Nimefanyiziwa na rafiki!!!!

Nimefanyiziwa na rafiki!!!!

Pole sana Mr Rocky, mkionana vp hasemi lolote? Msumbue angalau uambulie nusu hasara!

Nilichoishia kumwambia ni kwamba anirudishie tuu initial costs nilizotumia kama malipo ya kodi kwa miaka miwili na matengenezo ya ile sehem iwe ya biashara
Tunaonana mkuu Renegade ila ni kama wala ha=oni tatizo kwake ni poa tuu ila nimeshamuondoa kwenye list ya rafiki ni kama mshkaji tuu siku ziende
 
Last edited by a moderator:
in my life i have no permanent friend even permanent enemy but am permanent on issue take as normal,pull up you are socks aluta continoue!!!
 
Pole sana..daah...mimi sikopeshi watu naogopa kuvunja undugu au urafiki.....nadhani umejifunza vema..wkt mwingine never never
 
Ukitaka kugombana na rafiki au ndugu mkopeshe!!! Ni bora ukatae au amua kutoa kama msaada. Asilimia kubwa hawalipi halafu ukidai lawama kibao.
 
Pole mkuu umenikumbusha the same story ya kudhulumiwa na rafiki wa karibu, kwa sasa mimi ninapotoa ela kwa rafiki au ndugu ninatoa kama sadaka zikirudi sawa zisiporudi sawa. Hapo roho itakuuma zaidi kwa mambo na maneno yatakayotokea baada ya wewe kuchukua hatua wewe ndio utaonekana hujui ubinadamu na maneno mengi, usimuamini mtu siku nyingine kwani kukopesha kunaweza kukugombanisha na marafiki na ndugu.

Exactly Mkuu! Ukitaka lawama dai chako!!!
 
achana nae huyu, life will tell nakuambia!!!!!
Hii dhambi itamsumbua miaka yake yote

Tena mpk anaingia kaburini hiyo dhambi atakuwa nayo, na watu wa hivi huwa hawafanikiwa, maana ni matapeli, sasa atatapeli wengi, lakini atakutana na kiboko yake na yeye ndiyo atamuonyesha na kumlipia maovu yoote aliyoyafanya.
Mtu kama huyu Mvaa tai achana naye, na ukikutana naye msalimu na wala usimkumbushie deni, ni kama umemtwika jiko la moto kichwani maana atabaki na mawazo."ADUI YAKO MSALIMU, MPE CHAKULA NA MAJI, UTAKUWA UMEMPALIA MAKAA KICHWANI"
 
...ukiona manyoya ujue keshaliwa. mleta mada tuna RB? umeshakwenda ofisini kwa mwajiri wake? weka picha hapa tukusaidie kumtafuta. Vinginevyo tulia tu.
 
achana nae huyu, life will tell nakuambia!!!!!
Hii dhambi itamsumbua miaka yake yote

Sana tu. Kuna mtu alinizima 8m chaajabu nikampigia sim kumwambia kuwa nimemsamehe deni na nimemwachia mungu. Kwa woga wake akakimbilia polisi na kunishtaki kuwa nimemtishia maisha. Baada ya kukosa ushahidi akafuta kesi. Lakini hii leo anasota sana na sio mimi tu alinidhulumu, kumbe ni wengi na hicho ndo kinachommaliza. Jasho la mtu haliliwi bure bana.
 
1383348258696.jpg
 
pole sana mbele ya hela usimuamini mtu yoyotevyule.ila kuna watu wengine wana phd ya utapeli.maneno anayokupa unaingia line tu.huyo jamaa inaonyesha ni mmoja wao.kuna vijana wengine,hawajulikani wanaishi kwa utapeli tu,kazi kufanya hawataki wanaona haylo ndio maisha.ipo siku atapatikana tu
 
Marafiki wa kibongo. nuksi tupu. pole
 
kweli aisee mimi siachi kumkopesha mtu kama nnacho!!!ila nakukopesha kwa bond ukienda kulalama huko ooh jamaa nimempa laptop ya 1m kwa laki 3 cjui nini cjui nini utajiju ila mi najua nimekusaidia na utarudisha nitamsaidia mwingine!!!na ukizingua nauza laki saba nakupa laki nne zako...na sio muda nafungua micro ili niwe naweka na riba na kuchukua vitu juu....maana naona wanakuja kukopa wanaweka bond wanaenda kunisengenya wanalipa wanaenda kunisengenya tena etii ooh nimemrudishia viela vyake mara blah blah...wanaishiwa wanakuja tena na laptop ile ile nawapa kwa masharti yale yale na wanaendelea kulipa sasa nitaweka hiyo twenty % ya kujifutia machungu ya majungu...hakuna ubinadamu

Duu nimecheka sana
 
Mmenipa uchungu....nilimkopesha rafiki yangu alipungukiwa ada 1.2m na ilikua ni karibu na mitihani so angekosa kadi ya kufanya mtihani. Ni mfanyakazi na najua hadi kiasi cha mshahara wake mpaka ninavyoongea research amemaliza na anagraduate dec 2013. Kila nikimuuliza esa yangu ananipa matatizo ya nyumbani kwao na hii ni toka june 2012. Hata kupunguza japo 50,000 amegoma. Namuachia mungu.

Pole kiongozi nilidhani nimimi tu ndo nimefanyiwa mbaya na rafiki
 
Marafiki hawakopeshani bhana wanapeana tuuuu mimi huwa sikopeshi nje ya kiasi ambacho nikizikwa nitalalamika; kama mtu anataka milioni 5 namwambia nina laki 8. Kichwani nishapima kama hazirudi ni poa tu kama msaada kwa jamaa yangu

Ningalijua kwamba nitapigwa, ningemsaidia laki1
 
Back
Top Bottom