Ndio marafiki tulio nao kwa siku za leo na uaminifu umekwisha
Huwa sitaki sana kukumbuka marafiki maana ni mengi yamepita
mkuu mfuatilie na kama unafaham ofisi yake mfuate kabisa muonane uso kwa uso umsikilize nakuja na sera gani
Ila nahisi alitaka anipige M15 ile siku ya kwanza, sijui ningekuwa katika hali gani kwasasa
achana nae huyu, life will tell nakuambia!!!!!
Hii dhambi itamsumbua miaka yake yote
Mkuu Mvaa Tai pesa yako uliyoipata kwa jasho lako italalaje nje kwa miezi saba Mkuu huku jamaa akiendelea kukufanyia usanii wa kutotaka kuongea nawe!? Mfuate kazini kwake Mkuu ukamwambie bila kumung'unya unataka pesa yako haraka sana na ufuatiliaji uwe ni wa kila wiki usimpe nafasi kabisa ya kumuonyesha kama vile hiyo pesa yako ndio umekubali kwamba ameshakudhulumu. Fuatilia kwa karibu sana Mkuu kama ulivyoshauriwa na akina Rocky na Heaven on earth na kama hutajali rudi hapa kutufahamisha matokeo ya ufuatiliaji. Kila la heri.
duh kikulacho kiko nguoni kwako jaribu kuendelea kumvumilia tu kama alivyokuambia ila taa ya hatari inakaribia kuwaka
huu ushauri akiufanyia kazi,mbona pesa yake atalipwa maana jamaa ataona imekuwa kero.
Nakumbuka nilikuwa na Biashara na rafiki yangu, mimi ndio niliyevumbua ile Biashara nikamshirikisha na yeye, tukawa tunafanya pamoja, Mzigo tunapeleka wote, pesa ikitoka napokea mimi tunagawana sawa bin sawia, siku moja nilimuagizia yeye achukue ile pesa, kilichotokea !!? alitia ndani pesa yooote, niliamua kuiua ile Biashara na hatukuongea kwa mwaka 1, japo tulikuwa ofisi moja, Sikutaka Boss wetu ajue, lakini alihisi kuna kitu kinaendelea kati yetu, japo kulikuwa na maneno yakiendelea kwa kuwa mwanamke ambaye niliachana naye yeye akawa naye hivyo wengine walihisi hicho ndio chanzo cha ugomvi wetu, hii ilikuwa zamani kidogo.
Mkuu Renegade umenikumbusha machungu yangu na hii issue huwa sipendi hata kuiongelea maana bora hata wewe ya kugawana mimi sikupata kitu kwenye ile biashara na kairusha moja kwa moja na kabadilisha kila kitu kiko kwenye jina lake na jamaa alikuwa rafiki yangu mkubwa na nilimthamini kama ndugu yangu ila mwisho niliona nyota nyota bana