Nimegundua udhaifu mkubwa sana wa Serikali ya Tanzania katika kukabili suala la COVID-19

Lawama kwa serikali…lawama kwa serikali…lawama kwa serikali!
Ni wajibu wa kila mtz kujikinga na ugonjwa huu na magonjwa mengine! Kama unasubiri serikali ije ikukinge baada ya kutoa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa huu nchini basi utasubiri sana! Kwa maoni yangu serikali inafanya kinachotakiwa. Imetoa elimu, imefunga shule na vyuo na kuzuia mikusanyiko! haya yanapaswa yapige kengere kwenye masikio ya kila mtz maana siyo mambo ya kawaida kutokea! Unapoona mpaka serikali imechukua hatua hizo ujue imechukulia covd-19 kwa uzito unaostahili!
Na tz kihihivi tutavuka salama na mataifa mengine yatashangaa, Mungu yupo!
Ok mbona viongozi hao hao ndio wanaovunja marufuku waliyoyaweka.Ina maana wametuhadaa sisi wananchi.Tutakapokusanyika tusione tukibughudhiwa kwa sababu nyie ndio mliovunja utaratibu.Kama kweli tupo makini na tunasimamia yaliyotolewa ya kutokukusanyika Makondakta amevunja amri hiyo na Mh.Mambo ni sasa amkamate mara moja bila kuchelewa tujue kweli mko serious na sio mnaigiza.
 
namba hazidanganyi! Africa is resistant to Corona virus ikiaminiwa kama si joto kubwa basi ni Melanin, waafrika wangapi wamekufa kwa Corona? wengi kati ya waafrica waliokufa kwa Corona walikuwa na magonjwa mengine makubwa na weak immune system Corona imewapiga teke tu, hatupaswi kupanic kama wazungu huu ugonjwa ni hatari sana na unatupata na tunausambaza ila si wa kusimamisha maisha yetu, yule mgonjwa wa kwanza bongo hakuambukiza mtu yoyote katika wote aliokutana nao tofauti na uzunguni huyu angeua mji mzima hivyo lockdown si lazima cha msingi ni kuwa na bajeti na timu maalum kuhakikisha inasimamia karantini kwa kila anaeingia bongo! wasio na uwezo wa hotel nashauri walipiwe na fedha ya umma because this is a public health problem si individual case na the fact is si kila msafiri anaeshuka bongo ana mawe sababu almost 90+ percent ya watu wako kwenye informal based economy! mtu anaetoka nje kabla hajapanda ndege anaweka bajeti ni ukweli kwa asie muajiriwa bajeti ya hotel ya wiki mbili za karantini hawezi kuwa nayo kwa hela za mawazo!! i speak from personal experience!

Corona virus is an invisible enemy who hits you severely but you cannot revenge or fight back!The global wealth that was created from sell of weapons, loan interests and low prices of goods from poor countries is going to be spent the same way it was created! nani kaelewa?

Ukifikiri sana utaona labda Corona ni adhabu toka juu sasa tujiulize wenzetu wa west walichomkosea muumba! je ni watu weupe kuwakandamiza kuwaibia na kuwabagua kuwanyanyasa na kuwadharau watu weusi ? je ni high interest loans to poor countries au kutupa low prices? au ni slave trade and colonialism? au ni kutuingilia mambo yetu? au ni ushoga, au ni kutengeneza silaha na kutuuzia watu weusi tuuane? au ni vita yao dhidi ya magaidi na uislam?

mi nawaza Corona si binadamu tu wanaisambaza hata wanyama wa nyumbani pets, upepo, birds, ambulances, majengo ya hospital , aircrafts na nguo za wahudumu wa afya wa Corona!!!sababu kuna wagonjwa wapya wa Corona walikaa zao home bila kuwa na contact na waathirika wala majengo yenye corona!!
Hata watu wa Ulaya walikuwa wakiwaambia wachina maneno kama haya!
 
6. Serikali ilitakiwa by now iwe imesema ina vitanda kiasi gani kukabiliana na mlipuko, imetoa oda za vitanda vya dharura kwa kiasi gani ? Ina madaktari na wauguzi kiasi gani on standby kusupport mlipuko na je wameandaa budget ?
PPE za wauguzi wa afya zimeandaliwa kiasi gani? Je tuna viwanda vitakavyoweza kuanza mara moja kutengeneza locally mahitaji muhimu kama sanitizor, mask, gloves au hata jirani on ventilators?
Je kuna mafunzo ya haraka kwa wauguzi wote wa afya kuhusu nini kitatokea in worst case scenario?
Hospitali na vituo vya afya sasa wamejiandaa kiasi gani katika mapokezi ya mgonjwa yeyote, shida ni kuwa mgonjwa wa corona anaweza enda hospital akiwa hajui na atajulikana baada ya vipimo na hapo ameshafanya interaction ya kutosha?
Kwa watakao kuwa na hali mbaya tuko na ventilators ngp? Na je kwa hatua ya dharura tumeweka order ya ventilators ngp?

