Rais wa TLS, Fatma Karume anena haya baada ya kutolewa kwenye ratiba ya kuzungumza siku ya Sheria Tanzania

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Rais huyo wa TLS amegusia haya katika hiyo barua yake;
Nilitamani kuhudhuria kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanasheria, japokuwa nilipokea kwa njia ya mdomo katazo la mimi kuhudhuria au kuhutubia siku hiyo itakayofanyika tarehe 6/1/2019. Mwaka 2018 Mhe. Tundu Lissu alishindwa kuhudhuria kutokana na hali ya ugonjwa na alikuwa anaendelea na matibabu hivyo nilitamani mimi niweze kuhudhuria maadhimisho haya.

Anaendelea kusema, niliandaa hotuba inayoendana dhana ya sherehe za mwaka huu na niliiwasilisha kwa sekretarieti ili niweze kupata maoni kutoka TLS, mnamo tarehe 1/2/2019 mahakama iliomba kupitia hutuba hiyo na nilituma kwa njia ya baruaa pepe kwa kutimiza wajibu wangu.

Leo nimepokea barua inayosema mimi, TLS na Mwanasheria mkuu wa Serikali(Nahisi ni kwaajili ya kuweka tu usawa) hatutoweza kuhutubia UMMA kutokana na ufinyu wa muda. Haijawahitokea kwa muda wa zaidi ya miaka 20 kwenye historia ya kuwepo kwa TLS kushindwa kuhutubia kutokana na ufinyu wa muda ila hakuna lakushangaza kwenye ilo kutokana na hali ya kisiasa iliyopo Tanzania kwa sasa. Hili linaloendelea lisiwakatishe taama na mkae mkijua kwamba hali hii ni kwa muda tu.

Tafadhli ieleweke kwamba TLS ni chombe kinachoheshimu demokrasia na hivyo kama kuna mwanachama yeyote atakayehitaji/ataona kuna umuhimu wa kuhudhuria maadhimisho hayo anaruhusiwa.

Nawatakia Maadhimisho mema ya Siku ya Wanasheria.

=================================================================



TLS.PNG



Hotuba ya Rais wa Chama cha Wanasheria TanganyikaBibi Fatma Amani Karume, iliyokuwa isomwe
(Dar es Salaam Tarehe 06 Februari 2019)

Mheshimiwa Dr.JohnPombe Joseph Magufuli,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Prof. IbrahimJuma, Jaji Mkuu,
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Tanzania,
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani,
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu,
Waheshimiwa Wasajili wa Mahakamaya Rufani na Mahakama Kuu,
Waheshimiwa Mahakimu,
Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
NduguWanasheria wasomi wenzangu,
Mabibi na Mabwana.

Tangu utotoni nimefundishwa kwamba vilivyokuwemo kwenye mkoba wa mwanamke ni siri yake. Bibi, Mama au Shangazi akikutuma kumletea mkoba wake, kwetu ilikua marufuku kuchungulia ndani. Leo, nitaivunja miiko kwa kuwaeleza vichache ninavyobeba kwenye mkobawangu: miwani, maana sioni vizuri, rangi ya mdomohii ni muhimu, kipepeo, Dar kuna joto kali, na wanaonijua vizuri wanafahamu ukikuta pesa kwenye mkobawangu ni bahati. Lakini sitoki bila ya kubeba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sitaweza kugawa kila kilichopo ndani ya mkobaisipokua matamshi ya Katiba. Na ningependa kuanza hotuba yangu kwa kuwakumbusha Utangulizi na Misingi ya Katiba yetu. Katiba inaanza na utangulizi ufuatao:


“Kwa kuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmina kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya UHURU, HAKI, UDUGU na AMANI:
Na kwa kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge enye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyokuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:
Kwa hiyo basi, Katiba hii imetungwa na Bunge Maalum la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwana Serikali yenye kufuata misingi ya Demokrasia na Ujamaa. “

Misingi ya Katiba yetu ni UHURU,HAKI,UDUGU,AMANI,DEMOKRASIA NA UJAMAA. Ni muhimu pia kutambua kuwa neno Demokrasia limetajwa mara mbili katika utangulizi huu. Na waliotunga Katiba walielewa kwamba Mahakama huru inayotoa haki bila woga wala upendeleo wowote inahakikisha haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa na ina umuhimu wa pekee kwenye kulinda misingi ya katiba.

