Nimedhalilika ...

Nimedhalilika ...

Kwanini wewe ulitaka mtu na mume wake waachane? Huo haukuwa ushauri mzuri hata kidogo kwa kuwa haukutafakari mara mbili madhara ya wana ndoa kuachana baadaye inakuwaje
Sio mtu na mke wake,. Labda kama waoane saizi..
Ni mzazi mwenzie na sikua najua kama wakati ananiomba ushauri alikua mjamzito
 
NrNe.....

Wakuu Kuna namna watu wa hii nchi wanajitoaga akili sana..

Mwaka Jana Kuna binti alinifata kuniomba ushauri,. Na Kwa jinsi alivyonihadithia matendo ya My wake nikamshauri kiroho safi aachane nae afanye mambo yake ya msingi,. Nikaongea na maneno mawili matatu ili binti anielewe anatakiwa kufanya Nini...

Eti Jana amenipigia simu wamerudiana,. Na alivyokua mshenzi asiniambie mda huo wako wote, me nimeongea maneno yote nimemaliza kumbe wananiskia wote na ilikua video call.....

Hivi ujue kusutwa na mwanaume aibu sana, yaani nilijiskia kufedheheka, mwili mzima baridi, eti naambiwa me Kwa maneno yangu ndo nilisababisha wao wasiwe pamoja,. Eti nimetenganisha familia? Wakati sikua najua kama mda Wana maugomvi Yao binti alikua mjamzito ...

Nakaa nawaza how come amwambie Baby dad wake kwamba mimi ndio nilisababisha ,wakati binti alinifata mwenyewe kuomba ushauri na nikamshauri, . Kama ushauri wangu ulikua hauna maana mbona aliufanyia kazi....

Haya mambo sio ya kunitokea Mimi umri huu... Washenzi kweli hawa
NRNE FOREVER

Achana nao waambie SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWAA
 
Nilisahawah mshauri binti mjamzito ivi alitaka kutoa mimba alifanyia kazi ushauri wangu alivyojifungua mi nikala kona maana mission yangu ilikamilika
 
Me sipendagi kushauri shauri watu,. Sema huyu binti nlikua namuona anazo akili kumbe nae ndo walewale tu
Mwenzako anaogopa kuwa single, kukosa uhakika wa huduma, kudharauliwa na wanawake wenzake, n.k

Kushauri masuala ya ndio inahitaji kipaji toka kwa roho mtakatifu
 
Kuna watu wanapenda vibaya sana, hii ilitukuta maskani. Mchizi wetu alikuwa na mrembo wake na walikuwa kwenye mahusiano muda tu, Sasa siku moja mchizi anatuambia kwenye hayo mahusiano anateseka sana, inshort hajawahi kupewa tunda ikabidi tumshauri achane na yule mrembo na yeye mwenyewe alikubali ushauri wetu.
Baada kama ya siku tatu alikuja yule bint kutuchamba, tena ili kututhibitishia kuwa ile show Ina baraka zote yule bint alikuja na mamake mzazi. Sasa ikawa kama wanapokezana, binti anazisha mamtu anamalizia
Ile siku tulivuliwa nguo na kile kijiwe kilisambaratika.
😁😁😁😁😁Kmmk hiyo sio familia
 
Me nawaambia mkituliza akili muongee...hasa Mume na mke usije dhu utu kuwashauri kinyume au mbali na hapo..
 
Back
Top Bottom