Nimegundua udhaifu mkubwa sana wa Serikali ya Tanzania katika kukabili suala la COVID-19

Huyu kirusi alivyo na akili nyingi kama za kwako Hero, ataanza na wewe ili zikukae sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Infinix, wanaonitakiaga mabaya wote mwishowe huwa wananyoosha mikono kwa kujikuta nakumbana na mema badala ya mabaya! Kwangu corona virus alipita na akatoka nduki bila kuaga zaidi ya mwezi uliopita, maana alijuta kujipendekeza kwangu! Wasiwasi wangu ni kwako kama akikupitia utaweza ku'survive'! Maombi yangu hicho kirusi kisikusogelee ww na watanzania wengine wote ambao bado kuambukizwa! Na wale walioambukizwa wasiugue bali kirusi ndio kisalimu amri, na kwa wale waliougua, wapone haraka na tuendelee kulijenga taifa!
 
Kwakweli serikali ya Tanzania imelichukilia janga la COVID-19 kama jambo la mzaha kupita kiasi, hali hii imewafanya baadhi ya wananchi kubweteka kupita kiasi kutokana na janga hili.

Kwa haya niliyoshuhudia, nachelea kusema kuwa ikitokea COVID-19 ikaiathiri Tanzania kwa kiwango kikubwa basi mataifa mengine yataandika nne na kutucheka kwa kejeli. Haya yanasababishwa kwa kiwango chote na viongozi wetu wa serikali tuliowapa mamlaka ya kutuongoza. Nitaainisha uzembe huu uliopindukia katika maeneo machache.

1. Ni jambo la aibu sana baadhi ya raia wa Tanzania kuvuka mpaka wa Tanzania na Uganda na kisha kukamatwa ndani ya Uganda wakati kila nchi inalichukulia jambo hili kwa uzito wa aina yake labda isipokuwa Tanzania. Ni jambo la aibu kwa sisi kutumia uzembe wetu na kutokujua mambo kupeleka mzigo kwa wenzetu, kwa hili najisikia aibu sana kama Mtanzania.

Kwa jambo kama hili Uganda watatuona sisi kama watu wa mzaha sana kiasi kwamba mzaha wetu tunaupeleka hadi kwenye nchi za wenzetu ambazo kwa namna ya kipekee wamelichukulia jambo hili kwa umuhimu na ukubwa wa kiwango chake. Kwanini mamlaka za Tanzania mipakani hazikuwazuia watu hawa hadi wakavuka mpaka kati ya Uganda na Tanzania? Hawakuona umuhimu wa kuwaheshimu wenzetu walioamua kufunga mipaka yao ili kuikabili Corona kwa vitendo?

2. Hoteli zetu kutoza kiwango cha chini cha Tshs laki 2 kwa watakaojiweka karantini kwa siku moja pekee. Hili ni jambo la aibu sana kwetu kama nchi. Kwa wenzetu jambo hili limeihusisha jamii yote huku Rais wa nchi akiwa kamanda mkuu wa kikosi pambanaji. Hapa kwetu hakuna control yoyote juu ya jambo hili iliyoandaliwa hadi pale walipogutuka baada ya watu kulalamika.

Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa. Nimejiuliza, hata kwa hili hawakujiandaa? Yani mtu mwenye matatizo ambapo imembidi kuwekwa ama kujiweka pale ili kuwanusuru wengine anaenda kutozwa hela ya malazi ya anasa? What a shame! Mbaya zaidi kamanda mkuu yupo Dodoma anapiga picha akiwa amelala juu ya jiwe! Huu ni mzaha na kuwachukulia watu wako "Too low"

3. Utolewaji wa taarifa za mara kwa mara na kuwekeza nguvu kwenye vituo vya kupimia ugonjwa huu pamoja na kuwekeza nguvu kwenye kudhibiti usambaaji. Ni aibu kubwa kuwa Rais kasema kuwa anapeleka fedha za Mwenge kwenye kupambana na ugonjwa huu ila hakuna lolote kuhusu kupambana huko. Vituo vya usafiri wa umma, mahospitali mengi hakuna viosha mikono, hakuna kupulizia dawa.

Yani tupo kila mtu na lake. Mbaya zaidi hakuna taarifa za mara kwa mara kutoka kwa wahusika wa kutoa taarifa. Yani kwa kifupi ni kama serikali imelala kupita kiasi! Ni aibu eti sampuli zote ndani ya nchi zinapelekwa kituo kimoja pekee cha kupimia. Hatuoni kuwa tutakuwa tunachelewesha kuwabaini waathirika kwa haraka? Hatuoni madhara haya ya ucheleweshaji mpaka sasa?

4. Swala la mkuu wa mkoa wa Dar kutoka asubuhi asubuhi na kupeleka ujumbe kwa watu kuwa kuna mtoto wa Mbowe anaugua Corona. Ukiusoma uso wa Paul Makonda ni kama amepata "relief" fulani kwa mtoto wa Mbowe kuumwa ugonjwa tena kwake furaha zaidi ni Corona. Hakuna kiongozi hata mmoja aliyekosoa ujinga huu! Tunaanzaje kuwaamini kuwa mpo serious? Alichofanya Paul Makonda ni utoto mtupu na kwa alichofanya hakutakiwa kuendelea kuwa kiongozi. Lakini kwakuwa tayari kuna udhaifu, basi limeonekana ni jambo la kawaida kabisa kwa viongozi wa kitaifa wenye dhamana.

5. Hakuna uhamasishaji kwa watu wenye uwezo kujitoa ili jamii nzima iwe salama. Hili kimsingi linatakiwa kufanywa na serikali. Lakini kwakuwa hakuna kujali basi na wao wameamua kujikalia kimya tuu ili mradi liende huko litakakotua.

Mwisho naomba nieleze masikitiko yangu kuwa kwa hili jambo basi ni hatuna serikali makini. Pia ni heri watu wakajichukulia tahadhari wenyewe na pengine wanayoambiwa na serikali ya Tanzania basi wachanganye na zao! Hakuna uaminifu kwa kiwango kikubwa mno kutoka serikalini kuhusu janga hili la COVID-19.
Haya yalishasahaulika kwa sababu yalifanywa na mpendwa wetu... ndio unajiuliza hawa wanaopinga sasa kwanini hii mada hawakuitaka wakati ule?
 
Back
Top Bottom