Nimegundua udhaifu mkubwa sana wa Serikali ya Tanzania katika kukabili suala la COVID-19

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
9,585
2,000
Kwakweli serikali ya Tanzania imelichukilia janga la COVID-19 kama jambo la mzaha kupita kiasi, hali hii imewafanya baadhi ya wananchi kubweteka kupita kiasi kutokana na janga hili.

Kwa haya niliyoshuhudia, nachelea kusema kuwa ikitokea COVID-19 ikaiathiri Tanzania kwa kiwango kikubwa basi mataifa mengine yataandika nne na kutucheka kwa kejeli. Haya yanasababishwa kwa kiwango chote na viongozi wetu wa serikali tuliowapa mamlaka ya kutuongoza. Nitaainisha uzembe huu uliopindukia katika maeneo machache.

1. Ni jambo la aibu sana baadhi ya raia wa Tanzania kuvuka mpaka wa Tanzania na Uganda na kisha kukamatwa ndani ya Uganda wakati kila nchi inalichukulia jambo hili kwa uzito wa aina yake labda isipokuwa Tanzania. Ni jambo la aibu kwa sisi kutumia uzembe wetu na kutokujua mambo kupeleka mzigo kwa wenzetu, kwa hili najisikia aibu sana kama Mtanzania.

Kwa jambo kama hili Uganda watatuona sisi kama watu wa mzaha sana kiasi kwamba mzaha wetu tunaupeleka hadi kwenye nchi za wenzetu ambazo kwa namna ya kipekee wamelichukulia jambo hili kwa umuhimu na ukubwa wa kiwango chake. Kwanini mamlaka za Tanzania mipakani hazikuwazuia watu hawa hadi wakavuka mpaka kati ya Uganda na Tanzania? Hawakuona umuhimu wa kuwaheshimu wenzetu walioamua kufunga mipaka yao ili kuikabili Corona kwa vitendo?

2. Hoteli zetu kutoza kiwango cha chini cha Tshs laki 2 kwa watakaojiweka karantini kwa siku moja pekee. Hili ni jambo la aibu sana kwetu kama nchi. Kwa wenzetu jambo hili limeihusisha jamii yote huku Rais wa nchi akiwa kamanda mkuu wa kikosi pambanaji. Hapa kwetu hakuna control yoyote juu ya jambo hili iliyoandaliwa hadi pale walipogutuka baada ya watu kulalamika.

Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa. Nimejiuliza, hata kwa hili hawakujiandaa? Yani mtu mwenye matatizo ambapo imembidi kuwekwa ama kujiweka pale ili kuwanusuru wengine anaenda kutozwa hela ya malazi ya anasa? What a shame! Mbaya zaidi kamanda mkuu yupo Dodoma anapiga picha akiwa amelala juu ya jiwe! Huu ni mzaha na kuwachukulia watu wako "Too low"

3. Utolewaji wa taarifa za mara kwa mara na kuwekeza nguvu kwenye vituo vya kupimia ugonjwa huu pamoja na kuwekeza nguvu kwenye kudhibiti usambaaji. Ni aibu kubwa kuwa Rais kasema kuwa anapeleka fedha za Mwenge kwenye kupambana na ugonjwa huu ila hakuna lolote kuhusu kupambana huko. Vituo vya usafiri wa umma, mahospitali mengi hakuna viosha mikono, hakuna kupulizia dawa.

Yani tupo kila mtu na lake. Mbaya zaidi hakuna taarifa za mara kwa mara kutoka kwa wahusika wa kutoa taarifa. Yani kwa kifupi ni kama serikali imelala kupita kiasi! Ni aibu eti sampuli zote ndani ya nchi zinapelekwa kituo kimoja pekee cha kupimia. Hatuoni kuwa tutakuwa tunachelewesha kuwabaini waathirika kwa haraka? Hatuoni madhara haya ya ucheleweshaji mpaka sasa?