Nimeelezwa kwamba uongozi wa Mahakama umeamua kauli mbiu yamwaka huu kuwa ni : “Utoaji wa Haki kwa Wakati: Wajibu wa Mahakama na Wadau”, na nimeambiwa nijikite kwenye mada hiyo .

Nitaanza na Wajibu wa Mahakama na nitamalizia na wajibu wa wadau.


Wajibu wa Mahakama

Wajibu wa Mahakama umewekwa wazi kwenye Katiba yetu.

Ibara 107A (1) inasema,

“Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utowaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama”.

Ibara ya 107A(2)(b) ya Katiba inaeleza

“Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani-

a)Kutenda haki kwa wote bila ya kujaliHali ya mtu,kijamiiau kiuchumi;​
b)kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;​
c)kutoa fidia ipasavyokwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujib wa sheria mahususi ilioyotungwana Bunge;​
d)kukuza na kuendeleza usuluhishi bainaya wanaohusikakatika migogoro.​
e)kutenda haki bila ya kufungwa kupita kiasi na masharti yakiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.​

Ibara 107B

“Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale ya sheria za nchi.”

Kwa hiyo wajibu wa Mahakama ni kutoa HAKI.

Hadithi hadithi...........

Hapo zamani zakale, kulikua na familia ina baba, mama na watoto watatu, wawili wakiume na mmoja wakike. Watoto wakiume wakaoa wakapata watoto. Mtoto wa kike naye akaolewa lakini hakupata bahati ya kuzaa. Kwa furaha kubwa Baba na mama wakawa Babu na Bibi, na mtoto wa kike akawa Shangazi. Muda ukapita, Babu na Bibi wakafariki na wakaacha mali kama mashamba na nyumba. Familia ikakaa kikao na wakaamua msimamizi wa mirathi awe Shangazi. Mirathi ikafunguliwa, na Shangazi akawa msimamizi kwa hiyo mashamba na nyumba yakaingizwa kwenye jina lake kama msimamizi wa mirathi, lakini kaka zake wawili wakachukua na kuendeleza mashamba ya vijijini naye akawa anaishi kwenye nyumba ya Babu mjini. Maisha yakaendelea kama kawaidabila ya ugomvi wowote maana familia hii ilikua inaupendo sana. Kila wakivuna shambani kaka zake wakawa wanamtumia mazao Shangazi mjini naye Shangazi akawa anawasimamia kazi zao za kisheria huko mjini.

Muda ukapita, wale kaka wawili nao wakafariki, mume wa Shangazi naye akatangulia mbele ya haki na Shangazi akabaki peke yake kwenye nyumba ya Babu mjini. Siku moja Shangazi akatuma ujumbe kijijini kwa watoto wa kaka zake waje haraka kumuona. Walivyosikia wito wa Shangazi, wale watoto wakaendamjini kumtembelea. Kufika wakamkuta Shangazi anababaika kwa huzuni. Akawaeleza kwamba katapeliwa. Wakamuuliza “Umetapeliwavipi?” Akasema “Tangu alivyofariki mume wangu nimejisikia mpwekesana. Sasa kuna dada, aitwaye Mtu Mwema akawa ananitembelea mara kwa mara. Siku moja nilpokua ninaumwa akanipa karatasiili niweke sahihialinilaghai kuwa ninaweka sahihi kwenye makaratasi ili kumuwezesha yeye anisimamie kupata matibabu. Mimi nikatia sahihi. Juzi nilikua natafuta hati ya hii nyumba na sijaiona. Naogopa Mtu Mwema kanitapeli”. Akaanza kulia. Watoto wakatafuta mwanasheria naye alipofanya utafiti Wizaraya Ardhi, huyomwanasheria akakuta nyumba ya babu iko kwenye jina la Mtu Mwema kwa madai kapewa na Shangazi out of love and affection “kwa UPENDO”.

Mwanasheria msomi akatoa vitabu vyake, akatoa sheria zake akasoma. Alivyomaliza akawaambia watoto “Hii kesi ni rahisi sana maana kwenye sheria yetu, kifungu cha 25(1)(a) cha Sheria ya Mikataba huwezi kumpa mtu nyumba aliyekuwa sio ndugu yako wa damu au ndugu wa kupitia ndoa yako kwa UPENDO eti bila ya kulipwa senti moja. Mkataba huo unakua haramuna hautokubaliwa na Mahakama”. Akawaeleza watoto kwamba hiyo sheria iko ili kuwalinda watu wasitapeliwe. Watoto wakamwambia Shangazi asijalimaana sheria iko upande wake na kuna Mahakama itakayotiina kutoa haki. Kesi ikafunguliwa. Ikaenda miaka 3, jaji akahamishwa. Kesi ikasimama miaka 2 maana mahakama ikawa haina majaji wakutosha. Miaka 5 baada ya kesi kufunguliwa ikapata jaji mpya. Kesi ikaendelea.

Baada ya miezi michache, mara Shangazi akafariki. Kesi ikasitishwa tena maana sasa haiwezi kuendelea mpaka watoto wafungue mirathi ilibaada ya kuteuliwa na mahakama msimamizi wa mirathi ya Shangazi aendeleena kesi. Watoto wakafungua mirathi, Mtu Mwema akapinga mirathi akataka yeye awe msimamizi wa mirathi. Kesi ya mirathi ikaenda miaka 5. Jaji wakwanza kwenye kesi ya mirathi akahamishwa akaingia jaji mwengine. Alivyoingia jaji huyu Mtu Mwema akatoa pingamiza yake ya mirathi ya Shangazi, na Mahakama ikaamua mtoto wa kiume asimamie mirathi ya Shangazi, huku ikamlaani sana Mtu Mwema kwa kuchelewesha mirathi ya Shangazi pasipo sababu. Huyu mtoto akachukua hati yake ya usimamizi wa mirathi ya Shangazi akaendamahakamani ili kuendelea nakesi ya awaliya Shangazi dhidi ya Mtu Mwema. Kufika Mahakamani Mtu Mwema akaweka pingamiza kusema kama Kesi ya Shangazi itupwe kwa sababu imechelewa sana kuendelea.

Pingamizilake likakubaliwa na kesi ikatupiliwa mbali baada ya miaka 17. Mtoto akaamuakukata rufaa. Alipopewa makabrasha kutoka mahakamani akakuta kuna nakalaza Ushahidi hajapewa. Alipouliza akaambiwa na Msajili makabrasha ya Ushahidi yamepotea. Miaka 15 ikapita bado kesi haijakamilika, makabrasha ya Ushahidi yamepotea mahakamani, mtotonae kazeeka na kapata mshtuko wa moyo.

Sasa tujiulize kesi kama hii inaweza kutokea kwenye nchi yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo na kutochelewesha haki bila ya sababu zamsingi?

Kwa maoni yangu, na naamini mtakubaliana na mimi kuwa kesi kama hii haiwezi kutokea kwenye Mahakama inayotekeleza majukumu yaliyoko kwenye ibara ya 107(A) ya Katiba yetu. Kwanza kwa sababu (1) Mahakama yetu inatakiwakutoa HAKI; (2) kutochelewesha utoaji wa Haki bila ya sababu ya kimsingi na(3)pia kutenda haki bila kufungwa kupita kiasi na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.

Majukumu ya Mahakama yetu kwa mujibuwa Katiba yetu ni utoaji wa HAKI na si USIKILIZAJI wa kesitu.Hapo tuelewane kabisa. Haki ya kusikilizwa kesi yako inamadhumuni yakuhakikisha kuwa unapata USAWA MBELE YA SHERIA na si kuhakikisha unapata HAKI mbele ya sheria.Haki inapatikana pale Mahakama itaendeshwa na watu wenye uwezo, uzoefu, weledi, maadili, uhuru wa fikra, ambaohawana uoga na wanaoheshimu matakwa ya Katiba yetu. Kusikiliza kesi na kutoa maumuzi ni rahisi sana, na kila mtu anaweza kufanya hivyo. Lakini kusikiliza kesi na kutoa maamuzi ya haki ni vigumu maana inahitaji, KNOWLEDGE, EXPERIENCE, INDEPENDENCE, A SENSE OF DUTY, A CALLING AND FEARLESSNESS.

Haki zawananchi si usikilizwaji wa kesi zao tu na haki ya kukata rufaakwamaana kesi inaweza kusikilizwa, kesi inaweza kukatiwa rufaa bila ya HAKI kutendeka. Kwa mujibuwa katiba yetu majukumu ya Mahakama ni UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI.Huwezi ukawa mwoga na hapo hapoukatoa Haki. Huwezi ukaweka mbele maslahi yako na ukatoa Haki. Utabaki na woga tu lakini Haki (Justice) itakua ndoto.

Ili tuelewe umuhimu wa Katiba ningependa kutoa mfano mdogo tu. Kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway, vipimo baina ya vyuma vya reli vitabaki 4ft 8 ½ inchau 1,435 mm kutoka Dar mpaka Rwanda. Hii haiwezi kubadilika hata kama reli inapanda au kushuka mlima. Lakini mabehewa yanaweza kubadilika. Unaweza kuwa na behewa la kubeba mizigo, behewa la kubeba wanyama, behewa la kubeba mafuta, behewa la kubeba watu daraja la kwanza na behewa la kubeba watu daraja la mwisho ilimradi magurudumu ya mabehewa ni ya kutembea kwenye reli ya standard gauge. Ukiweka behewa lenye magurudumu makubwa au madogo kuliko ya standard gauge, behewa litapinduka na watu watajehuriwa. Ili standard gauge ifanye kazi ipasavyo, lazima magurudumu ya mabehewa yote yafuate muundo wa standard gauge.

Katiba ni reli yetu ya Standard Gauge, na kazi ya Mahakama ni kuhakisha kwamba mabehewa yote yanayowekwa kwenye reli yamefuata muundo wa Standard Gauge. Siku Mahakama ikiacha kufanya hiyo kazi kwa umakini na bila ya uoga, watu wataathirika. Ina maana kwamba Mahakama lazima pia ijitathmini yenyewe. Ijiulize mara kwa mara, kweli tunafuata Katiba ipasavyo au are we only paying lip service to our constitution? And if we are paying lip service who are the beneficiaries of this lip service? Is it the people of this country or our own comfort? These are hard questions to ask of oneself and harder still is the ability to answer these questions truthfully. A judiciary that dismisses an allegation from the Bar that its conduct contravenes article 107A of the Constitution by positing “You are using a hammer to hit a fly” fails to understand that every constitutional transgression is important because it does not matter if the wheels on the wagon for the standard gauge are 2 mm off or 10 m off, so long as they are off, they will not run smoothly on the Standard Gauge. And so it is with our country. Every transgression of the Constitution is important and must be checked if we are to have a country that functions on the rule of law and not the rule of fiat.

