Nimedhalilika ...

Nimedhalilika ...

Ilishanitokea hii,Waliachana baada ya miaka kadhaa mmojawapo akawa anahitaji kurudiana,huyu ambaye alikuwa anaombwa warudiane naye akaniomba mimi ushauri, Ushauri niliompa "wasirudiane" Bahati mbaya wakarudiana na waliporudiana yule aliyekuwa ananiomba ushauri akamwambia kila kitu kuhusu ushauri niliompa, Nashukuru Mungu wameachana tena.
 
Ulichokifanya ni sahihi , kwa sababu tukirudi kwenye uhalisia huwezi kumtetea bwana wake ukamuangamiza rafiki yako 😂😂 rafiki yako mmetoka mbali.

Huyo shemeji ungemchana nae , aache mambo ya kijinga
 
Anyway!
Lipokuja swala la mapenzi, usijichanganye sana na hayo maswala..can you imagine wakati unamdinya hata mchepuko/dem wako unaweza kumwamby tukana wazazi wako, kenge huyo bila aibu unajikuta anatukana matusi kama mwehu!
YOTE KWA YOTE, JITAHIDI KUEPUKA USHAURI WA KIMAPENZI MAANA NI NON PAYABLE JOB!
 
NrNe.....

Wakuu Kuna namna watu wa hii nchi wanajitoaga akili sana..

Mwaka Jana Kuna binti alinifata kuniomba ushauri,. Na Kwa jinsi alivyonihadithia matendo ya My wake nikamshauri kiroho safi aachane nae afanye mambo yake ya msingi,. Nikaongea na maneno mawili matatu ili binti anielewe anatakiwa kufanya Nini...

Eti Jana amenipigia simu wamerudiana,. Na alivyokua mshenzi asiniambie mda huo wako wote, me nimeongea maneno yote nimemaliza kumbe wananiskia wote na ilikua video call.....

Hivi ujue kusutwa na mwanaume aibu sana, yaani nilijiskia kufedheheka, mwili mzima baridi, eti naambiwa me Kwa maneno yangu ndo nilisababisha wao wasiwe pamoja,. Eti nimetenganisha familia? Wakati sikua najua kama mda Wana maugomvi Yao binti alikua mjamzito ...

Nakaa nawaza how come amwambie Baby dad wake kwamba mimi ndio nilisababisha ,wakati binti alinifata mwenyewe kuomba ushauri na nikamshauri, . Kama ushauri wangu ulikua hauna maana mbona aliufanyia kazi....

Haya mambo sio ya kunitokea Mimi umri huu... Washenzi kweli hawa
Angalau umejifunza kitu so next time huwezi kufedheheka tena.
 
Tunaungana na wewe ingawa inanukia kama chai
20250515_000445.jpg
 
Wakati alinifata mwenyewe kuomba ushauri wangu
Hatutofautiani sana Mimi watu wananiambia niwashauri kuhusu mapenzi, sjui uhusiano, mara akuambir hv mara vile

Mm nshawapiga onyo full stop kuniletea habari za uhusiano wao sihitaji na wamepunguza
 
Kuna watu wanapenda vibaya sana, hii ilitukuta maskani. Mchizi wetu alikuwa na mrembo wake na walikuwa kwenye mahusiano muda tu, Sasa siku moja mchizi anatuambia kwenye hayo mahusiano anateseka sana, inshort hajawahi kupewa tunda ikabidi tumshauri achane na yule mrembo na yeye mwenyewe alikubali ushauri wetu.
Baada kama ya siku tatu alikuja yule bint kutuchamba, tena ili kututhibitishia kuwa ile show Ina baraka zote yule bint alikuja na mamake mzazi. Sasa ikawa kama wanapokezana, binti anazisha mamtu anamalizia
Ile siku tulivuliwa nguo na kile kijiwe kilisambaratika.
 
AHAHAHAHHAHAHA kama nawaona!
 
Back
Top Bottom