Nimefika safari yangu, wife hajaniuliza hata kama nimefika salama

ukiona hivyo tatizo sio kuulizwa kama amefika kuna Tatizo kubwa lipo nyuma ya paziaaa linamfanya jamaa akose amani.
Mume asimame kiume kusolve tatizo badala ya kumwagia petrol anazidi kuukoleza moto.

Msiwe solid saaaana kwa wake zenu. Ni sawa unakuwa unakaza lakini sio Kila wakati unakaza tuuuuuuuu utafikiri umeoa komandoo!! Tena unamkazia wakati umesafiri ??

Maisha hayaendi hivo. Ni misimamo ya ujanani anyway
 
Ofcoz tulikuwa na kamgogoro flani wakati naondoka..
Lakini ni masaa 14 toka nifike in my destination ila wife hata hajanipia kunijulia hali ila whatsapp yuko mudo wote namuona online.

Nifanyaje wakubwa?
unajua panapo tatizo baina yako na mkeo,ujue tatizo hilo nyie nyote mmelichangia,halijasababishwa na mmoja tu,hivyo kaeni mtafute ufumbuzi wa pamoja
 
Kosa ulilofanya ni kusafiri kabla ya kutatua huo mgogoro, linapotokea jambo kama hilo la kusafiri huku kukiwa na mgogoro, hakikisha unatafuta kwanza suluhu ndipo usafiri, ulichokifanya ni hatari kwa afya ya ndoa yenu...

Wewe cha kufanya ni kumpigia simu na kumjulusha kuwa umefika salama bila kujali mgogoro uliopo baina yenu, la sivyo anaweza fanya jambo baya au wewe ukafanya jambo baya kama njia ya kunifariji.
 
Hayo mawazo taratibu yanakuletea kisukari na presha kwa kuyakaribisha bila kujua wewe potezea endelea na ratiba zako hapo utawaza mengi unaishia kujivuruga akili kisa mke, kuwa mwanaume tuma ujumbe habari nimefika salama ajibu asijibu atajua mwenyewe alafu endelea na mishe zako
 
Back
Top Bottom