji, sijui kama ulifanya tathmini ya kina kabla ya kuamua kujenga njiro, huenda ungegundua mapema kwamba kuna tatizo hilo na kujipanga namna ya kulikabili.

Hata hivyo bado una nafasi ya kuwasiliana na AUWSA ili kuhakikisha kwamba wanaweka mkakati maalum wa kuwawezesha kupata maji huko njiro.
Next time nikija arusha nitakuja kukusalimu, kama unatoa mialiko/makaribisho kwa wanaJF, hasa wale msiofungamana kiitikadi!
 
Na mto Themi umeanza kukauka!
Hata Sekei maji ni mpaka usiku ndiyo yanatoka tena kiduchu ile mbaya.
 
mkuu, chimba kisima, ndio njiro tunavyoishi..of course hata mm napoa mitaa hiyo hiyo nyuma ya radio 5.
Maji Njiro ni janga la kitaifa!
 
Mkuu MM.

Mkuu hata Sanawari ni kwangu pia Njiro ni nyumba yangu ya nne.Niliamua kuondoka Sanawari kwasababu Njiro nyumba ilimalizika miaka miwili iliyopita kazi ikawa kupata mpangaji wa stahili ya Njiro [angalizo nililenga wafanyakazi wa UNICTR] bahati mbaya UNICTR wanamaliza mikataba yao nikaona bora nijitose mwenyewe.Sanawari wapangaji wako wa kumwaga kabla sijahama tayari nilikuwa na msururu wa wapangaji.

Mkuu AUWSA wameajiri watumishi wa kukabiliana na malalamiko si kwaajili ya kutatua matatizo sina muda wa kuchezea na warasimu sana sana najipanga kuchimba kisima changu.

Makaribisho ni desturi na mila ya mtanzania unakaribishwa sana Arusha.

Nikupongeze kwanza kwa kuwa na kwako tena Njiro bila shaka umetumia jasho halali kusimamisha mjengo.

Nikupe pole kwa kukosa huduma ya maji, sijui kama ulifanya tathmini ya kina kabla ya kuamua kujenga njiro, huenda ungegundua mapema kwamba kuna tatizo hilo na kujipanga namna ya kulikabili.

Hata hivyo bado una nafasi ya kuwasiliana na AUWSA ili kuhakikisha kwamba wanaweka mkakati maalum wa kuwawezesha kupata maji huko njiro.
Next time nikija arusha nitakuja kukusalimu, kama unatoa mialiko/makaribisho kwa wanaJF, hasa wale msiofungamana kiitikadi!
 
Mkuu,
Hongera sana kwa hatua hiyo uliyofanya!

Hakika, Eneo la Njiro Kwa Msolla ni kati ya maeneo bora kabisa na ya kisasa, ukiacha shida ya maji!
Mnachoweza kufanya ni kuunganisha nguvu. Mtakapokuwa kama kundi ni rahisi kusikilizwa na mamlaka husika na kufanyiwa mpango wowote, kuliko kila mtu kufanya juhudi binafsi.
Off-records: Broda, Jumapili nilikuwa na shughuli ya mwanangu mtaani kwako hapo, ulikuwepo nini!...?...maaana niliona mtu 3 zinachatt kwenye simu non-stop, nikahisi hawa ni wanabodi!
 
Mkuu Mchaka Mchaka

Najipanga unajua kuchimba kisima unatakiwa utenge 12 - 18 Milioni.

mkuu, chimba kisima, ndio njiro tunavyoishi..of course hata mm napoa mitaa hiyo hiyo nyuma ya radio 5.
Maji Njiro ni janga la kitaifa!
 
Lowassa kachukua maji ngaramtoni kapeleka monduli watu wa ngaramtoni ndoo moja mia tano hawana maji
arusha huwa siwaelewi kabisa

Acha kupotosha watu maji ya monduli yana toka jeshini kwa gharama za lowasa .mto wa ngaramtoni ulisha kufa zamani maji yake ni madogo hata familia kumi hawawezi chota kwa pamoja ni kama mto temi ulivyo
 
Mkuu hapo kwa Msola si ni karibu sana na kwa Mheshimiwa Lema? Muulize inakuwaje?
 
huko kusiko na maji ni wapi?....au mi naishi Arusha ipi?....au idara ya maji wananipendelea mie tu....poleni sana wapenzi....
 
Hivi hayo maji ya Arusha si yale yanaoyharibu meno? Nimeuliza tu sina nia nyingine
 
Back
Top Bottom