Sasa nirudi kwenye ile hadithi yangu ya Shangazi. Nikisema hiyokesi imetokea hapa Tanzania mtaniamini? Kwa hao mnaoniamini basi inamaana kwamba mnaelewa udhaifu wa mfumo wetu wa utoaji haki, na kwa wale msioniamini, hamuelewi udhaifu huu na hamuwezi kuubadilisha mfumo wetu kamwe, maana hamuamini.

Hio kesi imetokea hapa Tanzania na baada ya miaka 15 bado iko Mahakamani. Ninangojea Mahakama iyatafute makarabasha. The heroes of my story are the family who still believe in our justice system and are still prepared to keep fighting for justice and not merely for the right to be heard and the right of a appeal.

Nisingependa kumaliza bila ya kugusia uendeshaji wa kesi za jinai Tanzania. Sisi Wanasheria tunaona huzuni sana namna criminal justice system inavyotumiwa kuonea na si kuendesha mashitaka dhidi ya watuhumiwa. Watu wanakamatwa na wanawekwa ndani bila ya dhamana wakati upelelezi wa kesi haujakamilika. Nina maswali mawili tu ya kuuliza: Kama upelelezi haujakamilika unauhakika gani kwamba huyu mtu ana kesi ya kujibu? Kama nitaendelea na mfano wangu wa Standard Gauge, Katiba yetu ya 1977 na mabadiliko yote yaliyofanywa kwenye Katiba hiini Kama mfumo mpya wa reli. Tujiulize kweli kukamata watu na kuwaweka ndani bila ya haki ya dhamana ni jambo linaloweza kuvumiliwa kwenye mfumo wa Katiba yetu yenyeBill of Rights?

Lingekuwa behewa, hili ni la Standard Gauge au tumeliacha behewa lililoundwa kutembeakwenyereli nyingine litembeekwenye reli yetu na kila likitembea linaathiri wananchi? Tujikumbushe kwamba non-bailable offences zilikuwepo kwa capitaloffences only hata kabla ya Katiba ya 1977 ninayoifananisha na ujengaji wa Standard Gauge ya Katiba yetu. Katiba yetu imetambua haki na wajibu muhimu wa wananchi (Bill of Rights), chakusikitisha ni kwamba badala ya makosa yaliyokuwa hayana dhamana kupunguzwa, yanazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda japokuwa Haki na wajibu Muhimu wa wananchi bado unatambulika na Katiba yetu.

Tumefika mahala ambapo makosa ya kutolipa kodi yanakuwa predicate offences kwa makosa ya utakatishaji wa pesa ambayo hayana dhamana. Kwahiyo mtu akishutumiwa kutokulipa kodi anaweza wekwa ndani bila dhamana kwa kosa la utakatishaji wa pesa. Na ataswekwandani mpaka pale D.P.P atakapoamua kukamilisha upelelezi na kuendelea na kesi. Wakati haya yanatokea, tumesahau kwamba, huyu “mtuhumiwa” ana watoto, ana mke, ana wazazi, ana ndugu na wote wanamtegemea yeye. Siku D.P.P akiamua hataki kuendelea na kesi, “mtuhumiwa” ana tolewa bila ya fidia. Ninajiuliza kweli hii ni HAKI iliyodhamiriwa na Katiba yetu?Kwa fikra zangu, Hapana, hapana na hapana tena.

Kama nilivyosema awali kazi ya Mahakama ni kuhakikisha Haki inatolewa kwa muda muafaka na kwa kuzingatia misingi ya katiba hasa Haki na Wajibu Muhimu wa wananchi. Tusikae tukamlaumu DPPtu, maana yeye hana wajibu wa kikatiba kutoa HAKI. Wajibu huo ni wa Mahakama.Kwa hivyo akishitaki watu wakati upelelezi haujakamilika, akifuta mashitaka baada ya mtu kukaa maabusu kwa miaka 6 akaamuru akamatwe tena pale pale Mahakamani, tunaweza kumlaumu kwa kutokufuata maadili ya Waendesha mashtaka, lakini sisi sote kama wananchi, including DPP mwenyewe, tunategemea Mahakama itende HAKI nahakuna muhimili mwingine utakao pata lawama isipokuwa Mahakama maana ibara 107A (1) inasema,

“Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utowaji haki katika jamhuri ya muungano itakuwa ni Mahakama”. Na wajibu huu haukwepeki.

