Nimefuatilia mtiririko wa visa, ni wazi kuwa Ndugai aliota mapembe na alikuwa akimdharau sana Rais Samia

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,117
4,808
Ukweli ni kwamba, Ndugai amekua mbabe kwa muda mrefu sana kwa wabunge kule mjengoni lakini alikua mtiifu namba moja wa Rais John Magufuli (R.I.P).

pamoja na mapungufu yote ya serikali ya JPM ikiwa ni pamoja na bajeti hewa mfano kuna baadhi ya wizara zilikua zinapewa hela ya bajeti 18% tu ya zile zilizotegemewa na hasemi,

Kipindi cha JPM mikopo mingi ilikopwa bila kuidhinishwa na bunge, miradi mingi ilifanyika bila kupitishwa na bunge, sikuwai kusikia hata sikumoja ndugai anasemea haya zaidi tu ni kuwa wapinzani walikua wakiibua hizi hoja anawazima,

Ndugai alimtii sana JPM na alimuheshimu kama Rais kamili

Tatizo lilikuja tu alipoapishwa Rais mwanamke, nafikiri hapa tatizo ni jinsia

Ndugai alianza kuota mapembe nakumbuka mtiririko wa visa Ndugai mbele ya hadhara na Media anasema "mwanamke ni mwanamke tu, huwezi kujilinganisha na mwanaume, unaenda kila sehemu unajisema wewe ni mwanamke kwani nani hajui? " hapa ni dhahiri kabisa Job alimlenga Rais na ukifuatilia clip ile ni wazi kabisa alikuwa akimteta Samia Suluhu.

Mbali na hilo nakumbuka siku ya kupokea fedha za uviko ile hafla Ndugai alipopewa nafasi ya kuongea ni kama vile alikuwa anafokea watu, Ndugai alikuwa akilalamika waliopanga ujenzi wa madarasa wapange kulingana na idadi ya watu wa kwenye majimbo, ni kweli kauli yake ilikuwa na mantiki lakini kwa namna alivyoongea ni kama vile alikuwa anafokea watu, imagine Sehemu ambayo na Rais yupo unaongea kama unafokea watu as if wewe ndio kiongozi mkuu upo unahutubia watoto, nilijiuliza sana siku ile ila nikanyamaza,

Hii ya kuhusu mkopo wa juzi huyu Job inawezekana alichoongea kina mantiki lakini ni kwa namna gani alikiwasilisha, alikuwa anamfokea nani pale? Ni kama vile alikuwa anamfokea aliyefuata huo mkopo, na kwanini ahusishe mkopo ule na uchaguzi wa 2025? kwanini aliwahii kisema uchaguzi wa 2025 tutaamua wenyewe?

Aisee itoshe tu kusema Ndugai aliota mapembe akaanza kujiona yeye ndio mkuu wa nchi Ndugai hana uchungu wowote na nchi hii isipokua hamataki Rais Samia, na hamtaki kwasababu ni mwanamke kiufupi Ndugai ana dharau hafai kuendelea kuwa spika wa Bunge amekosa heshima

Afukuzwe iwe fundisho kwa wote wenye dharau za kijinga

Anachofanya ni uhaini, Afukuzwe bila kuonewa haya angekuwa na uchungu na hii nchi asingeacha JPM akaenda kukopa mikopo ya kibiashara tena ya muda mfupi, angalia leo hii hata reli ya SGR haijakamilika lakini mikopo yake imeshaanza kurejeshwa tena na Riba juu, Ndugai alikuwa halijui hilo? Ndugai anajua nchi inapoteza shingapi kwa kuwalipa wabunge wasio na vyama? Ana uchungu gani na hii nchi huyu mtu analeta chuki zake binafsi dhidi ya Rais

Nataka kumwambia Job acheze na wabunge wake huko Taasisi ya Urais aachane nayo, dharau zake apelekee wagogo huko
 
Hapo ndipo mnapokosea kuangalia nani kasema badala ya nini amesema. Kubeba uchungu na kufurahia kwa misingi ya visasi, hakutakuondoleeni dhiki ya makosa yanayofanyika kama yapo.

CCM walipinga kila kilichosemwa bungeni na wapinzani, wakipigia makofi kila hoja ya serikali matokeo yake wamejikuta wako chaka, wanaanza kutoana macho wkati wamechelewa.

Ninaomba tujikite kujadili hoja ya Ndugai, hayo makosa yake yapo tu na yanaweza kujadiliwa lakini tusi nullify hoja nzito na za msingi na zenye maslahi kwa taifa eti tu kwa vile aliyesema ni mtu tuliye na uchungunaye. Haitupeleki kokote.

Ushabiki wa kufuata mikumbo ama misimamo ya kisiasa haina tija linapokuja suala la mustakabari wa Taifa. Vinginevyo hatutakuwa tofauti na mafisadi wa ccm.
 
Alimwona mwendazake kama Mungu wake...

Ikulu ilikuwa kama nyumbani kwake...

Hakuna shughuli aliyoifanya Mwendazake, mgogo asiwepo.

Alipoingia mama akakata mguu kutinga ikulu. Akianza kuikandya serikali kiaina.

Siku akauliza siku hizi mbona watu wa serikali hawaonekani Dodoma. ... hili lilikuwa dongo la kwanza kabisa kwa mama....

Baadae ile kauli "haina haja ya kusema mimi mwanamke, tunajua wewe ni mwanamke".... dongo la pili mama katulia tu

Sasa hili la mikopo.... wakati awamu zote zilizopita walikopa na mgogo nakusoma kitu... mama akaona isiwe tabu

Akamtengenezea bonge la taarab.... mgogo kachemka kuicheza kaenda zake kutulia nyumbani

Taarab la Samia, Khadija Kopa anasubiri sana.
 
Hapo ndipo mnapokosea kuangalia nani kasema badala ya nini amesema. Kubeba uchungu na kufurahia kwa misingi ya visasi, hakutakuondoleeni dhiki ya makosa yanayofanyika kama yapo...
Ndugai anahoja zipi za kijinga zile?

sasaivi kuna mikopo iko matured na haikukopwa na Rais samia, Rais anachokifanya anachukua mikopo isiyo na Riba na anaenda kulipa kwenye hiyo yenye Riba

hivi zaidi ya hilo mlitaka afanyeje? hii nchi haiwezi kulipa madeni na bado ikatumia fedha za ndani kuendeleza miradi, akifanya hivyo atashindwa hata kulipa mishahara ya watumishi,

sasabkipi bora akope mikopo ya kibiashara kama JPM au akope mikopo isiyo na riba?
 
Ukweli ni kwamba, Ndugai amekua mbabe kwa muda mrefu sana kwa wabunge kule mjengoni lakini alikua mtiifu namba moja wa Rais John Magufuli (R.I.P)...
Katika
Ukweli ni kwamba, Ndugai amekua mbabe kwa muda mrefu sana kwa wabunge kule mjengoni lakini alikua mtiifu namba moja wa Rais John Magufuli (R.I.P)..
Katika mambo kama haya ndipo natofautiana na WA Tanzania wenzangu Kwa tabia za kinafiki, na uvivu was kufuatilia mambo pamoja na kutafakari mambo, Huyu kwa hakika asinge stahili na hastahili kuwepo katika nafasi aliyonayo. Miaka mingi nasema amekuwa akilihujumu taifa wazi wazi.
 
Ukweli ni kwamba, Ndugai amekua mbabe kwa muda mrefu sana kwa wabunge kule mjengoni lakini alikua mtiifu namba moja wa Rais John Magufuli (R.I.P)
pamoja na mapungufu yote ya serikali ya JPM ikiwa ni pamoja na bajeti hewa mfano kuna baadhi ya wizara zilikua zinapewa hela ya bajeti 18% tu ya zile zilizotegemewa na hasemi,

Kipindi cha JPM mikopo mingi ilikopwa bila kuidhinishwa na bunge, miradi mingi ilifanyika bila kupitishwa na bunge, sikuwai kusikia hata sikumoja ndugai anasemea haya zaidi tu ni kuwa wapinzani walikua wakiibua hizi hoja anawazima,

Ndugai alimtii sana JPM na alimuheshimu kama Rais kamili

tatizo lilikuja tu alipoapishwa Rais mwanamke, nafikiri hapa tatizo ni jinsia

ndugai alianza kuota mapembe nakumbuka mtiririko wa visa ndugai mbele ya hadhara na Media anasema "mwanamke ni mwanamke tu, huwezi kujilinganisha na mwanaume, unaenda kila sehemu unajisema wewe ni mwanamke kwani nani hajui? " hapa ni dhahiri kabisa Job alimlenga Rais na ukifatilia clip ile ni wazi kabisa alikua akimteta samia Suluhu,

mbali na hilo nakumbuka siku ya kupokea fedha za uviko ile hafla ndugai alipopewa nafasi ya kuongea ni kama vile alikua anafokea watu, ndugai alikua akilalamika waliopanga ujenzi wa madarasa wapange kulingana na idadi ya watu wa kwenye majimbo, ni kweli kauli yake ilikua na mantiki lakini kwa namna alivyoongea ni kama vile alikua anafokea watu, imagine Sehemu ambayo na Rais yupo unaongea kama unafokea watu as if wewe ndio kiongozi mkuu upo unahutubia watoto, nilijiuliza sana siku ile ila nikanyamaza,

hii ya kuhusu mkopo wa juzi huyu Job inawezekana alichoongea kina mantiki lakini ni kwa namna gani alikiwasilisha, alikua anamfokea nani pale? Ni kama vile alikua anamfokea aliefata huo mkopo, na kwanini ahusishe mkopo ule na uchaguzi wa 2025? kwanini aliwai kisema uchaguzi wa 2025 tutaamua wenyewe?


Aisee itoshe tu kusema ndugai aliota mapembe akaanza kujiona yeye ndio mkuu wa nchi Ndugai hana uchungu wowote na nchi hii isipokua hamataki Rais Samia, na hamtaki kwasababu ni mwanamke kiufupi Ndugai ana dharau hafai kuendelea kuwa spika wa Bunge amekosa heshima


afukuzwe iwe fundisho kwa wote wenye dharau za kijinga

anachofanya ni uhaini, Afukuzwe bila kuonewa haya angekua na uchungu na hii nchi asingeacha JPM akaenda kukopa mikopo ya kibiashara tena ya muda mfupi, angalia leo hii hata reli ya SGR haijakamilika lakini mikopo yake imeshaanza kurejeshwa tena na Riba juu, ndugai alikua halijui hilo? Ndugai anajua nchi inapoteza shingapi kwa kuwalipa wabunge wasio na vyama? anauchungu gani na hii nchi huyu mtu analeta chuki zake binafsi dhidi ya Rais

nataka kumwambia Job acheze na wabunge wake huko Taasisi ya Urais aachane nayo, dharau zake apelekee wagogo huko
Kwani wagogo siyo watanzania? Hapo ndio umeharibu kabisa
 
Samia asiende kwenye hayo maombi yaliyoandaliwa na huyo mpiga zumari wa Ibilisi badala yake aalike Taarab nzuri iende kutumbuiza Ikulu nina wasiwasi sana na mziki wa Taarab huenda ukapotea hapa Nchini aupe promo.
 
Ukweli ni kwamba, Ndugai amekua mbabe kwa muda mrefu sana kwa wabunge kule mjengoni lakini alikua mtiifu namba moja wa Rais John Magufuli (R.I.P)...
Maandiko ya kiuchonganishi haya.

jitahidi uwe sehemu ya usuluhishi hapa duniani.

usibez kwenye kuchochea ugonvi na mifarakano itakusaidia
 
Hivi ukiwa mgogo na ukawa Spika wa bunge, unanyanganywa haki yako ya freedom of speech? Freedom of speech ni kwa kila mtanzania - tujadili hoja yake.,siyo Kabila lake au yeye mwenyewe! Mnaogopa kujadili hoja anazozileta mnakimbilia kujadili utu wake - hii siyo sawa.
Ukweli ni kwamba, Ndugai amekua mbabe kwa muda mrefu sana kwa wabunge kule mjengoni lakini alikua mtiifu namba moja wa Rais John Magufuli (R.I.P)...
 
Ukweli ni kwamba, Ndugai amekua mbabe kwa muda mrefu sana kwa wabunge kule mjengoni lakini alikua mtiifu namba moja wa Rais John Magufuli (R.I.P)...
Kwa msiojua Ndugai alianza kuidai Serikali itekeleze mradi wa Bandari ya Bagamoyo anzia mwaka 2019 kipindi hichi bado Magufuli hajafariki, kwaiyo nyie semen kuwa hamtaki kusikia mawazo mengine

 
Hivi ukiwa mgogo na ukawa Spika wa bunge, unanyanganywa haki yako ya freedom of speech? Freedom of speech ni kwa kila mtanzania - tujadili hoja yake.,siyo Kabila lake au yeye mwenyewe! Mnaogopa kujadili hoja anazozileta mnakimbilia kujadili utu wake - hii siyo sawa.
Ameshindwa kutekeleza wajibu wake kwanafasi take haaminikitena, hata Imani kidogo iliyokuwa imesalia ameifuta rasmi tena yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom