Serikali inaweza kuonesha udhaifu mkubwa sana tarehe 24.01.2024

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
CHADEMA wametangaza kufanya Maandamano ya amani mnamo tarehe 24.01.2024 jijini Dar es salaam. Wakati huo RC wa Dar es salaam inasemekana naye ameamru vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama wakiwemo JWTZ kufanya usafi siku hiyo hiyo katika jiji hilo.

Kama Serikali itawaamru wanajeshi kuzagaa mitaani kwa kisingizio cha kufanya usafi siku hiyo, kwa hakika Serikali itakuwa imeonesha udhaifu wa kiwango cha juu sana.

Katika mkasa huo, watakaoonekana ni washindi ni CHADEMA. Atakayeonekana ameogopa ni Serikali.

Kama CHADEMA kutangaza tu Maandamano, Serikali inatetemeka kiasi hicho, je, Al shaabab wakitangaza vita hali itakuwaje?

Si ndo viongozi wetu watakimbia kabisa Nchi hata kabla ya vita kuanza?

Big up CHADEMA. Endeleeni kuwachezesha muziki.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Lakini pia kwanini Serikali inaogopa Maandamano ya chama kilichosajiliwa kihalali na Maandamao ni takwa la kisheria..

Kama wameruhusu MIKUTANO YA HADHARA kwa nini hawataki Maandamano ya AMANI?..huku si ni KUVUNJA Katiba?

Ruhusuni Wananchi watoa MAONI yao!
 
  • Thanks
Reactions: apk
Na amini siyo yeye ila ni mawazo ya KIZIMKAZI aliyejificha kama ni mtu wa demokrasia.
 
Back
Top Bottom