Nimehamia Njiro "Kwa Msolla"

Nimehamia Njiro "Kwa Msolla"

Mkuu E Makofia,

Mkuu wangu bei ya kiwanja inategemea na Eneo,Ukubwa na Udongo.

Eneo la kiwanja kama liko barabara kuu bei ni kubwa kwasababu ni rahisi kwa biashara.Pia bei ya kiwanja inategemea kipo block gani mfano viwanja vya block A,B na C bei yake ni kubwa kwakuwa viwanja viko karibu na mjini ie Nane nane,IAA naTANESCO

Ukubwa wa kiwanja eg high density low density and medium.Low kwa kawaida bei yake ni kubwa 60 - 70 million.

Udongo mwekundu kwa kawaida bei yake ni kubwa kuliko udongo mweusi.Bei ya kiwanja medium kinachoweza kujengwa nyumba kubwa na nyumba ndogo ya mfanyakazi udongo mwekundu ni kati ya 30 - 40 milioni.Udongo mwekundu ni rahisi kujenga hakuna haja ya kuhamisha udongo.Udongo mweusi shughuli yake ni pevu lazima uhamishe udongo hence gharama za ujenzi zinakwenda juu sana.

Nadhani nimejitahidi kujibu maswali yako.

niliwahi kukwama mwaka juzi siku nzima nikahamia pale matongee kusuuza roho kwani nilichoka sana
bei ya viwanja imefika ngapi kuna changu hapo nimeweka fance nataka bei ikiwa juu niuze!
 
Ngongo, miezi miwili tu ya kukosa maji wapiga kelele! Unda urafiki na watu wa Idara ya maji ili upate upendeleo wa ration. Nilikaa miezi sita bila maji, walipokuja Idara ya maji kufuatilia bili nikawaambia wakate bomba ndo ikawa mwisho wa stori. Suluhu ni kuchimba kisima.
 
Mkuu Ibrah.

Niko kwenye mchakato unajua bei ya kuchimba kisima inakubidi ujipange kisawa sawa.

Mkuu,
Hongera sana kwa hatua hiyo uliyofanya!

Hakika, Eneo la Njiro Kwa Msolla ni kati ya maeneo bora kabisa na ya kisasa, ukiacha shida ya maji!
Mnachoweza kufanya ni kuunganisha nguvu. Mtakapokuwa kama kundi ni rahisi kusikilizwa na mamlaka husika na kufanyiwa mpango wowote, kuliko kila mtu kufanya juhudi binafsi.
Off-records: Broda, Jumapili nilikuwa na shughuli ya mwanangu mtaani kwako hapo, ulikuwepo nini!...?...maaana niliona mtu 3 zinachatt kwenye simu non-stop, nikahisi hawa ni wanabodi!

usisahau kumwalika shughuli ya tarehe 3 jmosi
 
Mkuu Ibrah.

Niko kwenye mchakato unajua bei ya kuchimba kisima inakubidi ujipange kisawa sawa.

Ngongo, meanwhile unakaribishwa Mrimba hardware kupata mahitaji ya maji, jamaa ndie kimbilio la wengi pale Kwa Msola, kwa siku anauza lita elfu 15 na bado yanamwishia.
 
Mkuu Ibrah,

Asante mkuu Mrimba napafahamu.Vipi Climax Resorts umeshafika kupata moja baridi moja moto pametulia isipokuwa bei ya vinywaji iko juu .

Ngongo, meanwhile unakaribishwa Mrimba hardware kupata mahitaji ya maji, jamaa ndie kimbilio la wengi pale Kwa Msola, kwa siku anauza lita elfu 15 na bado yanamwishia.
 
Hii sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 inakera sana. Sijui sheria mpya itatiwa lini saini na JK au kakimbilia tu ya mswada wa katiba kwa msukumo wa kisiasa?
Pole sana Ngungu kwa hilo
 
Mkuu Kikahe,

Ni kweli sheria ya manunuzi ina kera nadhani watungaji waliangalia upande mmoja wa shilingi kuzuia ufisadi.Halafu acha kuharibu jina langu unajua nilipewa na Babu mkuu mzaa Babu ahaaa aaaa.

Hii sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 inakera sana. Sijui sheria mpya itatiwa lini saini na JK au kakimbilia tu ya mswada wa katiba kwa msukumo wa kisiasa?
Pole sana Ngungu kwa hilo
 
Mh. Lema naye anaishi huko huko ebu check naye kama kunamkakati wowote wa kupunguza adha hiyo!
 
Wanajamvi,

Hatimae jana na leo maji tumepata maji simtank 5000 lts limejaa mapipa manne ya 500lts yamejaa nakwambia hadi raha nina maji ya kutosha mpaka mwaka mpya 2012.

Nimejiuliza mara mbili mbili kilio changu JF kilisaidia au AUWSA waliamua kutukomoa tu !.
 
Back
Top Bottom