Nimedhalilika ...

Nimedhalilika ...

Wanasemaga wapenzi hawashauriwagi eti rafiki na yote ni kwa ajili ya vitu kama hivyo.

We unajipinda kumshauri mtu kumbe saa hiyo amekuitikia sababu alikuwa na hasira , zikiisha anarudi wanatakana radhi mambo yanaendelea.

Pole rafiki.
Yaani,.
Mbona nimekoma
 
Nimecheka mwenyewe mkuu. Hususani ulivyohitimisha hii stori ya kufedheheshwa!

Mkuu siku nyingine mtu akikuomba ushauri unaohusisha pande mbili, epuka kutoa ushauri wa kuhutimisha. Jitahidi kutoa ushauri kumpa yeye uchaguzi wa mwisho wa maamzi anayopaswa kuchukua!
Kwakweli mambo Yao ni ya kuwaachia wenyewe
 
Sasa wazee/wanaume huwa hatushauri kuvunja ndoa.

Siku nyingine msikilize, kisha muulize moyo wake unamwambia nini? Mwambie avumilie au afuate moyo wake.
Kwanza saizi sitaki kuambiwa na mtu nimshauri kuhusu mapenzi
 
🤣🤣🤣🤣 ndio ukome!

Mapenzi hayanaga ushauri wewe, mie yalinikuta ila nikakataa unyonge, nami nikawachamba.
 
Vituko, kuna mtu kamfumania mke wa mtu akichakatwa mubashara. Akaenda kusema kwa mume wake kuwa mke amechepuka. Mwenye mke akamuambia mke wake nimeletewa unaa kuwa umechepuka, mke akakanusha. Jamaa mwenye mke akamuambia mke wake kuwa aliyemletea habari ni mchonganishi anayetaka kuvuruga ndoa ya watu, mke akamuunga mkono. Habari zikamfikia jamaa mtoa habari kuwa amesutwa na hao wanandoa. Mtoa habari alijisikia vibaya sana licha ya kuusema ukweli kwa mwanamke mchepukaji
Inaumiza sana aisee,.
Asa ukizingatia ulifanya Kwa roho Safi
 
Ilishanitokea hii,Waliachana baada ya miaka kadhaa mmojawapo akawa anahitaji kurudiana,huyu ambaye alikuwa anaombwa warudiane naye akaniomba mimi ushauri, Ushauri niliompa "wasirudiane" Bahati mbaya wakarudiana na waliporudiana yule aliyekuwa ananiomba ushauri akamwambia kila kitu kuhusu ushauri niliompa, Nashukuru Mungu wameachana tena.
Mbona wameachana Tena 😂😂
 
Back
Top Bottom