Tusimuachie Mungu ajibu haya maswali maana ametupa bongo. Yajibiwe kwa vitendo na kisha tuombe Mungu.

Wasalaam
Kajima
 
Lengo la hii mada ni hapo namba 4 tu
Wenzio buku saba akili hamna, huwa hawasogei kabisa nyuzi aina hii. Sasa wewe KIHARUSI umejitoa ufahamu ukajitumbukiza. Hizo NONDO kali na ambazo ni ukweli mtupu, unataka tuzipuuze, tuangalie upuuzi wa Makonda.
Ok, kama hoja ya mleta uzi ni namba 4, wewe hoja yako ni ipi hasa?
 
Mkuu unasomeka. Ila kitu kimoja dhahiri hakuna jitihada ya mmoja mmoja kujikinga na Corona itafanikiwa. Huu siyo ukimwi.

Hivi sasa Rwanda wagonjwa tayari 33 Kenya 25.

Rwanda watu quarantined costs zote ziko catered for na serikali. Wanapewa pia free internet na free access to local phone calls.

Kenya quarantined gharama wanalipa nusu ya zile gharama za normal accommodation costs kwenye given hotels.

Kwetu wana hike? Yaani imekuwa fursa?

Kweli hii ni Tanzania tu.

Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa janga la ugonjwa huu halitumiki kama fursa kwa mtu yoyote, kwa serikali au mtu yeyote.

Kuna magumashi sana kwenye utoaji taarifa za ukubwa wa tatizo. Haijulikani ni kwa faida ipi wala faida ya nani.

Kuhusu ya kujiuliza na alivyo jinasibu mkuu katika janga hili yawezekana ni tatizo la washauri wake zaidi. Hawa kina Kabadi hawa. Hawa kina makondakta hawa

Ninaamini serikali inajua bila hatua za total lockdown huu ugonjwa hauwezi kabisa kudhibitika na wala hatuwezi kuwa na maendeleo yoyote. Ila kwa makusudi wameamua kutuweka rehani kwanza.

Ni vyema wakajua tutajua kwa nini wanajivuta vuta wakituweka wananchi wote hatarini.

Mwalimu ni muda mzuri tutajajua tu. Maana fumbo mfumbie mjinga and you cannot fool all the people all the time.
KORONA itaumulika na kuuanika wazi UOVU wa serikali ya Magufuli, na itatuweka huru. Magufuli tangu aingie madarakani ameonesha udhaifu mkubwa katika kushughulikia na kuongoza nchi wakati wa majanga. Kuanzia wakati wa tetemeko kule Bukoba, alipojificha sijui akihofia kitu gani, akaibuka aliposikia kuna mzigo wa kutosha wa rambirambi kwa waathirika, akasepa nao. Ameendelea kutonesha vituko mbalimbali kila linapotokea janga la kitaifa.

Kwa mafuriko ya mvua ya mwaka huu na hii KORONA, Magufuli atavuliwa nguo mbele ya watanzania
 
Nchi masikini kama Rwanda ilivyofanya lockdown so far umeshasikia wananchi wake wangapi wamekufa kwa kukosa chakula?

Au huko hua wanafanya kazi gani za kuwafanya wawe na saving ya wiki 2?

Mkuu kuna akili ndogo na kubwa zote kaumba maulana.

Ndogo ndogo haina haja ya kubishana nazo.

Ila lockdown kama alivyosema Ramaphosa haja. Tatizo ni lini. Ikija tukiwa tumechelewa mno athari zitakuwa kubwa zaidi.

Serikali pia wanajua hivyo kuna kitu tu wanaficha not sure yet -" what."
 
Wenzio buku saba akili hamna, huwa hawasogei kabisa nyuzi aina hii. Sasa wewe KIHARUSI umejitoa ufahamu ukajitumbukiza. Hizo NONDO kali na ambazo ni ukweli mtupu, unataka tuzipuuze, tuangalie upuuzi wa Makonda.
Ok, kama hoja ya mleta uzi ni namba 4, wewe hoja yako ni ipi hasa?

Mkuu, thubutu. Aipate wapi hiyo hoja?

Hawana lolote kelele kama mavuvuzela tu.

Akileta hiyo hoja nikuombe unistue.
 
Issue ya korona ni ya kisiasa mkuu, kwani huoni namna marekani anavyopambana na mshindani wake ?? wakitupiana mpira kuwa nani kauleta huu ugonjwa??

Hizi hoja za Facebook siyo huku mkuu.

Za hivi ni za kupuuzwa tu.
 
namba hazidanganyi! Africa is resistant to Corona virus ikiaminiwa kama si joto kubwa basi ni Melanin, waafrika wangapi wamekufa kwa Corona? wengi kati ya waafrica waliokufa kwa Corona walikuwa na magonjwa mengine makubwa na weak immune system Corona imewapiga teke tu, hatupaswi kupanic kama wazungu huu ugonjwa ni hatari sana na unatupata na tunausambaza ila si wa kusimamisha maisha yetu, yule mgonjwa wa kwanza bongo hakuambukiza mtu yoyote katika wote aliokutana nao tofauti na uzunguni huyu angeua mji mzima hivyo lockdown si lazima cha msingi ni kuwa na bajeti na timu maalum kuhakikisha inasimamia karantini kwa kila anaeingia bongo! wasio na uwezo wa hotel nashauri walipiwe na fedha ya umma because this is a public health problem si individual case na the fact is si kila msafiri anaeshuka bongo ana mawe sababu almost 90+ percent ya watu wako kwenye informal based economy! mtu anaetoka nje kabla hajapanda ndege anaweka bajeti ni ukweli kwa asie muajiriwa bajeti ya hotel ya wiki mbili za karantini hawezi kuwa nayo kwa hela za mawazo!! i speak from personal experience!

Corona virus is an invisible enemy who hits you severely but you cannot revenge or fight back!The global wealth that was created from sell of weapons, loan interests and low prices of goods from poor countries is going to be spent the same way it was created! nani kaelewa?

Ukifikiri sana utaona labda Corona ni adhabu toka juu sasa tujiulize wenzetu wa west walichomkosea muumba! je ni watu weupe kuwakandamiza kuwaibia na kuwabagua kuwanyanyasa na kuwadharau watu weusi ? je ni high interest loans to poor countries au kutupa low prices? au ni slave trade and colonialism? au ni kutuingilia mambo yetu? au ni ushoga, au ni kutengeneza silaha na kutuuzia watu weusi tuuane? au ni vita yao dhidi ya magaidi na uislam?

mi nawaza Corona si binadamu tu wanaisambaza hata wanyama wa nyumbani pets, upepo, birds, ambulances, majengo ya hospital , aircrafts na nguo za wahudumu wa afya wa Corona!!!sababu kuna wagonjwa wapya wa Corona walikaa zao home bila kuwa na contact na waathirika wala majengo yenye corona!!
Hivi unajua kuwa stress inapunguza immune system ya mwanadamu?
Au na Hilo wafrika haitupati

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikaitahadharisha nchi yangu ninayoipenda sana Tanzania
 
Corona will not affect tanzania...
Neither cause a big tragedy like other European countries..

Do u know why?

Africans have a lot of problems more than corona.
Would you write the same comment today ?
 
Lawama kwa serikali…lawama kwa serikali…lawama kwa serikali!
Ni wajibu wa kila mtz kujikinga na ugonjwa huu na magonjwa mengine! Kama unasubiri serikali ije ikukinge baada ya kutoa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa huu nchini basi utasubiri sana! Kwa maoni yangu serikali inafanya kinachotakiwa. Imetoa elimu, imefunga shule na vyuo na kuzuia mikusanyiko! haya yanapaswa yapige kengere kwenye masikio ya kila mtz maana siyo mambo ya kawaida kutokea! Unapoona mpaka serikali imechukua hatua hizo ujue imechukulia covd-19 kwa uzito unaostahili!
Na tz kihihivi tutavuka salama na mataifa mengine yatashangaa, Mungu yupo!
Huyu kirusi alivyo na akili nyingi kama za kwako Hero, ataanza na wewe ili zikukae sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli serikali ya Tanzania imelichukilia janga la COVID-19 kama jambo la mzaha kupita kiasi, hali hii imewafanya baadhi ya wananchi kubweteka kupita kiasi kutokana na janga hili.

Kwa haya niliyoshuhudia, nachelea kusema kuwa ikitokea COVID-19 ikaiathiri Tanzania kwa kiwango kikubwa basi mataifa mengine yataandika nne na kutucheka kwa kejeli. Haya yanasababishwa kwa kiwango chote na viongozi wetu wa serikali tuliowapa mamlaka ya kutuongoza. Nitaainisha uzembe huu uliopindukia katika maeneo machache.

1. Ni jambo la aibu sana baadhi ya raia wa Tanzania kuvuka mpaka wa Tanzania na Uganda na kisha kukamatwa ndani ya Uganda wakati kila nchi inalichukulia jambo hili kwa uzito wa aina yake labda isipokuwa Tanzania. Ni jambo la aibu kwa sisi kutumia uzembe wetu na kutokujua mambo kupeleka mzigo kwa wenzetu, kwa hili najisikia aibu sana kama Mtanzania.

Kwa jambo kama hili Uganda watatuona sisi kama watu wa mzaha sana kiasi kwamba mzaha wetu tunaupeleka hadi kwenye nchi za wenzetu ambazo kwa namna ya kipekee wamelichukulia jambo hili kwa umuhimu na ukubwa wa kiwango chake. Kwanini mamlaka za Tanzania mipakani hazikuwazuia watu hawa hadi wakavuka mpaka kati ya Uganda na Tanzania? Hawakuona umuhimu wa kuwaheshimu wenzetu walioamua kufunga mipaka yao ili kuikabili Corona kwa vitendo?

2. Hoteli zetu kutoza kiwango cha chini cha Tshs laki 2 kwa watakaojiweka karantini kwa siku moja pekee. Hili ni jambo la aibu sana kwetu kama nchi. Kwa wenzetu jambo hili limeihusisha jamii yote huku Rais wa nchi akiwa kamanda mkuu wa kikosi pambanaji. Hapa kwetu hakuna control yoyote juu ya jambo hili iliyoandaliwa hadi pale walipogutuka baada ya watu kulalamika.

Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa. Nimejiuliza, hata kwa hili hawakujiandaa? Yani mtu mwenye matatizo ambapo imembidi kuwekwa ama kujiweka pale ili kuwanusuru wengine anaenda kutozwa hela ya malazi ya anasa? What a shame! Mbaya zaidi kamanda mkuu yupo Dodoma anapiga picha akiwa amelala juu ya jiwe! Huu ni mzaha na kuwachukulia watu wako "Too low"

3. Utolewaji wa taarifa za mara kwa mara na kuwekeza nguvu kwenye vituo vya kupimia ugonjwa huu pamoja na kuwekeza nguvu kwenye kudhibiti usambaaji. Ni aibu kubwa kuwa Rais kasema kuwa anapeleka fedha za Mwenge kwenye kupambana na ugonjwa huu ila hakuna lolote kuhusu kupambana huko. Vituo vya usafiri wa umma, mahospitali mengi hakuna viosha mikono, hakuna kupulizia dawa.

Yani tupo kila mtu na lake. Mbaya zaidi hakuna taarifa za mara kwa mara kutoka kwa wahusika wa kutoa taarifa. Yani kwa kifupi ni kama serikali imelala kupita kiasi! Ni aibu eti sampuli zote ndani ya nchi zinapelekwa kituo kimoja pekee cha kupimia. Hatuoni kuwa tutakuwa tunachelewesha kuwabaini waathirika kwa haraka? Hatuoni madhara haya ya ucheleweshaji mpaka sasa?

4. Swala la mkuu wa mkoa wa Dar kutoka asubuhi asubuhi na kupeleka ujumbe kwa watu kuwa kuna mtoto wa Mbowe anaugua Corona. Ukiusoma uso wa Paul Makonda ni kama amepata "relief" fulani kwa mtoto wa Mbowe kuumwa ugonjwa tena kwake furaha zaidi ni Corona. Hakuna kiongozi hata mmoja aliyekosoa ujinga huu! Tunaanzaje kuwaamini kuwa mpo serious? Alichofanya Paul Makonda ni utoto mtupu na kwa alichofanya hakutakiwa kuendelea kuwa kiongozi. Lakini kwakuwa tayari kuna udhaifu, basi limeonekana ni jambo la kawaida kabisa kwa viongozi wa kitaifa wenye dhamana.

5. Hakuna uhamasishaji kwa watu wenye uwezo kujitoa ili jamii nzima iwe salama. Hili kimsingi linatakiwa kufanywa na serikali. Lakini kwakuwa hakuna kujali basi na wao wameamua kujikalia kimya tuu ili mradi liende huko litakakotua.

Mwisho naomba nieleze masikitiko yangu kuwa kwa hili jambo basi ni hatuna serikali makini. Pia ni heri watu wakajichukulia tahadhari wenyewe na pengine wanayoambiwa na serikali ya Tanzania basi wachanganye na zao! Hakuna uaminifu kwa kiwango kikubwa mno kutoka serikalini kuhusu janga hili la COVID-19.

Tatizo umeeongelea kiTanzania zaidi wakati jambo hili ni "Pandemic" hivyo unapotaka ku stop cycle yake ni lazima uzingatie neno PANDEMIC
 
Issue ya korona ni ya kisiasa mkuu, kwani huoni namna marekani anavyopambana na mshindani wake ?? wakitupiana mpira kuwa nani kauleta huu ugonjwa??

Bado corona ni ishue ya kisiasa ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom