Nimechanganyikwa naomba mawazo yenu wanajf wenzangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimechanganyikwa naomba mawazo yenu wanajf wenzangu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by nnunu, Apr 30, 2011.

 1. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  NAHISI DUNIA IMENIGEUKA,
  muda wangu wote,juhudi zangu zote,ndoto zangu zote,
  maisha yangu yote naona kama ndiyo yamefikia mwisho.

  Nilifanya mtihani wa kidato cha sita kama private candidates,
  lakin NIMEFELI nina Dvn four (4) ya 18,GS-s,hst f, kisw -D,na eng f.
  ndoto za kwenda chuo kikuu zimeyeyuka ghafla,
  naona giza totolo mbele yangu,ila naamini kupitia,
  hapa JF naamini wadogo zangu,wanangu,wajukuu zangu,
  pamoja na wakubwa wenzangu mtanisaidia kimawazo nini cha kufanya.
  mimi napenda sana nikasomee CBE mambo procurement kwa kuanzia na
  diploma je ntaweza kufanikiwa kupata nafasi.Form nimeshachukua ila
  sijarudisha,wasiwasi wangu je nitaweza kupata nafasi??.
  matokeo ya form four yana hst-c,kiswa-c,eng-b,geo-d,
  civic-d,. Yataweza kunisaidia kuingia diploma??.

  Sitaki mkopo najilipia mwenyewe kwa sababu mimi siyo mwajiriwa,
  nimejiajili mwenyewe na vibiashara vyangu vyenye uwezo wa kuniwezesha,
  kumudu gharama zote kipindi chote cha masomo.
  Sijapeleka jukwaa la elimu kwa sababu kule kuna wachangiaji wachache,
  tofauti na huku ambako naamini nitapata mawazo mengi sana na yenye kunifaa.
  Nawaomba muwe wa wazi tu,kama inawezekana sawa na kama haiwezekani niambieni pia. Ukweli wako ndiyo mafanikio yangu.

  Samahani kwa maelezo marefu.
   
 2. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 875
  Trophy Points: 280
  Pole sana NNUU!
  Huna ya kukata tamaa kiasi hicho, sidhani kama kufeli kwako masomo ndiko kufeli maisha, ninachoamini maisha yataendelea na madamu maisha yanaendelea u can try again and again ukiamini kuwa kwa juhudi ufanyazo mwisho wa siku utafikia lengo lako.

  Kuhusu CBE jaribu kupata ushauri kutoka kwao nafikiri itakuwa ni njia nzuri ya kuwa sure na kuokoa muda pia!!

  Pole sana huna haja ya kukata tamaa na kupoteza matumaini kiasi hicho!!!!
  Mungu akutangulie usifikie maamuzi ya kuutesa Moyo wako!!!
   
 3. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 645
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kama umechukua form zijaze kisha rudisha kisha subiri majibu , usikate tamaa. tuma vyuo vingine pia.
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Unajua mkuu si kwamba wanaofeli huwa ni vilaza, hasha. Kufaulu inategemea pia na utulivu wako unapofika chumba cha mtihani. Usikate tamaa kwani bado una 99% za kufaulu maisha. Evidence umeshaionesha kwa kutaka kusoma cbe.
  Kuhusu cbe nenda kaongee nao, japo kuna uwezekano mkubwa wa kuanza ngazi ya cheti, ukifaulu unaenda diploma.
   
 5. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  asante sana kwa kunipa moyo,
  nitakwenda jumatatu nikaonane nao.
  Shukurani sana.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huna haja ya kukata tamaa, nenda huko CBE utapata ushauri zaidi!
   
 7. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ASANTE,
  NI CHUO KIPI KINGINE KILICHOPO HAPA DAR
  KINACHOTOA HIYO KOZI YA PROCUREMENT??,
  Siwezi kwenda nje ya mkoa ksb nina mtoto mdogo,
  siwezi kumwacha,ila kwa hapa DAR naweza kuhudhuria,
  vipindi bila matatizo yoyote.
  samahani kwa usumbufu.
   
 8. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  asante, kwa ushauri wako,
  pia upo sahihi kabisa,
  umakini wakati wa kufanya mtahani wowote ni muhimu.
   
 9. SAWEBOY

  SAWEBOY JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Unajua kufika chuo kikuu kuna njia nyingi sana mpendwa, kama lengo lako ni kufika chuo kikuu na kuendelea zaidi ya hapo basi jaribu njia mmbadala ambayo wengi ninaowafahamu mimi wamefanikiwa.

  So long as una uwezo wa kujilipia ada as you said, na pia naona matokeo yako hapo una : D = ya kiswahili, na S- ya GS, basi naomba uni- PM ili tuweze kujadilina vema na kukupa ushauri wa njia ya kupita na hatimaye ndoto zako kuweza kutimia kuendelea na masomo zaidi.

  Kuhusu CBE kuna competition sana siku hizi na hawachukui watu wengi so unaweza kuta -uka-apply then baadae ukakosa na ukakata tamaa ya kusoma tena.

  NB: Hata kama kuna mdau mwingine mwenye tatizo kama la huyu ndugu, basi ani-PM immediately na kuona kama anaweza fanikiwa au kuchange field na baadaye kujiendeleza zaidi kwa field uipendayo.
   
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  pole mkuu,nimefurahi kwamba umri umeenda lakini bado una mikakati chanya ya kujiendeleza kimasomo, anyway kiukweli ukiwa na D-tano za form 4 unaruhusiwa kuchukua hiyo kozi yako(ingawa sasa ina compition kiaina) kwa ngazi ya cheti mwaka mmoja, ukifaulu vizuri una tena chance ya kuchukua diploma same field...na baada ya hapo unasongesha. Sasa wewe kwa matokeo ya form 4,tayari una C-2 na B-1 na D-2...so you are qualified for diploma field of 3 yrs. NB, depends on comptition..just try and check it out.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimi mpaka leo hii sijaelewa kabisa curriculum inayotumiwa katika elimu ya upili Tanzania. Hata text books zinazotumiwa sizijui. Jinsi hata wanavyosahihisha hiyo mitihani sielewi.

  Kwa kifupi mfumo mzima wa elimu uko hovyo na shaghalabaghala kupita kipimo. Labda ni mimi ambaye sikuwa na pay attention darasani....but I think the whole educational system is so jacked up to prepare students to fail.
   
 12. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ASANTE kwa ushauri wako,
  ila jinsi ya kuanza kukuPM sifahamu, ila najua kureply PM tu,
  naomba unipm halafu mimi nitareply.
  samahani kwa kukusumbua.
   
 13. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ASANTE SANA KWA MAONI YAKO,
  nikienda kurudisha form jumatatu itabidi nikawaulize,
  then nione ntajibiwa nini.
  Nimeileta hapa jukwaani kabla sijarudisha form,
  ili niweze kupata mawazo zaidi, kama huu wa kwako,
  na mingine mingi zaidi.
  asante sana.
   
 14. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,223
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe wa pm unataka malipo ya ziada?
  kwanini usiwe muwazi kwa kuweka mawazo yako hapa tuyapime?

  Unataka uandikiwe PM ilimawazoyako yaonekane yameenda shule kumbe ukiyaweka wazi yatakua ya kitoto.

  Usitumie advantage ya watu wenye shida kuwalisha mawazo ambayo hayajachujwa.
   
 15. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  asante katavi,
  nimekuelewa ntaufanyia kazi ushauri wako.

  naona hata Like nayo imetolewa nashindwa kubofya,
  inabidi nijibu kwa njia hii tu.
  asante.
   
 16. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Kaka jambazi ASANTE sana kwa mawazo yako,
  hapo kwenye kukolezwa rangi napo pana maana sana tena sana,
  ndiyo Tanzania yetu hii kila kitu watu wanageuza dili.

  Lakin ningekuwa najua jinsi ya kuanza PM ningempm ili nimsikilize ushauri wake,
  labda unaweza kunisaidia japo angeweka hapa labda ungeweza kuwasaidia wengi,
  labda kuna wengine wenye tatizo kama langu japo hawajaweka wazi.
   
 17. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndiyo Tanzania yetu hii Nyani Ngabu,
  Laiti wangekuwa jinsi wengine tunavyoumia kwa ,
  kujituma angalau tujielimishwe ili tusiachwe nyuma na wasomi,
  wenzetu wala wasingekuwa wanafanya mchezo na elimu.

  Bado hatuna jinsi tutapambana hivyohivyo japo,
  IMENIUMIZA KUPITA KIASI.
   
 18. T

  Tall JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.maisha siku zote yana changamoto.
  2.changamoto zisikukatishe tamaa bali kukupa ari ya kusonga mbele.
  3.nenda chuo cha uhasibu kurasini,mwone mkuu wa idara ya procurement mama mavis ni mtu mzima.utatoka unachekelea.
   
 19. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndugu
  usikate tamaa yote maisha
  wasiliana na saweboy akupatie njia mbadala
  pamoja na michango mingine ya wadau
  Mungu awe pamoja nawe
  ninaamini siku moja utafika pale unapohitaji kuwa
   
 20. Mama Brian

  Mama Brian JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usijikite CBE tu pekee jaribu na vyuo vya ualimu pia, watu huwa wanadharau ualimu lakini unalipa sana, usikate tamaa. manake huko CBE utamaliza ajira pia matatizo.
   
Loading...