4. Swala la mkuu wa mkoa wa Dar kutoka asubuhi asubuhi na kupeleka ujumbe kwa watu kuwa kuna mtoto wa Mbowe anaugua Corona. Ukiusoma uso wa Paul Makonda ni kama amepata "relief" fulani kwa mtoto wa Mbowe kuumwa ugonjwa tena kwake furaha zaidi ni Corona. Hakuna kiongozi hata mmoja aliyekosoa ujinga huu! Tunaanzaje kuwaamini kuwa mpo serious? Alichofanya Paul Makonda ni utoto mtupu na kwa alichofanya hakutakiwa kuendelea kuwa kiongozi. Lakini kwakuwa tayari kuna udhaifu, basi limeonekana ni jambo la kawaida kabisa kwa viongozi wa kitaifa wenye dhamana.

5. Hakuna uhamasishaji kwa watu wenye uwezo kujitoa ili jamii nzima iwe salama. Hili kimsingi linatakiwa kufanywa na serikali. Lakini kwakuwa hakuna kujali basi na wao wameamua kujikalia kimya tuu ili mradi liende huko litakakotua.

Mwisho naomba nieleze masikitiko yangu kuwa kwa hili jambo basi ni hatuna serikali makini. Pia ni heri watu wakajichukulia tahadhari wenyewe na pengine wanayoambiwa na serikali ya Tanzania basi wachanganye na zao! Hakuna uaminifu kwa kiwango kikubwa mno kutoka serikalini kuhusu janga hili la COVID-19.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,187
2,000
Kwakweli serikali ya Tanzania imelichukilia janga la COVID-19 kama jambo la mzaha kupita kiasi, hali hii imewafanya baadhi ya wananchi kubweteka kupita kiasi kutokana na janga hili.

Kwa haya niliyoshuhudia, nachelea kusema kuwa ikitokea COVID-19 ikaiathiri Tanzania kwa kiwango kikubwa basi mataifa mengine yataandika nne na kutucheka kwa kejeli. Haya yanasababishwa kwa kiwango chote na viongozi wetu wa serikali tuliowapa mamlaka ya kutuongoza. Nitaainisha uzembe huu uliopindukia katika maeneo machache.

1. Ni jambo la aibu sana baadhi ya raia wa Tanzania kuvuka mpaka wa Tanzania na Uganda na kisha kukamatwa ndani ya Uganda wakati kila nchi inalichukulia jambo hili kwa uzito wa aina yake labda isipokuwa Tanzania. Ni jambo la aibu kwa sisi kutumia uzembe wetu na kutokujua mambo kupeleka mzigo kwa wenzetu, kwa hili najisikia aibu sana kama Mtanzania.

Kwa jambo kama hili Uganda watatuona sisi kama watu wa mzaha sana kiasi kwamba mzaha wetu tunaupeleka hadi kwenye nchi za wenzetu ambazo kwa namna ya kipekee wamelichukulia jambo hili kwa umuhimu na ukubwa wa kiwango chake. Kwanini mamlaka za Tanzania mipakani hazikuwazuia watu hawa hadi wakavuka mpaka kati ya Uganda na Tanzania? Hawakuona umuhimu wa kuwaheshimu wenzetu walioamua kufunga mipaka yao ili kuikabili Corona kwa vitendo?

2. Hoteli zetu kutoza kiwango cha chini cha Tshs laki 2 kwa watakaojiweka karantini kwa siku moja pekee. Hili ni jambo la aibu sana kwetu kama nchi. Kwa wenzetu jambo hili limeihusisha jamii yote huku Rais wa nchi akiwa kamanda mkuu wa kikosi pambanaji. Hapa kwetu hakuna control yoyote juu ya jambo hili iliyoandaliwa hadi pale walipogutuka baada ya watu kulalamika. Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa. Nimejiuliza, hata kwa hili hawakujiandaa? Yani mtu mwenye matatizo ambapo imembidi kuwekwa ama kujiweka pale ili kuwanusuru wengine anaenda kutozwa hela ya malazi ya anasa? What a shame! Mbaya zaidi kamanda mkuu yupo Dodoma anapiga picha akiwa amelala juu ya jiwe! Huu ni mzaha na kuwachukulia watu wako "Too low"

3. Utolewaji wa taarifa za mara kwa mara na kuwekeza nguvu kwenye vituo vya kupimia ugonjwa huu pamoja na kuwekeza nguvu kwenye kudhibiti usambaaji. Ni aibu kubwa kuwa Rais kasema kuwa anapeleka fedha za Mwenge kwenye kupambana na ugonjwa huu ila hakuna lolote kuhusu kupambana huko. Vituo vya usafiri wa umma, mahospitali mengi hakuna viosha mikono, hakuna kupulizia dawa. Yani tupo kila mtu na lake. Mbaya zaidi hakuna taarifa za mara kwa mara kutoka kwa wahusika wa kutoa taarifa. Yani kwa kifupi ni kama serikali imelala kupita kiasi! Ni aibu eti sampuli zote ndani ya nchi zinapelekwa kituo kimoja pekee cha kupimia. Hatuoni kuwa tutakuwa tunachelewesha kuwabaini waathirika kwa haraka? Hatuoni madhara haya ya ucheleweshaji mpaka sasa?

Mkuu unasomeka. Ila kitu kimoja dhahiri hakuna jitihada ya mmoja mmoja kujikinga na Corona itafanikiwa. Huu siyo ukimwi.

Hivi sasa Rwanda wagonjwa tayari 33 Kenya 25.

Rwanda watu quarantined costs zote ziko catered for na serikali. Wanapewa pia free internet na free access to local phone calls.

Kenya quarantined gharama wanalipa nusu ya zile gharama za normal accommodation costs kwenye given hotels.

Kwetu wana hike? Yaani imekuwa fursa?

Kweli hii ni Tanzania tu.

Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa janga la ugonjwa huu halitumiki kama fursa kwa mtu yoyote, kwa serikali au mtu yeyote.

Kuna magumashi sana kwenye utoaji taarifa za ukubwa wa tatizo. Haijulikani ni kwa faida ipi wala faida ya nani.

Kuhusu ya kujiuliza na alivyo jinasibu mkuu katika janga hili yawezekana ni tatizo la washauri wake zaidi. Hawa kina Kabadi hawa. Hawa kina makondakta hawa

Ninaamini serikali inajua bila hatua za total lockdown huu ugonjwa hauwezi kabisa kudhibitika na wala hatuwezi kuwa na maendeleo yoyote. Ila kwa makusudi wameamua kutuweka rehani kwanza.

Ni vyema wakajua tutajua kwa nini wanajivuta vuta wakituweka wananchi wote hatarini.

Mwalimu ni muda mzuri tutajajua tu. Maana fumbo mfumbie mjinga and you cannot fool all the people all the time.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,660
2,000
2. Hoteli zetu kutoza kiwango cha chini cha Tshs laki 2 kwa watakaojiweka karantini kwa siku moja pekee. Hili ni jambo la aibu sana kwetu kama nchi. Kwa wenzetu jambo hili limeihusisha jamii yote huku Rais wa nchi akiwa kamanda mkuu wa kikosi pambanaji. Hapa kwetu hakuna control yoyote juu ya jambo hili iliyoandaliwa hadi pale walipogutuka baada ya watu kulalamika. Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa. Nimejiuliza, hata kwa hili hawakujiandaa? Yani mtu mwenye matatizo ambapo imembidi kuwekwa ama kujiweka pale ili kuwanusuru wengine anaenda kutozwa hela ya malazi ya anasa? What a shame! Mbaya zaidi kamanda mkuu yupo Dodoma anapiga picha akiwa amelala juu ya jiwe! Huu ni mzaha na kuwachukulia watu wako "Too low"
Hili la kupelekwa hotelini tena za bei juu hata Kenya kuna tatizo kubwa. Ingekuwa vizuri wakatafuta namna nyingine au wapige marufuku kabisa kusafiri kuja Tanzania/Kenya kwa muda. Na wasafiri nadhani wanatakiwa wajiepushe kusafiri kipindi hiki labda kwa dharura tu. Soma hapo kwenye link chini

It’s a living hell for Kenyans flying back from overseas
 
Hili tatizo linajitokeza baada ya serikali kuamua kujiweka kando. Yani hadi watu walalamike! Kwa Kenya bei ina afadhali kuliko sisi kutoza kiwango kilekile cha kawaida kama watu wanaenda kufanya starehe kule.
 
Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,594
2,000
Kwakweli serikali ya Tanzania imelichukilia janga la COVID-19 kama jambo la mzaha kupita kiasi, hali hii imewafanya baadhi ya wananchi kubweteka kupita kiasi kutokana na janga hili.

Kwa haya niliyoshuhudia, nachelea kusema kuwa ikitokea COVID-19 ikaiathiri Tanzania kwa kiwango kikubwa basi mataifa mengine yataandika nne na kutucheka kwa kejeli. Haya yanasababishwa kwa kiwango chote na viongozi wetu wa serikali tuliowapa mamlaka ya kutuongoza. Nitaainisha uzembe huu uliopindukia katika maeneo machache.

1. Ni jambo la aibu sana baadhi ya raia wa Tanzania kuvuka mpaka wa Tanzania na Uganda na kisha kukamatwa ndani ya Uganda wakati kila nchi inalichukulia jambo hili kwa uzito wa aina yake labda isipokuwa Tanzania. Ni jambo la aibu kwa sisi kutumia uzembe wetu na kutokujua mambo kupeleka mzigo kwa wenzetu, kwa hili najisikia aibu sana kama Mtanzania.

Kwa jambo kama hili Uganda watatuona sisi kama watu wa mzaha sana kiasi kwamba mzaha wetu tunaupeleka hadi kwenye nchi za wenzetu ambazo kwa namna ya kipekee wamelichukulia jambo hili kwa umuhimu na ukubwa wa kiwango chake. Kwanini mamlaka za Tanzania mipakani hazikuwazuia watu hawa hadi wakavuka mpaka kati ya Uganda na Tanzania? Hawakuona umuhimu wa kuwaheshimu wenzetu walioamua kufunga mipaka yao ili kuikabili Corona kwa vitendo?

2. Hoteli zetu kutoza kiwango cha chini cha Tshs laki 2 kwa watakaojiweka karantini kwa siku moja pekee. Hili ni jambo la aibu sana kwetu kama nchi. Kwa wenzetu jambo hili limeihusisha jamii yote huku Rais wa nchi akiwa kamanda mkuu wa kikosi pambanaji. Hapa kwetu hakuna control yoyote juu ya jambo hili iliyoandaliwa hadi pale walipogutuka baada ya watu kulalamika. Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa. Nimejiuliza, hata kwa hili hawakujiandaa? Yani mtu mwenye matatizo ambapo imembidi kuwekwa ama kujiweka pale ili kuwanusuru wengine anaenda kutozwa hela ya malazi ya anasa? What a shame! Mbaya zaidi kamanda mkuu yupo Dodoma anapiga picha akiwa amelala juu ya jiwe! Huu ni mzaha na kuwachukulia watu wako "Too low"

3. Utolewaji wa taarifa za mara kwa mara na kuwekeza nguvu kwenye vituo vya kupimia ugonjwa huu pamoja na kuwekeza nguvu kwenye kudhibiti usambaaji. Ni aibu kubwa kuwa Rais kasema kuwa anapeleka fedha za Mwenge kwenye kupambana na ugonjwa huu ila hakuna lolote kuhusu kupambana huko. Vituo vya usafiri wa umma, mahospitali mengi hakuna viosha mikono, hakuna kupulizia dawa. Yani tupo kila mtu na lake. Mbaya zaidi hakuna taarifa za mara kwa mara kutoka kwa wahusika wa kutoa taarifa. Yani kwa kifupi ni kama serikali imelala kupita kiasi! Ni aibu eti sampuli zote ndani ya nchi zinapelekwa kituo kimoja pekee cha kupimia. Hatuoni kuwa tutakuwa tunachelewesha kuwabaini waathirika kwa haraka? Hatuoni madhara haya ya ucheleweshaji mpaka sasa?

4. Swala la mkuu wa mkoa wa Dar kutoka asubuhi asubuhi na kupeleka ujumbe kwa watu kuwa kuna mtoto wa Mbowe anaugua Corona. Ukiusoma uso wa Paul Makonda ni kama amepata "relief" fulani kwa mtoto wa Mbowe kuumwa ugonjwa tena kwake furaha zaidi ni Corona. Hakuna kiongozi hata mmoja aliyekosoa ujinga huu! Tunaanzaje kuwaamini kuwa mpo serious? Alichofanya Paul Makonda ni utoto mtupu na kwa alichofanya hakutakiwa kuendelea kuwa kiongozi. Lakini kwakuwa tayari kuna udhaifu, basi limeonekana ni jambo la kawaida kabisa kwa viongozi wa kitaifa wenye dhamana.

5. Hakuna uhamasishaji kwa watu wenye uwezo kujitoa ili jamii nzima iwe salama. Hili kimsingi linatakiwa kufanywa na serikali. Lakini kwakuwa hakuna kujali basi na wao wameamua kujikalia kimya tuu ili mradi liende huko litakakotua.

Mwisho naomba nieleze masikitiko yangu kuwa kwa hili jambo basi ni hatuna serikali makini. Pia ni heri watu wakajichukulia tahadhari wenyewe na pengine wanayoambiwa na serikali ya Tanzania basi wachanganye na zao! Hakuna uaminifu kwa kiwango kikubwa mno kutoka serikalini kuhusu janga hili la COVID-19.
Ulichoandika ni ukweli mtupu. Serikali hii ya jiwe ni janga si kwa nchi yetu tu bali kwa Afrika Mashariki yote.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,660
2,000
👇👇👇
👇👇
Hili tatizo linajitokeza baada ya serikali kuamua kujiweka kando. Yani hadi watu walalamike! Kwa Kenya bei ina afadhali kuliko sisi kutoza kiwango kilekile cha kawaida kama watu wanaenda kufanya starehe kule.
Kenya nao wanalalamikia bei. Dola 50 kwenda juu kwa siku.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,242
2,000
Na kama nimesikia vizuri kupitia taarifa ya habari ya Radio Free Africa usiku huu, tarehe 28 mwezi huu tunasitisha kupokea flight za kimataifa pale JNA kwasababu ndege zimepungua na si kwasababu ya kudhibiti ugonjwa.
 
Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,594
2,000
Hili la kupelekwa hotelini tena za bei juu hata Kenya kuna tatizo kubwa. Ingekuwa vizuri wakatafuta namna nyingine au wapige marufuku kabisa kusafiri kuja Tanzania/Kenya kwa muda. Na wasafiri nadhani wanatakiwa wajiepushe kusafiri kipindi hiki labda kwa dharura tu. Soma hapo kwenye link chini

It’s a living hell for Kenyans flying back from overseas
Kwa kujibu wa taarifa kwenye hiyo link, Kenya wanapewa alternative, (hadi hostel za chuo zinatumika). Na hata hiyo hotel aghali iliyotajwa rate yake ni US$ 60 ambayo ni chini ya laki mbili inayotozwa hapa kwetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom