Nimefanyiziwa na rafiki!!!!

Nimefanyiziwa na rafiki!!!!


Mkuu kwanza pole, watu dizaini hiyo wanakera kweli yani!

Jiatahidi kutafuta evidence including transactions na maelezo ya mshkaji wako mwenye duka....Ukipata ushahidi wenye mashiko basi Alhamndulilah.

Kisha kwa sababu ni rafiki na jirani na kwa mbali kama ndugu. Mtafute mtu wa karibu yenu na kwa pamoja mumfuate mshikaji umweleze mwanzo mwisho usumbufu aliokusababishia. Kisha umpe deadline la kulipa kulingana na mtakavyoelewana.

Akishindwa fikisha kesi kwa wazazi/ndugu zenu huko kijijini. Ikishindikana nenda polisi na ushahidi wako kama akiweza kutiwa nguvuni basi tunamshukuru Mungu!
Kupata evidence kuna ugumu kidogo maana nilimpa mkononi na hakuna meseji tuliyoandikiana zaidi ya meseji yake ya mwisho aliniandikia ya kuniambia amekaa Samaki samaki karibu na entrance baada ya hapo kila kitu tumekuwa tukipigiana simu tu, najifikiria kama inawezekana kupata sauti yake pale Vodacom lakini naona nitajichoresha sana maana hela yenyewe ni mbuzi ukilinganisha na mchakato wa kupata evidence
 
Tumezaliwa kijiji kimoja, nimekuwa naye kijijini na nimesoma naye shule ya msingi, tuliachana tukiwa tunakwenda Secondary mpaka tunamaliza vyuo vikuu ambavyo tumesoma vyuo tofauti, tulikuwa tukionana pale kijijini mara chache sana wakati wa likizo mpaka tulipomaliza chuo.

Baada ya kumaliza chuo tulionana Dar katika mihangaiko ya kutafuta kazi, tulibahatika kupata kazi katika Taasisi mbili tofauti, yeye alipangiwa mkoani mimi nilipata nafasi hapa hapa Dar, ni zaidi ya miaka sita hatukuwahi kuonana face to face zaidi ya kuwasiliana kwa simu na kuchart kwenye mitandao.

Mwaka 2012 alihamishiwa kikazi hapa makao makuu ya Taasisi yao, kutokana na ukweli kwamba hapa mjini mambo ni mengi hivyo imekuwa ngumu sana kuonana mara kwa mara kwa masaa ya kutosha kiasi kwamba tunaweza tukastukiana kama kuna mabadiriko makubwa ya tabia baina yetu, tumekuwa tukionana mara chache sana tena sehemu za Starehe.

Mwezi July2012 alinishirikisha deal moja zuri sana lilikuwa la maslahi ya kutosha lakini, ilitakiwa nichangie kama Million15 ndani ya wiki moja, kutokana na hali yangu kifedha nilipigana sana ndani ya wiki hiyo ikaniwia ngumu kuikamata M15 hivyo nikalikosa lile deal nilisikitika sana.

Mwezi April 2013 miezi saba iliyopita ilikuwa ni jioni siku ya jumapili alinipigia simu kwamba yupo Mlimani City kuna transaction ya 2,500,000 anataka kuifanya amefanikiwa kutoa 800,000 lakini kadi imezama itabidi aifuate kesho yake asubuhi, akaniambia anahitaji hard Cash 1,700,000 za haraka haraka kama itawezekana vinginevyo atapata hasara kubwa, kiukweli ishu aliyoniambia ilikuwa ni lazima niamini, isitoshe ni mshkaji.

Kutokana na ukweli kwamba huwa ananisifia kwamba mimi ni 'ALWATANI' hapa mjini nililazimika kupambana ili ipatikane hiyo 1,700,000 nisimuangushe jioni hiyo hiyo japo mimi nilikuwa na 900,000 kwenye Akaunti yangu nikaongezea na 700,000 kutoka kwa mshkaji wangu aliye na duka pale Mwenge, then nikamkabizia.

Kesho yake asubuhi ya saa4 alinipigia simu kwamba wamepatwa na msiba wamefiwa na mfanyakazi mwenzao Ofisini yeye kateuliwa kuwa mmoja wa watu waliotakiwa kwenda Kilimanjaro kupeleka Maiti/Msiba, hivyo akadai akipata time atachomoka mara moja aende Benki arekebishe ule mzigo, siku hiyo hakufanya hivyo sikutaka kumsumbua sana nikasubiri arudi ila nikajitahidi kumalizana na mshikaji wangu wa dukani kwa kuhamishia deni kwa mtu mwingine, aliporudi toka Kilimanjaro akanishirikisha tatizo lingine, amekuwa akifanya hivyo kila ninapompigia huku akiniomba nimvumilie.

Siku zimekwenda miezi inakatika mpaka sasa nikimpigia simpati nahisi kani-Block, nikimpigia kwa simu nyingine anapokea lakini akistukia ni mimi ananikatia simu, hiki kitu kimekuwa kinanikera sana hakuna kitu kinachokera kama kukatiwa simu na mtu ambaye wewe unadhania ni rafiki yako.

Wadau nishaurini nimfanyeje huyu jamaa, ikumbukwe kwamba sina ushahidi kwamba kanidhulumu na kanisababishia usumbufu.

Pole sana ndugu usipo onana na mtu kwa miaka miwili, tegemea mabadiliko makubwa sana kwa huyo mtu. Rafiki yako amebadilika, amekuwa tapeli.
 
Tafuta manati ya mzungu. Mtokee umwambie kwamba umeshafanya maamuzi. Kitakachofuata ni news tuu. Rafiki wa hivi anakera sana.

Manati ya mzungu yapo kaka ila niliwahi kufikiria kitu kama hicho wife akanishauri nisifanye hivyo maana tunaweza kuzalisha tatizo kubwa zaidi ya hilo
 
Una uhakika bado yuko kwenye hiyo kazi mpaka sasa? manake hapa pananukia harufu ya utapeli!! huyu jamaa ni tapeli mzoefu.

Ni mfanyakazi bado katika taasisi hiyo.
 
Kibaya zaidi si kila mtu yupo hivyo, hii ni changamoto kwakweli

Umenikumbusha na mimi mtu kasepa na 2m zangu ni wiki ya 3 sasa simu yake haipatikani. Kwa hiyo nimeamua kupotezea na kuendelea kulipa deni alilonisababishia. Yaani sometimes nikiwaza hadi naogopa tutashindwa kusaidiana kwenye shida kwa kuwa hatuaminiani sijui tunajenga jamii ya aina gani?
 
ple sana mkuu Mvaa Tai ila kisasi ni cha MUNGU tu so we mwangalie na kumwacha hivyo hivyo ila punguza mazoea na uishi naye kwa akili kubwa sana na uangalifu wa hali ya juu,
madhara ya kisasi:

hujui yeye amejiandaa kiasi gani akiwa ana uhakika kuwa iko siku utaujua ukweli,so unaweza amua lipa kisasi lakini akakushinda au kukuumiza hata zaidi.

kisasi kitakupotezea muda wako bure ambao ungeutumia kutafuta pesa zaidi kuzibia hilo pengo la hasra alilokuletea

mpotezee huyo rafiki mnafiki you still have opportunities to earn more than aliyokudhulumu,ila kuwa makini sana kuanzia sasa mazoea yawe ya salamu tu na sio mambo yako ya pesa au ya ndani zaidi na pia hakikisha hawi karibu hata na mke wako na watoto pia marafiki wa aina hiyo ni hatari sana.

kila la kheri mkuu.
Very useful!!!!
 
Pole mkuu umenikumbusha the same story ya kudhulumiwa na rafiki wa karibu, kwa sasa mimi ninapotoa ela kwa rafiki au ndugu ninatoa kama sadaka zikirudi sawa zisiporudi sawa. Hapo roho itakuuma zaidi kwa mambo na maneno yatakayotokea baada ya wewe kuchukua hatua wewe ndio utaonekana hujui ubinadamu na maneno mengi, usimuamini mtu siku nyingine kwani kukopesha kunaweza kukugombanisha na marafiki na ndugu.
 
Kwanz jamaa laikupiga sound atm kadi ya kutoa 2.5 bado haikuruhusiwa by then....haukuwa makini na je alikuomba mda gani kama ni mchana hata j.pili ilimlazimu kutoa ndani bila hata kadi ni id zake tuu zahitajika....pili alikupiga sound why you of all the pipo umpe hiyo hela!!!!uwe unareason siku nyingine...haupajui kwake au kazini kwake?hupajui panapouzwa maji ya kuchoma!!beba tindikali kampe dozi au kamuharibie kwa ngumi tuu au kazini kwake!!!au mfanyie umafia na wana mumteke mumpige picha za uchi azikomboe kwa mil 6!! Wewe kweli umetoka kijijini matombo....

Kwa hili kweli na kubali upeo wangu uliishia pale
 
Benki gani inatoa muamala wa zaidi ya mil. 1 kwa siku kwa njia ya ATM? Ungelifikiria hilo nadhani ungepambanua ukweli na uongo!
 
Kuna kitu cha kujifunza hapa.... Asante mkuu kwa Stori yako hii sina ushauri kwakuwa na mimi huwa ni Muhanga wa kudai hata kama nina ushahidi lakini nitabadili Tabia.
 
kweli aisee mimi siachi kumkopesha mtu kama nnacho!!!ila nakukopesha kwa bond ukienda kulalama huko ooh jamaa nimempa laptop ya 1m kwa laki 3 cjui nini cjui nini utajiju ila mi najua nimekusaidia na utarudisha nitamsaidia mwingine!!!na ukizingua nauza laki saba nakupa laki nne zako...na sio muda nafungua micro ili niwe naweka na riba na kuchukua vitu juu....maana naona wanakuja kukopa wanaweka bond wanaenda kunisengenya wanalipa wanaenda kunisengenya tena etii ooh nimemrudishia viela vyake mara blah blah...wanaishiwa wanakuja tena na laptop ile ile nawapa kwa masharti yale yale na wanaendelea kulipa sasa nitaweka hiyo twenty % ya kujifutia machungu ya majungu...hakuna ubinadamu
Umenikumbusha na mimi mtu kasepa na 2m zangu ni wiki ya 3 sasa simu yake haipatikani. Kwa hiyo nimeamua kupotezea na kuendelea kulipa deni alilonisababishia. Yaani sometimes nikiwaza hadi naogopa tutashindwa kusaidiana kwenye shida kwa kuwa hatuaminiani sijui tunajenga jamii ya aina gani?
 
acha tu ...kuna watu jamani hawajuagi wengine nao wana shida ya hela..mi nimemuachia tu mungu !
 
Huyo hakuwa rafiki wa ukweli,muhimu ni kumfuta Ofisini kwake kama unapafahamu.
 
Back
Top Bottom