Ninakwenda Segerea mara kwa mara na ninataka kuwaambia, December 2018, kulikua na watu walioko gerezaniwanaumeni 1,723, kati ya hao waliofungwa kwa mujibu ya hukumu ya Mahakama walikuwa 158 tu nawalioko rumandeni1,565. Upande wa wanawake kulikuwa na walioko gerezani313, waliofungwa baada ya kesi zao kusikilizwa walikua 66 na waliokorumandeni 247. Hiyo ndio hali halisi ya utoaji wa HAKI kwa upande wa kesi za jinai.

Ningependakumalizia naki-joke kimoja, dada yangu mpendwa Balozi Mwanaidi Maajar anapenda kuniambia mara kwa mara.

Siku moja Tembohuko Serengeti kamuona Paa anakimbia kweli huku akichungulia nyuma kila baada ya hatua chache. Tembo akamsimamisha Paa akamuuliza “Kulikoni? Mbona unakimbia kama unafukuzwa?” Paa akamjibu huku anahema “Nasikia wanatafuta mbuzi kwa kosa la money laundering”. Tembo kamtizama Paa kwa mshangao mkubwa akasema “Sasa wewe Paa unakimbia nini? Hujijui kwamba wewe ni Paa sio Mbuzi?” Paa akamtizama Tembo kama vile mjinga kweli akamjibu “Mimi ninajijua kwamba mimi ni Paa, wewe pia unajua kwamba mimi ni Paa, lakini hao wanaotafuta mbuzi wanajua mimi ni Paa? Na kama hawajui itanichukua miaka 20 kuthibitisha mahakamani kuwa mimi ni Paana Siyani mbuzi. Sina muda huo”. Alivyomaliza kusema akaendelea kukimbia kama anakimbizwa na ibilisi. Baada ya muda Paa akatizama nyuma akamkuta Tembo naye anakimbia kama anafuatwa na Israeli.

Wajibu wa Wadau
Sasa ninataka kusemawajibu wa wadau. Ninachukuwa fursahii kuwakumbusha wananchi wajibu wao ndani ya Ibara ya 26 inayosema kama ifuatavyo:

(1)“Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hiina sheria za Jamhuri ya Muungano.​
(2)“Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi”​

Ni wajibu wetu sote kufuata na kuitii Katiba na kuhakikisha hifadhi ya Katiba yetu. Na ni wajibuwetu sote kuilinda Katiba yetuna sheria zetu.

Ninataka kumaliza kwa kumnukuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kotoka Hotuba yake “Nyufa”

“Hatuwezi kuendelea kupuuza Katiba, ndiyo sheria ya msingi; sheria nyingine zote zinatokana na Katiba. Haiwezi kupuuzwa na hatuwezi kuendela na uatratibu wa kupuuza Katiba ya nchi yetu au kuwa na Rais anayeoneahaya kuitetea Katiba naye amechaguliwa kwa mujibu wa Katiba, ameapa kuilinda Katiba hiyo halafu anona haya hawezi kuitetea Katiba hiyo. Mtu ambaye kawezi kuitetea Katiba ya nchi yetu, hawezi kuilinda, hawezi kuisimamia baada ya kiapo, hatufai. Hafai!”.

Ahsanteni.

Fatma Amani Karume
President of the Tanganyika Law Society
2018 -2019
Dar es Salaam 1stFebruary 2018
 

Attachments

  • Hutuba ta Rais wa TLS.pdf
    309.3 KB · Views: 62
Laki Si Pesa,
Nyie watu vichwa vyenu sijui sehemu ya ubongo kumewekwa nini? Hatahudhuria kwa kuwa imesemwa eti hatahutubia kwa kuwa muda hautoshi. ilipopigwa kura kwenye baraza la uongozi la TLS 10/10 walisema wanachama wanaotaka kwenda kuhudhuria waende, 7/10 walipiga kura kuzuia Rais wa TLS asihudhurie sherehe hizo na 6/10 walipiga kura kukaa mbali na sherehe za siku ya sheria nchini.

Sasa kafukuzwa kivipi?
 
Very primitive! As the Americans say, you can take a person out of the bush but you can never take the bush out of him/her.
 
Nyie watu vichwa vyenu sijui sehemu ya ubongo kumewekwa nini? Hatahudhuria kwa kuwa imesemwa eti hatahutubia kwa kuwa muda hautoshi. ilipopigwa kura kwenye baraza la uongozi la TLS 10/10 walisema wanachama wanaotaka kwenda kuhudhuria waende, 7/10 walipiga kura kuzuia Rais wa TLS asihudhurie sherehe hizo na 6/10 walipiga kura kukaa mbali na sherehe za siku ya sheria nchini.

Sasa kafukuzwa kivipi?
Kiingereza ndo tatizo wakiongozwa na baba yao mwenye PhD ya korosho..
 
Nyie watu vichwa vyenu sijui sehemu ya ubongo kumewekwa nini? Hatahudhuria kwa kuwa imesemwa eti hatahutubia kwa kuwa muda hautoshi. ilipopigwa kura kwenye baraza la uongozi la TLS 10/10 walisema wanachama wanaotaka kwenda kuhudhuria waende, 7/10 walipiga kura kuzuia Rais wa TLS asihudhurie sherehe hizo na 6/10 walipiga kura kukaa mbali na sherehe za siku ya sheria nchini.

Sasa kafukuzwa kivipi?
Kura zimepigwa kuamua nini kifanyike baada ya kupokea barua inayotamka wazi hana nafasi ktk shughuli hiyo.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
The Tanzania law society
Hii title inaniacha mdomo wazi tangu lini barua za kiserikali zimeanza kutumia font za aina hii duh! Mnisamehe kwa kukosoa uandishi huu
Unaonekana ulikua kilaza shuleni enzi zako.....sasa TLS ni serikali hadi itumie fonti za serikali?????

Use a little commonsense basi. Au una uoni hafifu ndo mana unataka fonti za serikali
 
Ccm watu wa ajabu kweli fuateni utaratibu hata hili nalo mmeshindwa kutumia busara ,basi nchi mtaiweza kweli au ndio mazingaombwe tu .
 
Kura zimepigwa kuamua nini kifanyike baada ya kupokea barua inayotamka wazi hana nafasi ktk shughuli hiyo.
Siyo hana nafasi, bali hatahutubia, angekwenda na kiti chake kingekuwepo "Hightable". Kama nafasi ni kuhutubia basi swali la kuondolewa nafasi hiyo kwa hoja ya ufinyu wa muda linajitokeza. Ni kweli kila atakayeongea atakuwa na sifa zaidi ya Rais wa TL hivyo kustahili kuongea kuliko Rais wa TLS?

Au cheo chake kuitwa Rais ndiyo kunaleta shida?
 
Siyo hana nafasi, bali hatahutubia, angekwenda na kiti chake kingekuwepo "Hightable". Kama nafasi ni kuhutubia basi swali la kuondolewa nafasi hiyo kwa hoja ya ufinyu wa muda linajitokeza. Ni kweli kila atakayeongea atakuwa na sifa zaidi ya Rais wa TL hivyo kustahili kuongea kuliko Rais wa TLS?

Au cheo chake kuitwa Rais ndiyo kunaleta shida?
Ye ahutubie huko tweeter, Huku kwa watu SMART awaachie wenyewe.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Back
Top Bottom